Mikataba anayoingia Waziri Makamba ina mkono wa mkuu wa nchi? Kwanini hatusikii akiikemea? Wananchi wanabakia kunung'unika Taifa lao kufisadiwa

Haya mauzauza na dili anazofanya January Makamba yanaonyesha wazi kabisa yana ruhusa na mkono wa mkuu wa nchi maana alipaswa kuyazuia na kumtumbua mapema kabisa.
Hii mikataba sio inaandaliwa hapo 'chalinze kwa juu' huyu jamaa atazalisha mikataba ya ajabu kama ilivyokuwa awamu ya 5.
 
Aisee.. niliwaambia watu humu hizi tikitaka wanacheza tanesco sio kwamba hawawezi kudhibiti kukatika Kwa umeme, kuna wanasiasa wanatuletea Mambo meusi.
 

Na ndio maana watu wanapuuza sana ushauri,,,kwasabu wanaupata Free...
 
Takwimu zilizotolewa zinasema kwa miaka 10 ya Awamu ya 4, Kikwete aliongeza deni kwa Trilioni 23.
Na kwa miaka 5 ya Utawala wake, Magufuli aliongeza deni kwa Trilioni 29.
Tena kwa mikopo umiza.
Wewe unasema hakukopa zaidi ya Kikwete. Naomba ufafanuzi tafadhali.
 
Tulieni nchi ifunguliwe 🤣🤣🤣

Meko aliifunga hii nchi 🤣🤣🤣
 
Unaweza ukaniambia ni wapi kwa maana y anchi ama sehemu ambako hakuna hay Mambo mkuu..
Kama unazungumzia wizi, rushwa and the like, kila mahali yapo lakini kuna kuzidiana! Inawezekana kuzidiana kutokana na moral obligations au kuzidiana kutokana na taasisi zilizo sehemu mbalimbali zilizowekwa kupambana na ufedhuli huu!
 
Hiyo comment ya mdau kuhusu kikwete inahusiana vipi na kutetea legacy?
Sasa habari za JK zimetokea wapi wakati tunazungumzia issue ya taasisi za serikali kuajiri foreign legal firm?
 
Yaani wewe unadhani Waziri ataingia mkataba bila Attorney General na Cabinet kujua? Au umesahau swali ambalo Lowassa alimuuliza Kikwete kuhusu Richmond, "Ni kitu gani nilifanya hukujua?"
 
ushauri!!!!,kwa hiyo nch hii,kuanzia tanesco wote na mi PhD yao ,ni vilaza wote!!!? we can't be serious!!
 
Kwahiyo ukishaenda kusoma Aberdeen University ndo tayari unakuwa mtalaamu wa masuala ya mafuta na gesi, especially the legal side of the industry? Badala ya kujibu hoja unamwaga mapovu!!

Tatizo la watu aina yako, mtakuja hapa kumwaga povu kwa kila jambo ambalo mnaamini JPM hakufanya kwa sababu mnaamini ambacho hakufanya yeye ndo SAHIHI!

Mkuu Stroke,

Nilikuahidi kwamba ningerudi tena baadae nikishapata muda wa ku-research kidogo....

Man, tuhitimishe bila kupoteza muda kwa kusema yafuatayo...

Tutupo hapa JF pamoja kwa muda mrefu na tunafahamiana misimamo yetu!

Ingawaje hata nikisema bado unaweza kubisha but we both know kwamba, wewe Stroke, na hata Mleta Mada Mkuu Idugunde, nyinyi na hata huyo Kilatha niliyem-quote hapo juu lazima MTAPINGA jambo lolote mnaloamini JPM hakulitaka hata kama hamna taarifa kamili ikiwa kweli hakulitaka au vipi!

Now , let's cut to the chase, once and for all. Baada ya kuchunguza, nimegundua tenda kuhusu kuajiri a foreign company ilitangazwa wakati wa Mtukufu Mnayeamini hana makando kando yoyote, na ndie Mzalendo Namba 1 kwenye taiafa hili:-


Sasa je, ina maana Serikali ya Mzalendo John Pombe nayo haikuwaona makumi ya Watalaamu wenye uwezo wa kuishauri GNT?!

Na hata Wataalamu wa Sheria wenyewe, tena critic kama Fatma Karume, nao wanasema:-



Hivi unataka kusema wewe na mimi tuzifahamu corporate law firm Bongo kumzidi Fatma!! Na kwa alivyo Fatma, hapo kakosa cha kukosowa lakini akaona asitoke hivi hivi ndo maana akazungumzia suala ikiwa Public Procurement Act imefuatwa... nami namuunga mkono ingawaje kwa doc hiyo ya TPDC hapo juu, inaonekana ilifuatwa at least kutangaza open tender!

Nami narudia kama nilivyosema hapo awali: TUSIJIDANGANYE, HATUNA WATAALAMU! Hii ni zaidi ya mtu kuwa na L.L.B, L.L.M, and PhD ya Sheria!

Na hata hilo suala la software ambalo mnapenda sana kulizingumzia kirahisi rahisi tu, mosi ni Tanzania-Zambia Transmission Interconnector (TAZA) Project, inayofadhiliwa na World Bank, na tenda yake ilitangazwa enzi za huyo huyo!


Stay blessed y'all... nimesha-conclude mjadala kwa upande wangu vinginevyo mtu aniwekee profile ya legal firm kutoka Tanzania inayofanana angalau kwa 25% TU kulinganisha na ile profile niliyoiweka Baker & Bottis!! Au aniwekee profile za Wanasheria Wazalendo wenye uzoefu in oil and gas industry lakini kinyume cha hapo tutakuwa tunaendeleza league isiyo na tija!!
 
Kumbuka huwezi kupewa kazi yeyote serikalini bila 10%.
Hapo watu wanacheka tu.
 
Baada ya kuchunguza, nimegundua tenda kuhusu kuajiri a foreign company ilitangazwa wakati wa Mtukufu Mnayeamini hana makando kando yoyote, na ndie Mzalendo Namba 1 kweny
Unaweza kufafanua kwa nini tenda hii ime"stall" toka 2018 lakini imeweza kuwashwa sasa wakati usiyeamini alikuwa mzalendo hayupo? Najaribu kuwa objective katika suala hili.
====
Lile la kuhusu maana ya "bunge kuisimamia serikali" nina imani bado unalifanyia kazi, Mkuu. I trust that you will be back to the matter for me.

Regards,
TUJITEGEMEE.
 
Nini kilisababisha project hii isimame mpaka sasa ilivyofufuliwa upya??
 
Kwamba watu siriaz hawapo Tanzania na hawajazaliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…