Mike Pompeo afanya ziara ya hasira Israel, atoa ya moyoni

Mike Pompeo afanya ziara ya hasira Israel, atoa ya moyoni

Hawana mtetezi kivipi?
Huujui usemi wa mtegemea cha nduguye hufa masikini?

Hao ndugu zao genetically ni waarabu wenzao na sio wewe mtu mweusi.
Kweli Mkuu, hata Wenyewe wanajiita mabinami,hata lugha zimefanana

Lakini kiukweli Muisrael anamuonea sana Mpalestina,akisaidiwa na Mmarekani..

Mpalestina hana mtetezi,Majuzi tu Warabu wa middle East,Qatar,Baharain, Sudan na wengine wanafatia wamefanya ushirikiano wa kibalozi na Israel..

Taifa teule limekuwa taifa kamdamizi wakisadiwa na Mataifa makubwa..
 
Wapalestina wamatumiwa sana kwa maslahi ya wengine hasa viongozi wao ambao wamewafanya mtaji, hakuna namna ya wao kufanikisha agenda yao, ni bora wakubaliane kufuata mipaka iliyo kwenye ramani za mwanzo kabisa ambayo mataifa mengi wanaridhia na wawafanye Israel and western country kuwa washirika wataendelea na kupata amani, Wajue wafandhili wao walikua wanategemea mafuta na ndani ya miaka 20 ijayo bidhaa hii huenda itakua haina samani sana kwenye dunia kwani matumizi yanapungua na nchi nyingi zinagundua mafuta, hivyo wafandhili wako kwenye mihangaiko ya kuandaa namna ya kuendesha nchi zao.
Mmmmh! Kibinadamu na kwa fikra za zetu ni sawa mafuta yanaonekana kukosa deal kutokana na technolojia mpya Kama electrical car, nuclear fussion power plant, artificial photosynthesis, sugar cane to ethanol. Lakini Mungu alichowazawadia waarabu hakiwezi kosa thamani wakina elon musk wataweza kuinvent ila kufanya kiwe world wide ni vigumu.
 
Haya sawa najua ni hasira za upande wa pili hata jina lako linasadiki yaliyomo.
Jerusalem was named as Urusalim on ancient Egyptian tablets, probably meaning "City of Shalem" after a Canaanite deity, during the Canaanite period (14th century BCE). During the Israelite period, significant construction activity in Jerusalem began in the 9th century BCE (Iron Age II), and in the 8th century the city developed into the religious and administrative center of the Kingdom of Judah.[17] In 1538, the city walls were rebuilt for a last time around Jerusalem under Suleiman the Magnificent, when it was part of the Ottoman Empire. Today those walls define the Old City, which has been traditionally divided into four-quarters—known since the early 19th century as the Armenian, Christian, Jewish, and Muslim Quarters.[18] The Old City became a World Heritage Site in 1981, and is on the List of World Heritage in Danger.[19] Since 1860 Jerusalem has grown far beyond the Old City's boundaries. In 2015, Jerusalem had a population of some 850,000 residents, comprising approximately 200,000 secular Jewish Israelis, 350,000 Haredi Jews and 300,000 Palestinians.[20][note 4] In 2016, the population was 882,700, of which Jews comprised 536,600 (60.8%), Muslims 319,800 (36.2%), Christians 15,800 (1.8%), and 10,300 unclassified (1.2%).[22]
 
Jamaaa kavumisha alivyoandika alisema kwa kinywa chake. Ila ni maandiko yamesema hivyo ndo maana hiyo Israel haisemagwi vibaya aisee hata makampuni ya muisrael hayapigwa Vita hovyohovyo. Hata huyo Biden hawezi kubadili aliyo yaweka Trump hiyo inchi ni ndogo kuiangalia kwa macho ramanu lakini in reality watu wake wamefanya dunia imekua hivi leo
Aliyesema ni Mungu wa Israel siyo Mungu wangu. Sasa Mungu wa waisrael ulitegemea atasemaje kuhusu wa Israel? Hata Mungu wangu angesema hivyo hivyo juu yangu.
 
Kweli Mkuu, hata Wenyewe wanajiita mabinami,hata lugha zimefanana

Lakini kiukweli Muisrael anamuonea sana Mpalestina,akisaidiwa na Mmarekani..

Mpalestina hana mtetezi,Majuzi tu Warabu wa middle East,Qatar,Baharain, Sudan na wengine wanafatia wamefanya ushirikiano wa kibalozi na Israel..

Taifa teule limekuwa taifa kamdamizi wakisadiwa na Mataifa makubwa..
Ndo hivyo dunia itatawaliwa na wenye nguvu. Sema naskia waisrael walipigwa na wapalestina many years back wakaenda Europe then waliporudi wakatumia ustarabu kanakwamba wanaomba eneo kidogo ko mipaka sahii haieleweki.Hata hivyo imeandikwa hivyo Vita sisi wanadamu hatuwezi kuvimaliza.
 
Aliyesema ni Mungu wa Israel siyo Mungu wangu. Sasa Mungu wa waisrael ulitegemea atasemaje kuhusu wa Israel? Hata Mungu wangu angesema hivyo hivyo juu yangu
Mkuu sijui imani yako ila Kama wewe ni mkristo it means umemkubali yesu alizibeba dhambi zako na kukufanya uwe mrithi Wa taifa teule. Ko mungu wa israel ni mungu wako pia.
 
Hata Quran inatambua kabisa kuwa Israeli yuko kwenye ardhi waliyopewa na Mwenyezi Mungu,Q5:20-21
Ndiyo kusema Wapalestina hawana chao pale!
Kwenye Bible ardhi ya Israel waliyopewa inafika mpka Iraq na Ndani ya mto nile yaani lijipande la Misri. Kma kweli mnafuata vitabu vya dini kwa nni msiende hadi Iraq ambapo mpaka upo Tigris na Euphrates? Ama Biblia ilisema ni palestina tu?

Kingine je kila mtu akiamua kurudi kwenye ardhi yake ya kale nani atapona? Ethiopia wakidai Yemen, Ug waidai Bukoba na Kivu, kenya wadai kipande cha somalia, somalia nao waidai Ogaden kutoka Ethiopia n.k kuna mtu atakubali?

Kingine usichofaham wayahudi walishakuta watu wanaishi hapo, na mind you hawakuua wote so na hta Suleiman alipotaka kuua masalia yao akapigwa laana na Mungu. Je kma kuua wacanaan walilaaniwa why wakiua wapalestina mnadai walibarikiwa.

Naomba ujibu hoja kwa hoja kwa faida ya wasomaji.

NB: Kabla hujajibu hii post naomba umgoogle mtu anaitwa Folke Bernadottw. Ndio mzizi wa huu mgogoro
 
Wapalestina wamatumiwa sana kwa maslahi ya wengine hasa viongozi wao ambao wamewafanya mtaji, hakuna namna ya wao kufanikisha agenda yao, ni bora wakubaliane kufuata mipaka iliyo kwenye ramani za mwanzo kabisa ambayo mataifa mengi wanaridhia na wawafanye Israel and western country kuwa washirika wataendelea na kupata amani, Wajue wafandhili wao walikua wanategemea mafuta na ndani ya miaka 20 ijayo bidhaa hii huenda itakua haina samani sana kwenye dunia kwani matumizi yanapungua na nchi nyingi zinagundua mafuta, hivyo wafandhili wako kwenye mihangaiko ya kuandaa namna ya kuendesha nchi zao.
Sio kweli kuwa mafuta yakishuka thamani watahaha. Hizo nchi ulizotaja zimewekeza kwenye Sovereign Wealth Fund ambapo pesa za mafuta zinaingizwa kwenye skimu maalum ili ziweze kuzalisha pesa kupitia vitega uchumi mbalimbali hivyo hta mafuta yakikauka watakua na hazina ya kuwatosha hadi miaka 100+ bila kuuza mafuta.
TZ pia tunaanzisha SWF ili hta gesi ikiisha iwe na kibubu chake ambacho kinatunza pesa zinazotoka huko. Hivyo hta dhahabu au gesi zikikauka tutakua na alternative funds za kuinvest.
 
Kwenye Bible ardhi ya Israel waliyopewa inafika mpka Iraq na Ndani ya mto nile yaani lijipande la Misri. Kma kweli mnafuata vitabu vya dini kwa nni msiende hadi Iraq ambapo mpaka upo Tigris na Euphrates? Ama Biblia ilisema ni palestina tu?

Kingine je kila mtu akiamua kurudi kwenye ardhi yake ya kale nani atapona? Ethiopia wakidai Yemen, Ug waidai Bukoba na Kivu, kenya wadai kipande cha somalia, somalia nao waidai Ogaden kutoka Ethiopia n.k kuna mtu atakubali?

Kingine usichofaham wayahudi walishakuta watu wanaishi hapo, na mind you hawakuua wote so na hta Suleiman alipotaka kuua masalia yao akapigwa laana na Mungu. Je kma kuua wacanaan walilaaniwa why wakiua wapalestina mnadai walibarikiwa.

Naomba ujibu hoja kwa hoja kwa faida ya wasomaji.

NB: Kabla hujajibu hii post naomba umgoogle mtu anaitwa Folke Bernadottw. Ndio mzizi wa huu mgogoro
Huu mgogoro ni wa kawaida tu,ni mapito tu ya history,,hata waisrael walitawaliwa na wafilist enzi hawajawa taifa,,na hata baada ya hapo,waisrael walitawaliwa na wamisri,waasyria,waaram,wababel,wairan,wagiriki,warumi,waturuki etc,kwa maelfu ya miaka,
Israel iko palestina kwa chini ya miaka 80,,hiki ni kipindi kifupi mno,,miaka 200 ijayo habari itakuwa nyingine kabisa
 
Mmmmh! Kibinadamu na kwa fikra za zetu ni sawa mafuta yanaonekana kukosa deal kutokana na technolojia mpya Kama electrical car, nuclear fussion power plant, artificial photosynthesis, sugar cane to ethanol. Lakini Mungu alichowazawadia waarabu hakiwezi kosa thamani wakina elon musk wataweza kuinvent ila kufanya kiwe world wide ni vigumu.
Hizi bidhaa za madini ya kutoka ardhini ni mipango ya Mwenyezi Mungu kuwarahisishia wanadamu maisha ili wamuabudu kwa vizuri na pia wayafurahie maisha.Hivyo hata uvumbuzi uende mbali vipi utazunguka hapa hapa katika vitu vya asili kabisa siyo vile vilivyokarabatiwa kwa gharama kama miwa kuzalisha umeme au mbegu za nyonyo kutoa mafuta..
 
Trump na pompeo wanamfanya mungu aonekane muongo,
Last time mfalme wa iran,king cyrus alipowatoa waisrael utumwani na kuwarudisha jerusalem na kuwapa fedha za kujenga upya mji wa jerusalem,mungu alimpya mfalme Cyrus cheo cha masiha,
This time arround,Trump alijiita masiha baada ya kukubali jerusalem iwe mji mkuu wa israel,
Mungu wa wayahudi aliwahi kusema,"nitamlaani atakaeilaani israel,nitambariki,atakaeibariki israel,"
Badala ya trump kubarikiwa,amepata mkosi wa kuukosa urais.
Unabii umeshindwa kutimia..
Nakumbuka kelele zilikuwa nyingi.... Mara ooh kaletwa na Mungu, Mara unabii umetimia sijui hekalu litajengwa kipindi cha Trump. Ssa cjui watajificha wapi na unabii feki waliolishana.
 
Nakumbuka kelele zilikuwa nyingi.... Mara ooh kaletwa na Mungu, Mara unabii umetimia sijui hekalu litajengwa kipindi cha Trump. Ssa cjui watajificha wapi na unabii feki waliolishana.
Ndo maana israel hawataki kuuvunja masjid haram ili wajenge hekalu pale,,maana kwa mujibu wa unabii,mwana wa adamu hawezi kuja mpaka ipite vita kuu au armegodon,,sasa nani anataka kufa mapema aziache raha za dunia?.kwa vitu vya kubuni buni..
 
Uko sawa kabisa.Trump na Pompeo kama kwamba wanawahi kupata sifa ya kuwa ndio waliotekeleza ajenda ya siri yenye anuwani ya Makazi ya waisrael Palestina na ardhi ya Golan ya Syria. Biden hatorudi nyuma na atatekeleza ajenda nyengine zilizojificha ndani ya utawala wa Marekani.Historia nayo inamtaja Joe Biden kuwa mkereketwa mkubwa wa Israel kuliko hata Trump.
Yote hayo yanatoa picha kuwa Palestina isiyo na mtetezi hata miongoni mwa ndugu zake kuwa itakuwa imekwisha.Kwa upande wa nguvu zisizo na kikomo za Mwenyezi Mungu na mipango isiyong'amulikaya mbele ya wanaadamu Palestina itakuja kuibuka mshindi na kushinda njama zote za binadamu.
Hiyo ni ndoto unayoota mchana wa jua kali
 
Mkuu sijui imani yako ila Kama wewe ni mkristo it means umemkubali yesu alizibeba dhambi zako na kukufanya uwe mrithi Wa taifa teule. Ko mungu wa israel ni mungu wako pia.
Mimi ni Mkristo lakini kuna mambo mengi kwenye Biblia yamekuwa misinterpreted wa maslahi ya watu flani.
 
Ndo hivyo dunia itatawaliwa na wenye nguvu. Sema naskia waisrael walipigwa na wapalestina many years back wakaenda Europe then waliporudi wakatumia ustarabu kanakwamba wanaomba eneo kidogo ko mipaka sahii haieleweki.Hata hivyo imeandikwa hivyo Vita sisi wanadamu hatuwezi kuvimaliza.
Pale Palestina kuna eneo takatifu lililotajwa kwenye Qur'an ambapo ni kama ngazi aliyotumia mtume Muhammada s.a.w kupanda mbinguni.Hilo linajulikana wazi na waisrael na kwa vile ni watu wa njama kila siku kutaka kushindana na muumba wao wanajaribu kupahodhi ili wajitangazie ushindi mbele ya Allah aliyetukuka.Kama una akili timamu na unajuwa nguvu zake huwezi kupata shaka kuwa eneo hilo hata walizungushie nyuklia na hapo ndani wazuie waislamu wote kuingia hawatoweza kulidhibiti.
Kumbuka jeshi la Abraha lililokuwa na silaha nzito walipotaka kuiteka Alkaaba wasimamizi wa nyumba hiyo walisema wao ni dhaifu hawawezi kushindana na jeshi hilo na wanamwachia mwenyewe alilinde.Hakuna aliyeweza kuingia hapo na wote walipigwa na videge vidogo dogo vilivyotoka jahannamu na askari wote na kamanda wao wakawa kama majani yaliyotapikwa na wanyama..
Hawa wafalme wanaozunguka nyumba ya Alaqsa kama hawawezi kusaidia kuilinda ni hasara kwao na haimahanishi ushindi kwa Israel.
 
Kwenye Bible ardhi ya Israel waliyopewa inafika mpka Iraq na Ndani ya mto nile yaani lijipande la Misri. Kma kweli mnafuata vitabu vya dini kwa nni msiende hadi Iraq ambapo mpaka upo Tigris na Euphrates? Ama Biblia ilisema ni palestina tu?

Kingine je kila mtu akiamua kurudi kwenye ardhi yake ya kale nani atapona? Ethiopia wakidai Yemen, Ug waidai Bukoba na Kivu, kenya wadai kipande cha somalia, somalia nao waidai Ogaden kutoka Ethiopia n.k kuna mtu atakubali?

Kingine usichofaham wayahudi walishakuta watu wanaishi hapo, na mind you hawakuua wote so na hta Suleiman alipotaka kuua masalia yao akapigwa laana na Mungu. Je kma kuua wacanaan walilaaniwa why wakiua wapalestina mnadai walibarikiwa.

Naomba ujibu hoja kwa hoja kwa faida ya wasomaji.

NB: Kabla hujajibu hii post naomba umgoogle mtu anaitwa Folke Bernadottw. Ndio mzizi wa huu mgogoro
Mkuu huyu Folke Bernadott ndiye yule mpatanishi wa Kwanza wa UN kuhusu huu mgogoro aliyeuawa na magaidi wa Israel (Lehi) chini ya Yitzakh Shamir aliyekuja baadae kuwa waziri mkuu wa Israel miaka ya 1980 mpaka kipindi cha vita ya kwanza ya Ghuba?

Kama ndiye yeye sidhani kama ni sahihi kumuita mzizi wa huu mgogoro ila mzizi wa huu mgogoro ni uanzishwaji wa dola ya kiyahudi kwenye makazi ya Wapalestina yaliyokuwa chini ya uangalizi wa Uingereza mpaka mwaka 1948.

Labda tuseme kuuawa kwake kulikwamisha mgogoro huu kupatiwa ufumbuzi kipindi kile ukiwa kwenye hatua za awali.

Ila kumbuka hawa magaidi wa Lehi waliomuua Bernadott walifanya hivyo ili kumzuia kumshawishi Ben Gurion (waziri mkuu wa Israel wakati huo) na UN waridhie pendekezo lake la kuigawa hiyo ardhi, ila hawakujua kama Waziri mkuu Ben Gurion alishakataa pendekezo hilo kitambo.
 
Ndo hivyo dunia itatawaliwa na wenye nguvu. Sema naskia waisrael walipigwa na wapalestina many years back wakaenda Europe then waliporudi wakatumia ustarabu kanakwamba wanaomba eneo kidogo ko mipaka sahii haieleweki.Hata hivyo imeandikwa hivyo Vita sisi wanadamu hatuwezi kuvimaliza.
Jina palestine asili yake ni filstian,,wafilisti,,hawa wafilisti walikuja mwambao wa caanan,miaka ya zamani,ear ancient Egypt kingdom,wakitokea visiwa vya crete,wakapiga kambi miji ya kando ya bahari mfano Gaza,
Baadae walikuja kuwa na nguvu sana wakatawala eneo kubwa,wakati israel inaanza kuwa tawala chini ya mfalme saul,kabla yake walitawaliwa na wafilist,hawa wafilisti waliendelea kuhangaishana na waisrael hata kipindi cha daud,(mind you Daud,siyo historical figure na anaweza kuwa hajawahi kuwepo).
Lakini jina palestine,lilianza kutumika rasmi kama jina la province ya warumi,wakati eneo la caanan lulipoangukia katika utawala wa warumi,
Toka hapo,wakaazi wa caanan,wakaja kujulikana kama wakaazi wa palestine,
Ndo maana kabla israel hawajajitangazia uhuru 1948,hata wayahudi walijulikana kama raia wa palestine,
 
Huu mgogoro ni wa kawaida tu,ni mapito tu ya history,,hata waisrael walitawaliwa na wafilist enzi hawajawa taifa,,na hata baada ya hapo,waisrael walitawaliwa na wamisri,waasyria,waaram,wababel,wairan,wagiriki,warumi,waturuki etc,kwa maelfu ya miaka,
Israel iko palestina kwa chini ya miaka 80,,hiki ni kipindi kifupi mno,,miaka 200 ijayo habari itakuwa nyingine kabisa
Huenda upo sahihi ila sio sahihi sana.

Ina maana Wapalestina inabidi wavumilie miaka 200 ijayo ili wawe taifa? Unajuaje miaka hiyo huenda mataifa mengi yakawa yamekwishaungana kuunda taifa moja?
 
Huenda upo sahihi ila sio sahihi sana.

Ina maana Wapalestina inabidi wavumilie miaka 200 ijayo ili wawe taifa? Unajuaje miaka hiyo huenda mataifa mengi yakawa yamekwishaungana kuunda taifa moja?
Sio lazima wawe taifa,,Tanzania yenyewe miaka 200 ijayo haitakuwa kama hii ya leo,
Populationwise israel inaweza jikuta inamezwa na palestine miaka hiyo,,yaani nature,natural selection ndo itaamua
 
Back
Top Bottom