Mike Pompeo afanya ziara ya hasira Israel, atoa ya moyoni

Sio lazima wawe taifa,,Tanzania yenyewe miaka 200 ijayo haitakuwa kama hii ya leo,
Populationwise israel inaweza jikuta inamezwa na palestine miaka hiyo,,yaani nature,natural selection ndo itaamua
Kwanini ushikilie Israel inaweza kumezwa na Palestina kwani wao Palestina hawawezi kumezwa na Israel?

Angalia wakati huu ardhi ya Jerusalem mashariki,Hebron,ukingo wa magharibi ambayo walowezi wa kiyahudi wamenunua na wanaendelea kununua toka kwa Wapalestina na kuwahamisha kwa nguvu ili kuendeleza makazi yao, utasemaje huenda wakamezwa.
 
Videge vilitoka wapi 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nchi ya ISRAEL ilianzishwa 1948 baada ya kwisha vita vya pili vya Dunia..

Sababu kubwa ya kuanzishwa Taifa la Waisrael ni kutokana na mateso waliyopata kutoka Kwa Hitler

Kwanza ilipendekezwa wapewe Ardhi Uganda,baadae ndio wakapewa Ardhi Palestina

Nchi ya Israel ilianza kupanuka pale Waisrael walipoanza kununua Ardhi kutoka Kwa Wapalestina

1967 Israel ilipigana na Nchi za Kiarabu,vita vijulikanavyo kama vita vya siku sita

Kwa masada wa Mataifa makubwa Israel ilishinda vita vile

Ushindi wa vita vile iliifanya Israel ikombe Ardhi kubwa ya Palestine ambayo hawajairejesha mpaka leo

Cha kushangaza Waisrael wanawafanyia WaPalestina yale yale waliyofanyiwa wao na Hitler
 
Exactly huyo ndio alitoa suluhisho zuri ila wao wakampuuza na ndio maana vurugu mtindo mmoja. Haiwezekani ratio ya ardhi inazidi kupanuliwa kila kukicha. Kma wangekuwa wanataka amani wangerejesha mipaka ya kabla ya 1967 at least za pendekezo la 55:45.

Hata Rabin walimmaliza kisa tu kutafita compromise na wapalestina. Huu mgogoro hautaisha kma wahafidhina hawatakubali kupoteza maslahi yao kwa ajili ya amani ya kudumu.
 
Kwa mashariki ya kati hakuna vitega uchumu ambavyo wanaweza kuzalisha pesa ya kutosha kuendsha nchi zao bila mafuta, wana hifadhi ya pesa kwabwa kushinda Tz ni sawa ila ina kikomo, Tz tuna za miezi 6, na tunaanzisha mingine kwa ajili ya maliasili ni sawa, wao wanaweza kuwa na za miaka 2 au 10, ila zitaisha, inabidi wazalishe bizaa na kuuza huduma kama china ili wapunguze utegemezi wa mali asili, na hio ni safari ndefu.
 
Hivi hawa Wayahudi asili yao ni wapi? kwani kila mahali wanaambiwa ni wa kuja, hili swali lisipojibiwa itakua vigumu kumaliza huo mgogoro.
 
Videge vilitoka wapi 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Habari hizi zinapatikana katika Qur'an kwenye sura nzima iliyoteremshwa kwa ajili yake na kuonesha hali ilivyo Mwenyezi Mungu anapokasirishwa.Adhabu halisi si hapa duniani ni huko akhera. .Ina maana videge hivyo viitumwa kwa kazi maalum.Utajuwa pia kwanini waislamu ndio wa mwanzo kujua ufanisi na ukali wa mapigano kutoka angani.
Ukipenda Sura hiyo isikilize kutoka kwa Abdulbasit msomaji mahiri wa Qur'an kutoka Misri.
 
Hivi hawa Wayahudi asili yao ni wapi? kwani kila mahali wanaambiwa ni wa kuja, hili swali lisipojibiwa itakua vigumu kumaliza huo mgogoro.
Wayahudi wa kweli asili yao ni Palestine,Warabu na Wayahudi ni binami,wanatoka katika ukoo mmoja..

Inasemakana Nabii Abraham alioa wake wawili mmoja kutoka Iraq na na Mmoja kutoka Egypt,..

Watoto wa Abraham kutoka wake zake Hao ndio ukazaa Uyahudi na Uarabu..

Kidini Wayahudi wamelaniwa na kuapizwa na Mungu kuwa wata tanga tanga na Dunia mpaka mwisho wa Dunia

Kisa cha Mungu kuwalaani Wayahudi ni kwasababu Mungu aliwapa uwezo ukubwa ili ayaendeleze.yale anayotala Duniani kupitia kwako..

Wayahudi wamempinga kila Mtume walioletewa na Mungu,wamepinga mpaka sasa Yesu

Mapenzi ya Mungu aliyaondoa Kwa hawa watu,badala yake wakapewa Warabu..

Kumbuka kuwa Kabla ya Muhamad Mitume yote ilikuwa ni Wayahudi

Hawa watu Wako kila Nchi uwezo wao, inasemekana hata watawala wa Saudi Arabia,Moroko ml ni Wayahudi

Wayahudi ni wamoja,wanalindana wanasaidiana,hiyo ndio silaha yao tangu mwanzo wa Dunia

Hawa Wayahudi wanaotawala sasa pale Israel wote ni Wazungu kutoka Ulaya Mashariki,Poland,Urusi nk..
 
Map ya Bible inaonyesha hilo eneo karibu lote ni Israel na karibia robo ya Syria nayo ni Israel.

Waarabu wana matatizo sana.
 
Musa aka Moses allpowaondoa Wayahadi aliamrishwa na na Mungu awapeleke Mlima wa Sinai..

Katika mlima wa Sinai ndipo Musa alipopewa amri kumi za Mungu,baada ya kutanga tanga na Jangwa Kwa muda wa miaka 40..

Hii Stori yako kuwa Waisrael walipewa Ardhi mpaka Iraq umeitoa Biblia gani ya Ngwajima??
 
Nikama tu wanajaribu kusolve maswala ya energy kuepuka mafuta hapohapo wanajaribu kutengeneza polymer mpya zitaweza kuliplace metals ko demand ita baki palepale
 
Map ya Bible inaonyesha hilo eneo karibu lote ni Israel na karibia robo ya Syria nayo ni Israel.

Waarabu wana matatizo sana.
Wayahudi hawana Ardhi hawa ni Watu Waliokuwa hawakai sehemu Mmoja,Kama vile Wamasai

Warabu na Wayahudi wote walikuwa wakikaa sehemu moja..

Wayahudi ni Watu wa maslahi watu wa kuhama Hama Hama

walikuwa Wengi Ujarumani Hitler akawafanyishia wakaondoka wakaendaa Nchi za Ulaya Mashariki,Urusi,Poland

Sasa wamejaa Marekani..

Biblia Kila mtu anatia chake usiamini sana hicho kitabu,sorry

Chini ni map ya Palestine, map inaonyesha vipi Ardhi ya WaPalestina inavyokuwa ndogo siku hadi siku.

 
Mkuu kuwekeza sio lazima middle east huoni wanawekeza nchi za magharibi.... Wananunua hisa za makampuni makubwa, wananunua vilabu vya michezo, wanawekeza kwenye real estate n.k hivyo hta mafuta yakikata leo bado wanaweza sustain uchumi wao kwa miaka zaidi ya 100.

Uchumi hauelekei huko kwenye bidhaa kma unavyodai ila service sector inaweza kukupa matrilion hta kma hauna bidhaa. Macau hawana bidhaa ila inategemea casino zinazojaza watalii kuingiza matrilion ya shilingi kila mwaka. .

Hta US bidhaa tu yaani trade in goods inapigwa mbali sana na nchi kibao ila ikija kwenye financial Assets na trade in services wapo vizuri. So sio lazima uuze bidhaa za kushikika ndio uchumi ukue.

Mifano ipi mingi sana
 
Katika vitabu vya dini hamna hata kitabu kimoja kilichotaja Taifa la Israel,katika vitabu vya dini Wayahudi wanatajwa kama watu sio Taifa..

Waisrael hawajawahi Kuwa na TAIFA na kama sio UN mwaka 1948 kuwakatia Kipande cha Ardhi pale Palestine basi mpaka leo wangelikuwa wanatanga tanga wanahangaika na Ulimwengu
 
Asante Sana, najua wananunua vitu mbali mbali nchi za magharibi, kama tutaweza kuusoma uchumi wa maghari na china kwa undani sio wa kwenye media tutajua kama watafaidika au laa, tuache ya kwao tutafute tiba ya nyumbani.
 
Joshua 1:4
Your territory will extend from the desert to Lebanon, and from the great river, the Euphrates—all the Hittite country—to the Mediterranean Sea in the west.

Ndio nmejengea hoja kma wanafuata mipaka ya bible kwanini wasivamie Iraq na Misri? ila wanawabana wapalestina pekee if at alp basis ya madai ni biblical borders .
 
Ipi, kwani hapo walipo ni middle east na kuna wanaodai sio kwao
Abraham alikua katokea Ur huko Mesopotamia na Canaan/Israel ilikua na makabila 13 tayari. Kwahiyo hapo walivamia tu na kuua wenyeji ndio wakapachukua. so hapakuwa kwao na huo ndio ukweli ambao wengi hatupendi kuukiri.
 
Abraham alikua katokea Ur huko Mesopotamia na Canaan/Israel ilikua na makabila 13 tayari. Kwahiyo hapo walivamia tu na kuua wenyeji ndio wakapachukua. so hapakuwa kwao na huo ndio ukweli ambao wengi hatupendi kuukiri.
Hii Ur, Mesopotamia na Canaan kwa sasa zina majina gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…