Kamari ni jambo la kiroho, tena ni roho mchafu.
Football betting, online casino, slots machines, na aina zote za kamari unazozijua ni vitu vya kiroho.
Wengine huenda kwa wanajimu kuosha nyota zao au kupewa kipawa cha kubashiri (predicting ability), ila hii ni kufuru na machukizo kwa Mungu.
Kamari ili upate pesa lazima ujue kucheza na destiny yako, destiny za watu wengi zimeibiwa au kuchafuliwa na wachawi, mapepo na majini.
Ili upate mafanikio kwenye betting lazima uhakikishe nyota (destiny) yako haijachafuliwa vinginevyo utaishia kusikia tu watu wamepata milioni 10,20, laki 5 n.k.
Kwa watu wa Mungu kamari ni dhambi maana inaleta masononeko , kama mbavyojua masononeko ni kukosa amani, na mtu akikosa amani ndani ya moyo wake hawezi kumuona Mungu.
Roho wa Mungu anataka mahali shwari, penye amani.
Mtu wa Mungu unaweza kubeti na ruhusa na uongozi wa Kimungu na si kufanya betting kuwa kazi yako rasmi.
Shetani ataitumia betting kukuvuruga na Roho wa Mungu aondoke ndani yako ubaki empty.