Mikoa 10 inayoongoza Kwa Ujenzi Holela (Squatters) Kwa Tanzania

Tanga isiwepo ina asilimia ndogo ya slums
Hujui unachoongea zaidi ya kuropoka , unadhani ni takwimu za localized area hizo kwamba sensa ilifanyika mjini pekee?

Huo Mkoa sio tuu uko top 5 ya slums bali unaongoza Kwa vijumba vya tembe,matope ,maudongo na aina zingine za umaskini
 
Hujui unachoongea zaidi ya kuropoka , unadhani ni takwimu za localized area hizo kwamba sensa ilifanyika mjini pekee?

Huo Mkoa sio tuu uko top 5 ya slums bali unaongoza Kwa vijumba vya tembe,matope ,maudongo na aina zingine za umaskini
😅😅😅😅 kweli kabisa, ni pale mjini kati tu ndo mkoloni alipa pangilia.
 
Bila Dar kuongoza Kwa slums hiyó list ni fake
 
Halafu unatakiwa kuelewa sensa haijasema slums ni maeneo Ambayo hayajapimwa. . Kama ni slums Dar ni ya kwanza
 
Kwa kagera it's true, Mazingira Yako hovyo kweli. Ni wachafu alafu nshomile.
 
Mjue kutofautisha kati ya kupimwa na kurasimishwa, na kupangiliwa.
Kunaweza kuwa na kijiji nyumba zake zimepangiliwa kimtaa vizuri kabisa lakini hazijarasimishwa wala hazijapimwa na kuwekwa kwenye ramani za mipango miji au upimaji.

Unaweza kuwa na eneo la mjini kabisa na viwanja vimepimwa na vimerasimishwa na kuwa kwenye mipangomiji ingawa choo cha jirani kinaangalia baraza lako. na mbele kuna duka la kinyozi na pembeni mwa nyumba kuna ki-grocery na nyuma uani kuna mabanda ya kuku.

Kuna sehemu zimepimwa ila zipo hovyo sana ingawa hazihesabiwi kama slums. Mfano ni Goba, nyumba nzuri ila pako hovyo hakuna mitaa iliyonyooka na mabonde kibao kama Capri Point ya Mwanza nayo ni mpangilio wa hovyo tu.
 
Mkuu.

Ukiua mtu mmoja kati ya wawili, umeua 50%.

Ukiua watu milioni moja kati ya milioni 2, umeua 50%.

Hayo mauaji yote ni sawa kwa sababu ni 50%?
naam, percentage hua inamtego sana, makampuni makubwa yanaweza funga na faida ya asilimia 30% kwa mwaka, mtu binafsi nanaweza funga na asilimia 200% faida kwa mwaka. ila ukija fungua kampuni mtaji 1 billion , mtu binafsi mtaji 10 million, so kampuni imemuacha mbali sana kwenye actual figures
 
Huu ni uongo,hapo kwenye list ya mikoa inayoongoza kuwa na uswahili toa Tanga na Singida,pia kwa mikoa inayoongoza kuwa na mipango miji mizuri usiache kuiweka Dodoma...
 
You nailed it
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…