Mikoa 10 ya Tanzania ambayo Wakazi wake wana Maendeleo na Kipato kikubwa

Sema nini, shilingi imeshuka sana thamani ila watanzania hawazingatii anguko la shilingi yetu.

Weka kwa dola ya marekani ndio utaona tunavyojitekenya na kucheka wenyewe.
Dola ya Marekani ndio medium of exchange? Harafu hii inahusianaje na mada?

Mwisho bei zinazotumika kuthaminisha uchumi ni za mwaka 2019 so kama ni exchange rate ambayo NBS wameitumia ni ya 2019 na sio Sasa hivi.Walishafikiria Hilo kabla Yako.
 
Unajua hizi takwimu zina shida kubwa.
Mfano mbaazi inayolimwa huko Babati au Arusha ikiuzwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar hesabu za TRA zitasoma mapato ni Dar.
Sidhani kama kuna shida labda wewe ndio una shida ya kutafsiri takwimu.

Mbaazi Ina Mnyororo wa thamani ambao unaweza anzia shambani Bahati Hadi sokoni India Kila mtu na nafasi yake.

Mzalishaji anauza tena Kwa Mnada wa online analipwa chake ,kile chake kama ameingiziwa kwenye account au cash atapokea hela yake lakini kaka amesafirisha na kuja kuuzia Dar hapo muamala utasoma Dar lakini uhalisia ni kwamba wanunuzi wengii wanafuata kule uzalishaji uliko so sioni shida.

Mwisho Kila mtu atapata chake kulingana na value chain ya bidhaa au Huduma , haiwezekani Zambia azalishe Madini kwao harafu akiezport ,eti ushuru wa kutumia Bandari yetu Wapewe wao,hakuna kitu kama hicho,ndio mfano unaogopa wewe hapa.Akiyefabya exports ndio atapata hela la sivyo fanya export Kwa ndege hapo hapo Mkoani kwako kama una uwanja ila kama huna imekukata.
 
Hongera kwa kujibu maswali
 
Dola ya Marekani ndio medium of exchange? Harafu hii inahusianaje na mada?

Mwisho bei zinazotumika kuthaminisha uchumi ni za mwaka 2019 so kama ni exchange rate ambayo NBS wameitumia ni ya 2019 na sio Sasa hivi.Walishafikiria Hilo kabla Yako.
Dola ndio mkata fitna, shilingi ya 2019 ni kubwa kuliko ya leo 2024. Sasa kama 2019 pato ni 1,200,000 alafu thamani ya shilingi ikaporomoka kwa 15% pato la 2024 likawa ni 1,250,000 hapo ongezeko ni lipi?
 
Lengo la kutumia thami ya nyuma kuthaminisha uzalishaji wa Sasa hivi ni kukabiliana na inflation Kwa hiyo figure ziko sawa ,zingetumika za Sasa ingekuwa kubwa zaidi.

Dola sio medium of exchange ya Tanzania hata kama inatumika llkuweka kama gauge.

Dola Moja kwa Tanzania inakupa wali nyama ,Dola Moja kwa Marekani haiwezi kukupa wali nyama
 
Random statistic! 😳
 
Una hoja mkuu 'Ngongo'.

Lakini haya yote yanatokana na jinsi hiyo taaluma ya uchumi ilivyo, siyo sayansi, mambo mengi ni "kupima upepo" na kutabiri hali kutokana na upepo unavyo vuma.
Najuwa wenyewe wenye taaluma yao wanabisha sana juu ya hili.
 
Wacha kebehi Kwa Wachumi,hakuna upepo unaopimwa Bali ni research findings ndio zinaleta hayo majibu.
 
SAWA.
Kwa hiyo tuseme bado ni "mchumi mbichi", bado hujaiva sawasawa. Akili yako bado ipo kwenye "kutapika" yale uliyo kariri vitabuni zaidi badala ya kuyatumia kwa uelewa husika kufuatana na hali halisi ilivyo.
Nimeiva
 
Bado sana. Usighaili ushauri. Unao mwelekeo, lakini bado unachanganya mambo sana, bila shaka kwa sababu binafsi tu za kupenda kuwa chawa.
🤣🤣🤣🤣🤣 Yaani Mimi nafuata nyayo za Prof.Muhamad Yusuf Rais wa Mpito wa Bangladesh na mshindi wa tuzo ya Nobel kwenye Uchumi.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Yaani Mimi nafuata nyayo za Prof.Muhamad Yusuf Rais wa Mpito wa Bangladesh na mshindi wa tuzo ya Nobel kwenye Uchumi.
Simjui huyo, lakini nadhani hata katika taarifa hiyo hiyo bado ina makosa. Una uhakika kwamba ni "Rais wa mpito" na siyo "Waziri Mkuu wa Mpito"?
Ngoja nitazame kama habari yako hii ni ya kweli!

Kwanza wala siyo 'Yusuf', hilo jina wewe umelipata wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…