Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

Mikoa 13 Kinara wa Kuchangia Kodi ya TRA mwaka 2023

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kutoka kwenye takwimu za Mapato ya Kodi za TRA yaani Regional Tax Statistics za mwaka 2023/2024 zimebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia Mapato makubwa ya Kodi Kwa mwaka 2023.

Uchambuzi wa awali nilioufanya umebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia zaidi Mapato ya Kodi ya kuanzia Bilioni 60 na zaidi.

Orodha hiyo Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 inasomeka kama ifuatavyo;(Figures are in "000" Million Tanzania Shillings).

1. Dar es Salaam =7,416.95
2. Arusha =356.28
3. Kilimanjaro =234.88
4. Tanga =203.28
5. Songwe = 176.81
6. Dodoma =163.17
7. Mwanza =160.66
8. Mara =143.13
9. Kagera =118.94
10. Mtwara =116.44
11. Mbeya =85.10
12. Morogoro =67.60
13. Pwani =60.60

Screenshot_20240806-163541.jpg

My Take
1.Vyanzo vya Kodi kama Utalii, Property Tax,OPMU,MTD na Large Tax Payers Sio sehemu ya takwimu za Mikoa Kwa sababu ni Kodi ya Jumla ambayo Haina mchanganuo wa Mkoa ilikokusanywa.

2.Figurrs za Mkoa wa Dar es Salaam zimehusisha Mikoa ya kikodi iliyoko Dar ambayo ni Ilala,Kinondoni,Temeke,Tegeta,Kariakoo,DSM Service Centre na JNIA.

✓Credits;TRA Regional Tax Statistics 2023/2024.

Observation
•Mapato ya Kodi Kwa Mikoa Mingi mwaka ulioisha wa 2023/2024 Yalishuka sana ukilinganisha na Mwaka 2022/2023. Huenda Mvua za El Nino zilichangia Hali hiyo na sababu zingine.Utalii na Makaa ya Mawe viliokoa jahazi.

•Mkoa wa Mtwara umefanya vizuri Sana kwenye Mapato Kwa sababu ya Bandari ya Maboresho ya Bandari ya Mtwara ,amri ya Rais kusafirisha korosho Kupitia mtwara na Kusafirisha shehena kubwa kabisa ya Makaa ya Mawe kutoka Ruvuma na Njombe.

•Mwanza inazidi kupotea kwenye Ramani ya Uchumi wa Tanzania huku nafasi yake ikichukuliwa na Mikoa mingine.Mlioko Mwanza Jiji lenu limekumbwa na nini Hadi shughuli za Uchumi zinazorota?

Mwisho.
•Pamoja kwmaba TRA ndio taasisi mama ya kukusanya Mapato ila Tanzania Ina taasisi nyingi sana zinazokusanya Mapato ya Serikali,hivyo mchango wa Mkoa kwenye Uchumi wa Nchi unapimwa sawaia Kupitia GDP.

Pia soma Mikoa 15 Inayoongoza Kuchangia Kodi za TRA Tanzania

Angalizo
•Uchambuzi huu sio rasmi hivyo uchukuliwe Kwa muktadha huo.Taasisi Zenye mamlaka husika ndio zitafanya Uchambuzi wake wa kina kama zikiona inafaa.
 
Attachments

mkoa wa Mara mnaweza kuonesha vyanzo vyake mpaka ikaipiku mikoa kama Morogoro na ikawa imepishana kidogo na Mwanza.
Mikoa yote yenye border posts/Inayopakanan na Nchi jirani na Bandari ndio Ina makusanyo makubwa.

Kundi Hilo Lina Mikoa ya Dar,Arusha,Tanga, Kilimanjaro,Mara,Songwe,Kagera na Mtwara.
 
Kutoka kwenye takwimu za Mapato ya Kodi za TRA yaani Regional Tax Statistics za mwaka 2023/2024 zimebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia Mapato makubwa ya Kodi Kwa mwaka 2023.

Uchambuzi wa awali nilioufanya umebainisha Mikoa 13 ambayo imechangia zaidi Mapato ya Kodi ya kuanzia Bilioni 60 na zaidi.

Orodha hiyo Kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 inasomeka kama ifuatavyo;(Figures are in "000" Million Tanzania Shillings).

1.Dar es Salaam =7,416.95
2.Arusha =356.28
3.Kilimanjaro =234.88
4.Tanga =203.28
5.Songwe = 176.81
6.Dodoma =163.17
7.Mwanza =160.66
8.Mara =143.13
9.Kagera =118.94
10.Mtwara =116.44
11.Mbeya =85.10
12.Morogoro =67.60
13.Pwani =60.60

My Take
1.Vyanzo vya Kodi kama Utalii, Property Tax,OPMU,MTD na Large Tax Payers Sio sehemu ya takwimu za Mikoa Kwa sababu ni Kodi ya Jumla ambayo Haina mchanganuo wa Mkoa ilikokusanywa.

2.Figurrs za Mkoa wa Dar es Salaam zimehusisha Mikoa ya kikodi iliyoko Dar ambayo ni Ilala,Kinondoni,Temeke,Tegeta,Kariakoo,DSM Service Centre na JNIA.

✓Credits;TRA Regional Tax Statistics 2023/2024.

Observation
•Mapato ya Kodi Kwa Mikoa Mingi mwaka ulioisha wa 2023/2024 Yalishuka sana ukilinganisha na Mwaka 2022/2023. Huenda Mvua za El Nino zilichangia Hali hiyo na sababu zingine.Utalii na Makaa ya Mawe viliokoa jahazi.

•Mkoa wa Mtwara umefanya vizuri Sana kwenye Mapato Kwa sababu ya Bandari ya Maboresho ya Bandari ya Mtwara ,amri ya Rais kusafirisha korosho Kupitia mtwara na Kusafirisha shehena kubwa kabisa ya Makaa ya Mawe kutoka Ruvuma na Njombe.

Mwisho.
•Pamoja kwmaba TRA ndio taasisi mama ya kukusanya Mapato ila Tanzania Ina taasisi nyingi sana zinazokusanya Mapato ya Serikali,hivyo mchango wa Mkoa kwenye Uchumi wa Nchi unapimwa sawaia Kupitia GDP.

Pia soma Mikoa 15 Inayoongoza Kuchangia Kodi za TRA Tanzania

Angalizo
•Uchambuzi huu sio rasmi hivyo uchukuliwe Kwa muktadha huo.Taasisi Zenye mamlaka husika ndio zitafanya Uchambuzi wake wa kina kama zikiona inafaa.
1. Umeweka Top 13 ili Mbeya tu iwepo🤣🤣🤣

2. Wapi Iringa?

3. Nimependa jinsi Arusha na Kilimanjaro wanavyoiacha mbali Mwanza. Hivi Mwanza ukitoa Ziwa Victoria inabakiwa na nini?

4. Hongereni Kagera. Naona mnakuja kuja
instanbul
 
Hayo ni mawazo Yako.

Mwaka Jana niliweka top 15 ila mwaka huu Mikoa Mingi imefanya vibaya sana ukiacha Mtwara,Kagera na Mbeya kwenye List hapo wengine wameshuka sana.

2.Iringa ni Mkoa maskini tuu,fungua Excell utaona ilichokusanya.

3.Mwanza sijajua ilikuwa na nini mwaka huo maana makusanyo yameshuka sana

4.Kagera Iko kwenye List siku zote Kwa sababu ya Border na Nchi jirani.
 
Sasa kwa nini Mbeya inapewa hadhi ya Jiji huku Kilimanjaro inaachwa huku mapato ya Kikimanjaro ni Mara 3 ya Mapato ya Mbeya.
Muwe mnasema mada kabla ya kukurupuka.

Hadhi ya Jiji inatokana na sababu Nje ya ulizosema.

Pia nimeweka wazi kwamba Nchi Ina vyanzo vingi sana vya Mapato achilia mbali hayo ya TRA.

Mfano haya hayapo kwenye hiyo List ya TRA, Manispaa ya Moshi inaweza pata makusanyo ya ndani ya Bilioni 20? 👇👇
juma_zuberi_homera_1720609958796204.jpg
 
mkoa wa Mara mnaweza kuonesha vyanzo vyake mpaka ikaipiku mikoa kama Morogoro na ikawa imepishana kidogo na Mwanza.
Mara wana mbuga ya wanyama maarufu kuliko zote afrika, mbuga hii huchangia 80% ya mapato ya utalii Tanzania. Mara wana ziwa, wana mpaka, wana migodi mikubwa na midogo, na shughuli nyingine za kilimo na ufugaji.
 
1. Umeweka Top 13 ili Mbeya tu iwepo🤣🤣🤣

2. Wapi Iringa?

3. Nimependa jinsi Arusha na Kilimanjaro wanavyoiacha mbali Mwanza. Hivi Mwanza ukitoa Ziwa Victoria inabakiwa na nini?

4. Hongereni Kagera. Naona mnakuja kuja
instanbul
Ukanda wote wa Wasukuma kumejaa umasikini,hata hiyo Mwanza wanayoibeba ni Wakurya kutoka Mara.
 
Back
Top Bottom