BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
NISHATI: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuzimwa kwa huduma katika Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovoti 220 kutoka Msamvu hadi Dodoma ili kuruhusu umaliziaji kazi kwenye vituo vya Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) vya Msongo wa Kilovoti 220/33
Mikoa itakayoathirika kutokana na kazi hiyo itayodumu kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 jioni Julai 3 na 4, 2024 ni Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Singida, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mwanza, Mara, Geita, Arusha, Kilimanjaro na Manyara
TANESCO imesema ukarabati huo unalenga kuimarisha mifumo ya uendeshaji wa Treni pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa TANESCO katika uendeshaji wa njia ya Kilovoti 220 ya SGR kati ya Msamvu na Dodoma.
Pia Soma:
- Shirika la Reli: Treni ya SGR haitumii umeme mwingi