Mikoa Migumu Kutoboa Kimaisha

Mikoa Migumu Kutoboa Kimaisha

Kwenye umaskini Totoro ndipo kwenye fursa kubwa. Kuna wahindi fulani wanaita Kampuni yao Shinyanga imporium walianzia maisha Shinyanga, zamani huko, kufikia miaka ya 2000 walikuwa Dsm wakisafirisha spare za baiskeli toka nje na kuuza Tanzania nzima.
Aisee
Wewe msukuma kabisa Shinyanga
Vipi Delight cinema, Ashiana hotel, na disco la butiama
Ule mtaa wa Shinyang Emporium wote ulikuwa umejaa maduka ya wahindi miaka ile, kina Makecha, Aziz video, na ile tea shop nyuma ya benki tulikuwa tunaenda kununua jelebi
 
Japo wanasema maisha popote ila Kwa Mikoa hii ukienda kutafuta maisha basi tegemea kutoboka badala ya Kutoboa 😬😬

1.Kilimanjaro
2.Shinyanga
3.Simiyu
4.Kagera
5.Singida
6.Rukwa
7.Tabora
8.Dodoma
9.Lindi
10.Kigoma

My Take
Baadhi ya Mikoa Ina potential nzuri ni vile tuu haijafunguliwa kimiundombinu eg Lindi.

Pia soma Mikoa 10 Yenye Watu Maskini Zaidi Tanzania: Kagera namba 2, Dodoma namba 5. Nini Kinaiponza Mikoa Hii Maarufu?
Ili utoboe katika mkoa husika angalia fursa zilizopo hapo. Sasa vijana mnahamanna firsa za dar mnataka mzipeleke mkoani. Yaani uende Mbeya kuuza maji unafikiri utatoboa?
 
Sio kwamba wenyeji wamezubaa...

Kimsingi wafipa sio wakabila, ndio maana rukwa kuna unafuu kwenye utafutaji...

Kuna mikoa ukienda utatamani kulia wenyeji walivyo wabaguzi...

Kila unachokifanya utafanyiwa figisu hadi uondoke.
Kwani Rukwa inawafipa tuu Mkuu. Sehemu zote za Rukwa nimezitembelea na naendelea kuzitembelea ndio chaka langu la utafutaji, ni kweli watu wake sio Wakabila ila hawajui kuchangamkia fursa kwa ukubwa wanakuridhika flani hata wakipata kidogo sawa tuu kwao hata hao wafipa pia wako hivo.
 
DUH ASEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

 
Ili utoboe katika mkoa husika angalia fursa zilizopo hapo. Sasa vijana mnahamanna firsa za dar mnataka mzipeleke mkoani. Yaani uende Mbeya
Hapa unazungumzia mkulima mkubwa au mfanyabiashara ndio wanaweza kutafuta soko nje ya Mkoa.

Vipi wakulima wadogo? Kwa nini hao wanunuzi wasije wenyewe? Unakoenda kuuza ndiko wanapata mzunguko wa hela nyie mnasalia kupiga miayo kusubiria mavuno mengine.

Mikoa ya hivyo huwezi toboa ,Bora hata uende Lindi ukalime korosho.
Hapo Akili Kumkichwa Bablai, unaweza ukalima na kuwa mfanyabiashara kwa wakati mmoja. Hao matajiri wakilimo wa Mbeya hasa Mpunga walioko Bonde la Ziwa Rukwa ni matajiri wa kutupwa na hao wasukuma wahamiaji wanalima na kufuga wamechangamkia fursa na wanakipato kizuri. Ila changamkia fursa kutokana na eneo ulilopo ndio maana nikasema Rukwa bado kuna fursa ila hasa kwenye Kilimo na Ufugaji utatoboa usije na iphone store au duka la urembo huku Muze, Kiliamatundu au Kapenta.
 
Aisee
Wewe msukuma kabisa Shinyanga
Vipi Delight cinema, Ashiana hotel, na disco la butiama
Ule mtaa wa Shinyang Emporium wote ulikuwa umejaa maduka ya wahindi miaka ile, kina Makecha, Aziz video, na ile tea shop nyuma ya benki tulikuwa tunaenda kununua jelebi
Sasa watafute walipo hao gabacholi toka Mwadui na Lyabukande Shinyanga. Utawakuta Da, London , Vancuva, New York, Tokyo. Nk
 
Kwangu mimi naona migumu ni hii
1.Kilimanjaro
2.Singida
3.Pemba
4.Rukwa
5.Tanga
6.Dodoma
7.Kigoma
8.Shinyanga
9.Lindi
10.Dodoma
 
Rukwa ni kweli wenyeji wamezubaa (ila wachapakazi) na uzuri sio wakabila, wageni wamekamatia fursa hasa Sekta ya Kilimo. Ukiwekeza kwenye Kilimo umetoboa ila uwe mbunifu pia wa kutafuta masoko nje ya mkoa wa Rukwa utapata faida hata mara mbili mpaka tatu.
Wafipa wamejazana zanzibar hawana kabisa mpango wa kurudi
 
Back
Top Bottom