Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Unaujua mkoa wa Geita?
Bii mikoa 4, yote ninaifahamu in and out. Geita inaweza kukudanganya ukifika tu hapo mjini, ambapo napo mji hauna mpangilio mzuri. Lakini ukienda huko pembeni kwenye wilaya na vijiji vyake, ni hoi bin taabani. Pita hata hiyo barabara ya kutoka Kasamwa nenda Ngoma mpaka Msalala, utaona ilivyo nyuma bado. Simiyu, pita hiyo barabara ya Mwigumbi, Maswa, Dutwa mpaka Lamadi, utauona uhalisia, na hayo ni maeneo ya barabarani, lakini ukiingia ndani huko, ni hoi kabisa.
Njombe, hata vijiji vyake vipo vizuri. Nimepita huko sikuwahi huona nyumba ya miti au tope, nyingi ni matofali ya kuchoma, na kuezekwa bati. Pia watu wao huko vijijini ni wazalushaji wakubwa wa mazao ya chakula na mbao. Njombe, mtu akipata magunia 50 ya mahindi, huyu ni mtu duni sana, wakati Geita na huko Simiyu, ataonekana mkulima mkubwa. Njombe wealth distribution, ni nzuri, huenda kuliko mkoa wowote.