nguvu ya buku
Senior Member
- Jul 15, 2025
- 168
- 549
Matokeo ya Form 6 yametangazwa, lakini kwa wazazi na walezi wa mikoz ya kanda ya mashariki na Kanda ya Ziwa, haya si matokeo ya furaha bali ya mateso.
Kigoma, atavi, Tabora, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara huwezi kukuta chuo cha serikali chenye degree ya Law wala Degree za Engineering.
walezi tunaosomesha limekuwa ni pigo kubwa kwetu, Gharama ni kubwa, Mwanafunzi yupo Kagera au Mara anasafiri maelfu ya lilometa mpaka Mbeya, safari ya siku 2 hadi 3 kufuata chuo cha Sheria au Sayansi.
Inafika mahala tunashindwa hata kuhudhuria mahafali au kuwasalimia watoto / ndugu zetu kwa sababu ya umbali mrefu na gharama kubwa za usafiri.
Makao makuu ya mikoa hiyo ni Mwanza. Ni jiji ambalo limekuwepo kwa muda mrefu tangu enzi ambazo Tanzania ilikuwa na majiji mawili tu (Dsm na Mwanza), Ni jiji la pili kwa watu wengi, Ni mkoa wa pil kwa idadi ya watu wengi. Hata hivyo, hadi leo Mwanza haina chuo kikuu chochote cha serikali. Vilivyopo ni matawi ya vyuo vya kati na bado hakuna kinachotoa kozi za sheria wala sayansi kama vile kozi za engineering katika ngazi ya degree. Tunasikitika, tunaumia na tunashangaa , kwa nini? Huu ni ubaguzi wa wazi unaotuchosha na kutudhalilisha.
Ukiangalia maeneo mengine, hali ni tofauti
- Tanga, Kilimajaro, Arusha, Manyara - vyuo vipo Arusha na Moshi.
- Dar, Pwani, Morogoro, Mtwara, Lindi - Vyuo vipo Dar na Morogoro
- Mbeya, Ruvuma, Njombe, Iringa, Songwe, Rukwa - Vyuo vipo Mbeya na Iringa
- Kanda ya Kati Dodoma ni kitovu cha kitaifa, vyuo ni vingi na vingi zaidi vitajengwa.
Lakini Mikoa ya Magharibi na inayozunguka Ziwa je ? Kimya. Giza. Ubaguzi !
Saut Mwanza ni chuo cha Kanisa, walikuwa ndio kimbilio la wengi lakini wamefungiwa kutoa degree ya sheria.
Kuna tawi la chuo cha DIT Mwanza lakini sio level ya degree