View attachment 3414597
Matokeo ya Form 6 yametangazwa, lakini kwa wazazi na walezi wa Kigoma na Kanda ya Ziwa, haya si matokeo ya furaha bali ya mateso.
Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara huwezi kukuta chuo cha serikali chenye degree ya Law wala Degree za Engineering. (Pia ukiongezea Katavi na Tabora)
walezi tunaosomesha limekuwa ni pigo kubwa kwetu, Gharama ni kubwa, Mwanafunzi yupo Kagera au Mara anasafiri maelfu ya lilometa mpaka Mbeya, safari ya siku 2 hadi 3 kufuata chuo cha Sheria au Sayansi.
Baadhi yetu tunashindwa hata kwenda kuwasaliia au kuhudhuria Graduation kwa sababu ya nauli kubwa na umbali mrefu.
Makao makuu ya mikoa hiyo ni Mwanza, Ni jiji kwa muda mrefu tangu enzi nchi ikiwa na majiji mawili tu (Dar na Mwanza), ni mkoa wa pili kwa watu wengi Tanzania, Lakini hata hivyo, hakuna chuo kikuu chochote zaidi ya matawi (campus) za vyuo vingine ! Tunasikitika, tunaumia na tunashangaa, Kwa nini ? Kwa nini jiji kubwa na lenye watu wengi hivi halina chuo / kikuu ? Huu ni ubaguzi wa wazi unaotuchosha na kutudhihaki.
Hata hizo campus hakuna yoyote ya Chuo kikubwa kama Udsm, Udom, Mzumbe. Kuna campus za vyuo vya kati tu.
- Kanda ya Kaskazini (Tanga, Kilimajaro, Arusha, Manyara) - vyuo vipo Arusha na Moshi.
- Kanda ya Pwani (Dar, Pwani, Moro, Mtwara, Lindi) - Vyuo vipo Dar na Morogoro
- Mbeya, Ruvuma, Iringa, Songwe, Rukwa - Vyuo vipo Mbeya na Iringa
- Kanda ya Kati Dodoma ni kitovu cha kitaifa, vyuo ni vingi na vingi zaidi vitajengwa.
Lakini Kigoma na Kanda ya Ziwa je ? Kimya. Giza. Ubaguzi !
Saut Mwanza walikuwa wanadahili degree ya sheria ila kwa sasa wamefungiwa,
Kuna tawi la chuo cha DIT Mwanza lakini sio level ya degree