AlanusJosephat53
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 747
- 746
Kwa hiyo mtu wa kanda ya ziwa hawezi kusoma Dar au mkoa mwingine!?Wanaogopa serikali wakifiri wanaweza kuwasomesha wanyarwanda na burundi
Kwa hiyo mtu wa kanda ya ziwa hawezi kusoma Dar au mkoa mwingine!?Wanaogopa serikali wakifiri wanaweza kuwasomesha wanyarwanda na burundi
Ni gharama zaidi, Ni mbali zaidi, vijana wengi hukatisha ndoto zao, ni ubaguzi wa maendeleoKwa hiyo mtu wa kanda ya ziwa hawezi kusoma Dar au mkoa mwingine!?
Simiyu hakuna TIA ila Kuna IFM. Usichanganye bro.Vyuo vilivyopo ni kozi za kawaida
Tabora - Chuo binafsi cha ualimu cha mchungaji Mihayo
Kigoma - Chuo cha uhasibu TIA (angalau hiki kina hadhi kipo pia Mwanza na Simiyu)
Katavi - Chuo cha ufugaji wa nyuki
DIT si wapo Mwanza au hawatoi degree!?Matokeo ya Form 6 yametangazwa, lakini kwa wazazi na walezi wa Kigoma na Kanda ya Ziwa, haya si matokeo ya furaha bali ya mateso.
Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara huwezi kukuta chuo cha serikali chenye degree ya Law wala Degree za Engineering. (Pia ukiongezea Katavi na Tabora)
walezi tunaosomesha limekuwa ni pigo kubwa kwetu, Gharama ni kubwa, Mwanafunzi yupo Kagera au Mara anasafiri maelfu ya lilometa mpaka Mbeya, safari ya siku 2 hadi 3 kufuata chuo cha Sheria au Sayansi.
Baadhi yetu tunashindwa hata kwenda kuwasaliia au kuhudhuria Graduation kwa sababu ya nauli kubwa na umbali mrefu.
Makao makuu ya mikoa hiyo ni Mwanza, Ni jiji kwa muda mrefu tangu enzi nchi ikiwa na majiji mawili tu (Dar na Mwanza), ni mkoa wa pili kwa watu wengi Tanzania, Lakini hata hivyo, hakuna chuo kikuu chochote zaidi ya matawi (campus) za vyuo vingine ! Tunasikitika, tunaumia na tunashangaa, Kwa nini ? Kwa nini jiji kubwa na lenye watu wengi hivi halina chuo / kikuu ? Huu ni ubaguzi wa wazi unaotuchosha na kutudhihaki.
Hata hizo campus hakuna yoyote ya Chuo kikubwa kama Udsm, Udom, Mzumbe. Kuna campus za vyuo vya kati tu.
- Kanda ya Kaskazini (Tanga, Kilimajaro, Arusha, Manyara) - vyuo vipo Arusha na Moshi.
- Kanda ya Pwani (Dar, Pwani, Moro, Mtwara, Lindi) - Vyuo vipo Dar na Morogoro
- Mbeya, Ruvuma, Iringa, Songwe, Rukwa - Vyuo vipo Mbeya na Iringa
- Kanda ya Kati Dodoma ni kitovu cha kitaifa, vyuo ni vingi na vingi zaidi vitajengwa.
Lakini Kigoma na Kanda ya Ziwa je ? Kimya. Giza. Ubaguzi !
nimekosea lakini haibadili uhalisia TIA na IFM vyote ni vyuo vya kati vinafanana kwa kiasi kikubwa kwa kutoa kozi za uhasibu, masoko na ugaviSimiyu hakuna TIA ila Kuna IFM. Usichanganye bro.
Halafu fatilia takwimu zako, haupo sahihi kwenye hili swala
Makao makuu ya Kanda ya magharibi ni Tabora.
Je hakuna vyuo?
Mbona hujakitaja TEKU tawi la Tabora, Chuo Cha uhazili.waziri @gwajim
nimekosea lakini haibadili uhalisia TIA na IFM vyote ni vyuo vya kati vinafanana kwa kiasi kikubwa kwa kutoa kozi za uhasibu, masoko na ugavi
Ok, makuu ya Kanda ya magharibi ni Tabora, je kuna chuo chochote cha degree zaidi ya cha ualimu cha Mchungaji Mihayo?
Chuo hicho unachosema bila shaka ni cha Mwalimu Nyerere, wana degree moja tu, sayansi ya BiasharaKuna chuo kipo Butiama kinamaliziwa kujengwa....fuatilia, ni chuo kikubwa sana kikikamilika
Uwe unaelewa hata kichwa cha post mkuuMbona hujakitaja TEKU tawi la Tabora, Chuo Cha uhazili.
Kwani lengo ni kujenga nchi au kila jamii ijitegemee?
Mwaka huu wataongeza kozi, ujenzi umeshika kasi kipind cha Samia baada ya kupata pesa za HEET..Chuo hicho unachosema bila shaka ni cha Mwalimu Nyerere, wanadahili kozi moja tu, sayansi ya Biashara
hivi hakijamalizika tu kujengwa ? maana ni tangu enzi za Kikwete.
Kwa mwaka huu tayari wameshatoa kozi wanazodahili,Mwaka huu wataongeza kozi, ujenzi umeshika kasi kipind cha Samia baada ya kupata pesa za HEET..
Mwakani mchina anakabidhi majengo...pako fresh sana
Matokeo ya Form 6 yametangazwa, lakini kwa wazazi na walezi wa Kigoma na Kanda ya Ziwa, haya si matokeo ya furaha bali ya mateso.
Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara huwezi kukuta chuo cha serikali chenye degree ya Law wala Degree za Engineering. (Pia ukiongezea Katavi na Tabora)
walezi tunaosomesha limekuwa ni pigo kubwa kwetu, Gharama ni kubwa, Mwanafunzi yupo Kagera au Mara anasafiri maelfu ya lilometa mpaka Mbeya, safari ya siku 2 hadi 3 kufuata chuo cha Sheria au Sayansi.
Baadhi yetu tunashindwa hata kwenda kuwasaliia au kuhudhuria Graduation kwa sababu ya nauli kubwa na umbali mrefu.
Makao makuu ya mikoa hiyo ni Mwanza, Ni jiji kwa muda mrefu tangu enzi nchi ikiwa na majiji mawili tu (Dar na Mwanza), ni mkoa wa pili kwa watu wengi Tanzania, Lakini hata hivyo, hakuna chuo kikuu chochote zaidi ya matawi (campus) za vyuo vingine ! Tunasikitika, tunaumia na tunashangaa, Kwa nini ? Kwa nini jiji kubwa na lenye watu wengi hivi halina chuo / kikuu ? Huu ni ubaguzi wa wazi unaotuchosha na kutudhihaki.
Hata hizo campus hakuna yoyote ya Chuo kikubwa kama Udsm, Udom, Mzumbe. Kuna campus za vyuo vya kati tu.
- Kanda ya Kaskazini (Tanga, Kilimajaro, Arusha, Manyara) - vyuo vipo Arusha na Moshi.
- Kanda ya Pwani (Dar, Pwani, Moro, Mtwara, Lindi) - Vyuo vipo Dar na Morogoro
- Mbeya, Ruvuma, Iringa, Songwe, Rukwa - Vyuo vipo Mbeya na Iringa
- Kanda ya Kati Dodoma ni kitovu cha kitaifa, vyuo ni vingi na vingi zaidi vitajengwa.
Lakini Kigoma na Kanda ya Ziwa je ? Kimya. Giza. Ubaguzi !
Diploma na degree?Kwa mwaka huu tayari wameshatoa kozi wanazodahili,
ni kozi moja tu ! sayansi ya biashara, Imeisha hivyo !
Uzi unahusu Degree, kozi zimeshatolewa kwa vyuo vyote vitavyodahili wanafunzi mwaka huu, hicho chuo kuna kozi moja tuDiploma na degree?
Anyway, tusubiri nilisikia kuna kozi TCU wamezi approve tayari
Nadhani mwakani wataanza nyingi zaidi...Uzi unahusu Degree, kozi zimeshatolewa kwa vyuo vyote vitavyodahili wanafunzi mwaka huu, hicho chuo kuna kozi moja tu
SHIDA YA WATU WA KIGOMA UBISHI NA UJUAJI.Dkt. Gwajima D
Mhe. Dkt Dorothy Gwajima tunaomba msaada wako katika wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kutambua kwamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa (Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) na Kanda ya Mashariki (Tabora, Kigoma na Katav) hakuna kabisa vyuo vya Degree vya Sheria wala Sayansi. (Nimeambatanisha Pdf ya vyuo vya degree )
Wanawake na Wasichana wa Kanda ya Ziwa wanabaki nyuma:
Ukosefu wa vyuo vya karibu unaathiri zaidi wanawake, ambao mara nyingi hawaruhusiwi kusafiri mbali au hushindwa kwa sababu ya ukosefu wa usaidizi wa kifamilia. Hii inasababisha watoto wa kike kukatisha masomo na kuwa hatarini kuingia kuolewa badala ya kuendelea masomo.
Makundi maalum kama wenye ulemavu hushindwa kabisa kupata elimu ya juu:
Umbali na mazingira magumu ya kusafiri kwao ni kizuizi kikubwa. Bila vyuo vya karibu, ndoto zao zinazimika kabla hata hazijaanza.
Walezi, hasa wanawake wanabeba mzigo mzito wa kifedha na kihisia:
Wanachukua mikopo ya riba kubwa, kuuza mashamba ya urithi, ili kumpeleka mtoto mikoa ya mbali kusoma. Huu ni mzigo wa kimfumo unaoweza kupunguzwa kwa kuwa na vyuo karibu. mtoto akiwa karibu gharama za usafiri, chakula, malazi, zinaweza kupunguzwa akisomea nyumbani.
Elimu ni kichocheo cha maendeleo ya jamii:
Kwa kusaidia uwepo wa vyuo hivi, utakuwa unatoa fursa kwa mamilioni ya vijana hasa wanawake na makundi maalum kujikwamua kiuchumi, kijamii na kielimu. Utakuwa sehemu ya historia ya kupunguza pengo la elimu ambalo limeikumba kanda hii kwa miongo mingi.
Tunaomba Mheshimiwa:
- Uwasilishe hoja hii katika vikao vya Serikali na Bunge.
- Ushirikiane na Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuona namna ya kuharakisha uwepo wa angalau chuo kikuu kimoja cha Seikali Mwanza.
- Uandae kikao na wadau wa elimu wa kanda husika na wanawake wa jamii kujadili athari halisi.
Mapendekezo
Katika maeneo tajwa kijengwe chuo kikuu kimoja hata viwili kama ilivyo kwa Dodoma (Udom), Dar (Udsm), Mbeya (MUST), Morogoro (Mzumbe)
Kujengwe kampasi za vyuo vikuu kama Mzumbe, Udom, Udsm, MUST, n.k. na ziwe na kozi muhimu za degree, Nimefuatilia post flani humu humu Jamiiforums kuna Campus ya DIT imejengwa Mwanza lakini kozi wanazotoa ni Diploma tena ni za kushona viatu na mikanda kwa ngozi za wanyama, wanafunzi bado wanajazana DIT ya Dar kozi zenye demand.
Kuboresha miundo mbinu vyuoni kitaifa kwa watu wenye mahitaji maalum.
kwani wamewazuia kusoma kanda zingineLawama nyingine ni za kitoto sana.
Kule Chato mwenzenu kapeleka uwanja wa ndege, benki, jengo la TRA n.k lakini yameishia kuwa makazi ya popo na ng'ombe!
Leo mnataka vyuo vya sheria. Acheni utoto!