Mikoa ya kanda ya Ziwa na Magharibi hakuna vyuo vya degree vya Sheria wala sayansi, Serikali imetusahau?

nguvu ya buku

Senior Member
Joined
Jul 15, 2025
Posts
168
Reaction score
549


Matokeo ya Form 6 yametangazwa, lakini kwa wazazi na walezi wa mikoz ya kanda ya mashariki na Kanda ya Ziwa, haya si matokeo ya furaha bali ya mateso.

Kigoma, atavi, Tabora, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara huwezi kukuta chuo cha serikali chenye degree ya Law wala Degree za Engineering.

walezi tunaosomesha limekuwa ni pigo kubwa kwetu, Gharama ni kubwa, Mwanafunzi yupo Kagera au Mara anasafiri maelfu ya lilometa mpaka Mbeya, safari ya siku 2 hadi 3 kufuata chuo cha Sheria au Sayansi.

Inafika mahala tunashindwa hata kuhudhuria mahafali au kuwasalimia watoto / ndugu zetu kwa sababu ya umbali mrefu na gharama kubwa za usafiri.

Makao makuu ya mikoa hiyo ni Mwanza. Ni jiji ambalo limekuwepo kwa muda mrefu tangu enzi ambazo Tanzania ilikuwa na majiji mawili tu (Dsm na Mwanza), Ni jiji la pili kwa watu wengi, Ni mkoa wa pil kwa idadi ya watu wengi. Hata hivyo, hadi leo Mwanza haina chuo kikuu chochote cha serikali. Vilivyopo ni matawi ya vyuo vya kati na bado hakuna kinachotoa kozi za sheria wala sayansi kama vile kozi za engineering katika ngazi ya degree. Tunasikitika, tunaumia na tunashangaa , kwa nini? Huu ni ubaguzi wa wazi unaotuchosha na kutudhalilisha.

Ukiangalia maeneo mengine, hali ni tofauti
  • Tanga, Kilimajaro, Arusha, Manyara - vyuo vipo Arusha na Moshi.
  • Dar, Pwani, Morogoro, Mtwara, Lindi - Vyuo vipo Dar na Morogoro
  • Mbeya, Ruvuma, Njombe, Iringa, Songwe, Rukwa - Vyuo vipo Mbeya na Iringa
  • Kanda ya Kati Dodoma ni kitovu cha kitaifa, vyuo ni vingi na vingi zaidi vitajengwa.

Lakini Mikoa ya Magharibi na inayozunguka Ziwa je ? Kimya. Giza. Ubaguzi !

Saut Mwanza ni chuo cha Kanisa, walikuwa ndio kimbilio la wengi lakini wamefungiwa kutoa degree ya sheria.

Kuna tawi la chuo cha DIT Mwanza lakini sio level ya degree
 
Kozi ipi ya sheria mbona kila mara tunasikia amemaliza Degree ya Sheria SAUT Mwanza?
 
Wasomi wa Kagera na Kigoma kwanini hawakufanya lobbying ya kutosha vyuo vikuu vije vijengwe pande hizo au ndio ubinafsi ?
 
Mwaka uliopita pale SAUT LLB walisajiliwa wanafunzi 500+ sa sijui iyo historia yako ni ya Wakati ujao bro??
Utakuwa umechanganya kozi ya Ualimu

Kozi ya sheria ilikuwa na wanafunzi wachache sana SAUT

Mwaka huu kwenye udahili unaosimamiwa na tume ya usimamizi wa vyuo vikuu, SAUT hakuna kozi ya sheria
 
Warundi kina Kagame wamesoma Udsm
Paul Kagame studied briefly at the University of Makerere in Uganda but did not complete a full degree. His formal education was interrupted by his involvement in military and liberation movements. Later, he received military training in countries such as the United States (Command and General Staff College at Fort Leavenworth, Kansas). His leadership skills were shaped more by military and political experience than by academic credentials..
 
Baada ya muda mfupi nitakuja na takwimu safi sijui mengi kuhusu school of law maana me npo faculty ya engineering mkubwa.
 
Wenzenu Singida wameomba na wanapelekewa Chuo kitakachofundisha degree ya ufigaji nyuki na ulinaji wa asali bala ya kuomba VETA Singida ndiyo iongezewr hizo cpurse na course za mapokezi na ulalimu kwa wateja na kazi za ndani
 
Utakuwa umechanganya kozi ya Ualimu

Kozi ya sheria ilikuwa na wanafunzi wachache sana SAUT

Mwaka huu kwenye udahili unaosimamiwa na tume ya usimamizi wa vyuo vikuu, SAUT hakuna kozi ya sheria
Dirisha la udahili lililofunguliwa Tarh 08/07/2025 course unayosema haipo ipo mkuu ktk chuo cha SAUT maybe tuje kwenye concept kwamba hakuna chuo cha serikali ukanda wa ziwa na sehemu zingine ulizozitaja,hoja za kuzingatia ni kwamba serikali haina utayari huo au labda watu wa ukanda huo hawapo tayari kwa ajili ya kutunukiwa shahada,au ni nini tatizo hadi kada za msingi kama hizo tuletewe na wamisionari katika maeneo hayo??
 
Mkuu uwe unafuatilia habari, Kuna mabadiliko yamefanyika kwa baadhi ya vyuo kutodahili baadhi ya kozi

Udom wamefuta kozi kama 8, Saut wamefuta kozi 4 ikiwemo sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…