Mikoa ya kanda ya Ziwa na Magharibi hakuna vyuo vya degree vya Sheria wala sayansi, Serikali imetusahau?

Vyuo vilivyopo ni kozi za kawaida

Tabora - Chuo binafsi cha ualimu cha mchungaji Mihayo
Kigoma - Chuo cha uhasibu TIA (angalau hiki kina hadhi kipo pia Mwanza na Simiyu)
Katavi - Chuo cha ufugaji wa nyuki
Simiyu hakuna TIA ila Kuna IFM. Usichanganye bro.
Halafu fatilia takwimu zako, haupo sahihi kwenye hili swala

Makao makuu ya Kanda ya magharibi ni Tabora.

Je hakuna vyuo?
 
DIT si wapo Mwanza au hawatoi degree!?
 
waziri @gwajim
Simiyu hakuna TIA ila Kuna IFM. Usichanganye bro.
Halafu fatilia takwimu zako, haupo sahihi kwenye hili swala

Makao makuu ya Kanda ya magharibi ni Tabora.

Je hakuna vyuo?
nimekosea lakini haibadili uhalisia TIA na IFM vyote ni vyuo vya kati vinafanana kwa kiasi kikubwa kwa kutoa kozi za uhasibu, masoko na ugavi

Ok, makuu ya Kanda ya magharibi ni Tabora, je kuna chuo chochote cha degree zaidi ya cha ualimu cha Mchungaji Mihayo?
 
Mbona hujakitaja TEKU tawi la Tabora, Chuo Cha uhazili.

Kwani lengo ni kujenga nchi au kila jamii ijitegemee?
 
Chuo hicho unachosema bila shaka ni cha Mwalimu Nyerere, wanadahili kozi moja tu, sayansi ya Biashara

hivi hakijamalizika tu kujengwa ? maana ni tangu enzi za Kikwete.
Mwaka huu wataongeza kozi, ujenzi umeshika kasi kipind cha Samia baada ya kupata pesa za HEET..
Mwakani mchina anakabidhi majengo...pako fresh sana
 
Mwaka huu wataongeza kozi, ujenzi umeshika kasi kipind cha Samia baada ya kupata pesa za HEET..
Mwakani mchina anakabidhi majengo...pako fresh sana
Kwa mwaka huu tayari wameshatoa kozi wanazodahili,

ni kozi moja tu ! sayansi ya biashara, Imeisha hivyo !
 

lakini baiskeli si zimefika jamani
kuweni na shukrani hata kidogo
 
Dkt. Gwajima D

Mhe. Dkt Dorothy Gwajima tunaomba msaada wako katika wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kutambua kwamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa (Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) na Kanda ya Mashariki (Tabora, Kigoma na Katav) hakuna kabisa vyuo vya Degree vya Sheria wala Sayansi. (Nimeambatanisha Pdf ya vyuo vya degree )

Wanawake na Wasichana wanabaki nyuma kielimu:
Ukosefu wa vyuo vya karibu unaathiri zaidi wanawake, ambao mara nyingi hawaruhusiwi kusafiri mbali au hushindwa kwa sababu ya ukosefu wa usaidizi wa kifamilia. Hii inasababisha watoto wa kike kukatisha masomo na kuwa hatarini kuingia kuolewa badala ya kuendelea masomo.

Makundi maalum kama wenye ulemavu hushindwa kabisa kupata elimu ya juu:
Umbali na mazingira magumu ya kusafiri kwao ni kizuizi kikubwa. Bila vyuo vya karibu, ndoto zao zinazimika kabla hata hazijaanza.

Walezi, hasa wanawake wanabeba mzigo mzito wa kifedha na kihisia:
Wanachukua mikopo ya riba kubwa, kuuza mashamba ya urithi, ili kumpeleka mtoto mikoa ya mbali kusoma. Huu ni mzigo wa kimfumo unaoweza kupunguzwa kwa kuwa na vyuo karibu. mtoto akiwa karibu gharama za usafiri, chakula, malazi, zinaweza kupunguzwa akisomea nyumbani.

Elimu ni kichocheo cha maendeleo ya jamii:
Kwa kusaidia uwepo wa vyuo hivi, utakuwa unatoa fursa kwa mamilioni ya vijana hasa wanawake na makundi maalum kujikwamua kiuchumi, kijamii na kielimu. Utakuwa sehemu ya historia ya kupunguza pengo la elimu ambalo limeikumba kanda hii kwa miongo mingi.

Tunaomba Mheshimiwa:

  • Uwasilishe hoja hii katika vikao vya Serikali na Bunge.
  • Ushirikiane na Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuona namna ya kuharakisha uwepo wa angalau chuo kikuu kimoja cha Seikali Mwanza.
  • Kujenga kampasi za kudahili kozi za degree kwa vyuo vya sheria na sayansi (Mzumbe, Must, Udsm, n.k.) katika mikoa tajwa
  • Uandae kikao na wadau wa elimu wa kanda husika na wanawake wa jamii kujadili athari halisi.
  • Kuboresha miundo mbinu vyuoni kitaifa kwa watu wenye mahitaji maalum.
 

Attachments

Diploma na degree?
Anyway, tusubiri nilisikia kuna kozi TCU wamezi approve tayari
Uzi unahusu Degree, kozi zimeshatolewa kwa vyuo vyote vitavyodahili wanafunzi mwaka huu, hicho chuo kuna kozi moja tu
 
SHIDA YA WATU WA KIGOMA UBISHI NA UJUAJI.

1.MUHIMBILI WAMEANZA UJENZI WA CHUO KIKUU CHA MUHAS CAMPUS YA KIGOMA NA UJENZI UNAENDELEA upo katika hatua nzuri

2.TIA wanajenga chuo CAMPUS na ushakamilika kina mpango wa kupokea wanafunzi takribani 300+

3.Kagera UDSM wanajenga campus yao mkoa kagera.

4.Katavi Sua wanajenga campus.

Waha punguzeni ujuaji muwe mnafuatilia vitu Mimi Niko mkoa wenu mna ujuaji sana
 

Attachments

  • FB_IMG_17531889652462478.jpg
    217.7 KB · Views: 23
  • FB_IMG_17531889456417707.jpg
    376.5 KB · Views: 26
  • FB_IMG_17531889335795482.jpg
    450.5 KB · Views: 28
  • FB_IMG_17531888087381971.jpg
    478.2 KB · Views: 24
  • FB_IMG_17531887249595262.jpg
    80.8 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…