Umetengeneza static charge mwilini. Mwili unaweza kuwa charged aidha kama una carpet kwako na ukawa unatembea juu ya hilo carpet ukiwa umevaa leather shoes au kuvaa nguo ambazo ni synthetic (Kama vile Polyesters). Sasa unaposhika kitu ambacho kinapitisha umeme ambacho kina potential tofauti na wewe static charges zilizopo kwako zinakuwa zinataka kuflow ili kuleta usawa katika potential. Jambo la kufanya nenda ukashike material ambayo ipo grounded, kwa mfano bodi la gari ili udischarge.
Rai yangu kwa vijana wa Kitanzania punguzeni pumba. Ukisoma comment nyingi humu ni pumba tupu. Kama jambo hulijui basi acha anayelijua alitolee ufafanuzi. Busara ni pale unapoanza kukubali kuwa kuna mambo mengi huyajui.