Mikopo kwa njia ya simu kilio kipya kwa Watanzania

Mikopo kwa njia ya simu kilio kipya kwa Watanzania

emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
acha utani mkuu udaiwe 1000, unyimwe mkopo wa 30m, kweli aliwezekani oficer mkopo wako anamatatizo na hataki kukusaidia, labda ni njia yake ya kuomba percetage, uwe macho.
Jaribu ndo utajua kama ni utani
Usikope! Naenda taratibu, wakati mwingine ukinyimwa Mkopo shukuru tu, hivi 30m riba yake ni kiasi gani? Utumwa huu Ndugu zangu, unaweza kukuza biashara taratibu tu bila presha pia!
Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye hana mkopo, riba inategemea na muda wa kurejesha
 
Hata hivyo waliniambia nikajaze fomu, mimi tu nijafanya hivyo. Ina maana kwa watumishi huu mfumo wa ESS umeunganishwa na hizo system za kungamua wadaiwa sugu
Fomu ya mkopo ukijaza kuna ingine unajaza kuruhusu taarifa zako zipelekwe credit reference bureau kujua taarifa zako za ukopaji na ulipaji ukoje hapo ndio penye shughuli pevu

System lazima itapike nyongo kama mtu mkopaji sugu kulipa popote
 
Fomu ya mkopo ukijaza kuna ingine unajaza kuruhusu taarifa zako zipelekwe credit reference bureau kujua taarifa zako za ukopaji na ulipaji ukoje hapo ndio penye shughuli pevu

System lazima itapike nyongo kama mtu mkopaji sugu kulipa popote
Naachana nao ngoja niwekeze kwenye saccoss ya ofisini.
 
T
Ni wewe tu una ongezewa viwango kadiri unavyokopa na kulipa wanakupima uaminifu wako tu

Wako watu wengi tu mbona akihitaji milioni sekunde tu mzigo unaingia na wako kibao mitandao yote tu milioni kitu kidogo mno cha msingi kuwa mwaminifu kukopa na kulipa .Huhitaji kupanga foleni kukopa benki au kujaza mikaratasi kibao na midhamana kibao kukopa milioni moja

Pesa kama hiyo ni kukopa simu kiganjani tu au online si ya kuzurura hata kwa ndugu kuomba

Simu zimekuja kurahisisha maisha kuna watu hawataki
Tatizo WA Tanzania wanadhani alie mkopesha ni bwege hana akilia anampaje pesa wakati hamjui.
 
Jaribu ndo utajua kama ni utani

Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye hana mkopo, riba inategemea na muda wa kurejesha

Ninafanya biashara ya sales ya about “: $400,000 Kwa mwaka, kipindi cha Kikwetw ilifika $600,000

Nishawahi kufuatwa na Bank kukopeshwa, nataka nikueleze sijawahi kopa Bank life time yangu!

Nimewahi kopa mzigo, mali kauli, stock with no interests na kwa wadau wa Karibu, But Bank, never and forever I will not!
 
Ninafanya biashara ya sales ya about “: $400,000 Kwa mwaka, kipindi cha Kikwetw ilifika $600,000

Nishawahi kufuatwa na Bank kukopeshwa, nataka nikueleze sijawahi kopa Bank life time yangu!

Nimewahi kopa mzigo, mali kauli, stock with no interests na kwa wadau wa Karibu, But Bank, never and forever I will not!
$400,000 annual sales hiyo turn-over sio mbaya kama sio kazi ya uagent wa bidhaa za watu, zenye high sales faida kidogo, kama soft drinks beer supermarket nk
 
Wanajamvi habari zenu,

Kama kawaida nikikutana na kitu kipya lazima nikileta hapa kwa faida ya wengine. Ni kwamba wiki iliyopita nilikuwa nimeomba mkopo wa milioni 30 hivi kwenye mojawapo ya benki hapa nchini. Hii benki nimekuwa mteja wao tangu 2006 kama sikosei nimeshakopa kwao kwa zaidi ya mara tatu hii ikiwa ya nne. Ajabu ni kwamba, baada ya kufanya process zote za mkopo nilipigiwa simu nikaambiwa sitopewa mkopo kwa sababu mimi ni mdaiwa wa Sugu wa Mpewa nina deni la tangu mwaka 2020. Nilistuka kidogo lakini nikasema ngoja nifuatilie, hatua ya kwanza nilipiga simu Vodacom huduma kwa wateja kujua katika line zangu mbili za voda ni ipi ina deni?

Majibu kutoka Vodacom walinambia line zote hazina madeni isipokuwa kuna line moja likopa shilingi elfu 5 na ikawa muda wa kurejesha umepita. Hivo wakati deni linalipwa tayari taarifa zangu zilishaenda huko CRB kama mdaiwa Sugu. HII NI LINE AMBAYO ALIKUWA ANAITUMIA KIJANA WANGU CHUO kwa sababu wakati anaingia chuo alikuwa na miaka 16 kwa sababu alichagua kusoma kwa njia ya Cert, Diploma & Degree.

NI NINI CHA KUFANYA hili lilikuwa swali la pili. Jibu likawa kwamba nenda ofisi za vodacom zilizokaribu nawe ili upate ufafanuzi zaidi. Baada ya kufika Vodashop. Majibu ya Vodacom nenda NCBA Benki upate ufafanuzi zaidi. NCBA kwa official letter kabisa wakajibu hakuna deni na wakaonyesha tarehe ya mkopo na tarehe ambayo mkopo ulilipwa.

SWALI TENA NINI CHA KUFANYA KUCLEAR TAARIFA ZANGU HUKO CREDITINFO, jibu wapigie Simu, baada ya kupiga simu nikajieleza kisha nikaelekezwa kwenye Website yao ambapo nilijaza form ili kupewa taarifa zangu.
Majibu yalikuja ya ina mbili kwamba lile deni la Mpawa lilipwa lakini kwa kuchelewa hivo hizo taarifa zitabaki hivo kwa kipindi cha miaka sita tangu deni kulipwa.

MAAJABU SASA: Hata hii benki niliyokuwa ninaomba mkopo kwao nayo imeniorodhesha kama mdaiwa sugu kwa mikopo yote miwili ambayo yote nilishalipa nikamaliza. mkopo 2019 - 2022 na mkopo 2023 - 2024 ambayo yote imelipwa. Kwani baada ya kumaliza mkopo wa pili niliomba mkopo mwingine ambao ni watatu na sijafanya TOPUP.

Hili la benki nimefungua Dispute kupitia CRB ambaye ataawandikia ili wanijibu ndani ya siku 15 wakishindwa kufanya hivo nitakuwa huru kuwashitaki kwa Defamention. KUHUSU MKOPO WA BENKI NISUBIRI MPAKA MIAKA 6 IPITE.

Wasi wasi wangu ni kuwa kuna watu wengi sana ambao ama kwa kujua au kutojua huenda majina yao yako CRB na wako Blacklisted, kwa sababu kuna watu wamesajiri line za simu ambazo zinatumiwa na ama watoto, house girl, shamba boy nk. Katika hili nadhani CRB wangeangalia namna nyingine ya kurekodi taarifa wanazopokea kutoka kwa CREDITORS.

Mwisho nimenyimwa loan ya milioni 30 kwa sababu tu ya kucheleweshwa Deni la shilini elfu 5 ambayo iko chini ya NCBA.
Chai
 
Technology inakua siku hadi siku, kwa dunia ya leo mtu akishakua na taarifa zako za Nida anakua amemaliza kila kitu
 
Ahahah aisee..kwahiyo wewe una relax na zile text wanazotukia watu wako wa karibu?????? Au hao hawana tabia hizo??
iko hivi mimi nilikopa pesa x wakanipa elf 25 siku ya kulipa bado siku moja wakaanza sim na ahadi kibao ukilipa mkopo tunakuongezea hela mimi fasta nikalipa huwez amini wakagoma kunipa tena chance ya kukopa nikaja kujaribu cash x ikaingia hela sasa wakaanza sim zisizoisha namb zinapishana mpya mpya mimi sipokei mwisho wakaanza kunitumia mimeseji ya kijinga wasap nikawa najibu mbona mnadai kama nimekopa mamilioni ya hela mara rudisha hela tunakutangaza kama mdaiwa sugu nikawaambiabsawa tangazeni hela yenu silipi meseji za vitisho za matusi nishaitwa sana mbwa malaya sasa mm nalipa iweje kwa mfano?
 
Back
Top Bottom