Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Bank zote zinafuata masharti kuwa ni lazima 1/3 ya mshara wako baada Kodi, hifadhi ys Jamii inabaki kwa ajili ya familia. Zaidi ya hapo hakuna Afisa Utumishi anaweza ingiza makato hayo! Kwanza Posta, pili crdb na nmb ni mwisho
 
Bank zote zinafuata masharti kuwa ni lazima 1/3 ya mshara wako baada Kodi, hifadhi ys Jamii inabaki kwa ajili ya familia. Zaidi ya hapo hakuna Afisa Utumishi anaweza ingiza makato hayo! Kwanza Posta, pili crdb na nmb ni mwisho
Mh.tutanachotaka kujua ktk mikopo ya benki ni hiki
1.Percentage ya riba ya mkopo
2.Urahisi wa kupata mkopo(Kwa maana ya mahitaji ya viambatisho pamoja na muda wa kupokea..)
3. Ukubwa wa makato yao
4. Muda wa kukaa na mkopo eg.Miaka 3,4,5,6,au 7?
Ukitupatia haya kwa ulinganisho wa benki zote basi tunakuwa na nafasi nzuri ya kuchagua.Lakini kusema tu CRDB is the best mara Posta mara NMB mwingine ACB..n.k haitatusaidia.
 
Tangu uzi uanze hadi leo crdb ana point nyingi
So crdb ndio bank bora ya kuchukulia loan kwa wafanyakazi

Naafiki hoja hii....kikubwa kinachonivutia ni uwazi wa gharama za mkopo na riba...hakuna figisufigisu katika hili..
 
Kigezo, inabidi utupe Kigezo maana wengineo wanasema kwamba Tanzania Postal Bank wapo vizuri sana

Tafta mtaalamu akukokotoleee mfumo wa riba za mabenk...kisha linganisha. Lakin njia rahisi sana ni wewe kwenda bank tatu tofaut kuuliza kama nitakopa mfano tsh 10 kwa miaka 5 kila mwez nitalipa tsh ngap?! Kisha kila benk watakupa rejesho la kila mwezi...sasa chukua hilo rejesho..zidisha mara muda mkopo ya miez 60...tizama ni benk ipi jumla ya marejesho itakuwa nafuu kuliko ingine...hapo utakuwa umepata jibu. Pia muhimu sana kuwauliza gharama za mkopo ni kiasi gani.
 
Ukifuatilia maelezo haya from the begining up to this point, aaah huna haja ya kuweweseka taarifa nyingi kwa 90% zimechambuliwa hapa, kinacho baki ni mtu binafsi kuamua ni Bank ipi itakidhi mahitaj yako.
 
=========================================================================== Kwa maelezo yako hapo juu tofauti ya riba ipo kama ifuatavyo:-

1. Tsh. 11,300,000/- kwa miaka 6 na makato ya Tsh. 257,000/- kwa mwezi ni sawa na riba ya 18% kwa mwaka/per annum au 1.5% kwa mwezi.
2. Tsh. 9,500,000/- kwa miaka 6, kwa makato ya Tsh. 251,000/- kwa mwezi ni sawa na riba ya 24% kwa mwaka au 2% kwa mwezi.

Note: Viwango vya mkopo ulivyotaja ni tofauti kama vinavyoonekana hapo juu (Bolded)

- Hivyo kwa uwiano sawa wa viwango vya mkopo makato ni kama ifuatavyo:-

4. Tsh, 11,300,000/- kwa miaka 6 na riba ya 18% au 24% itapelekea makato ya Tsh. 257,728.04 (18%) au 297,493.19 (24%)
5. Vivyo hivyo Tsh. 9,5000,000/- itapelekea makato ya Tsh. 216,674.02 kwa riba ya (18%) au Tsh. 250,104.89 kwa riba ya 24%

Hope umeona tofauti.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Miaka 6×12= miezi 72, 72×257,728.04= 18556418.9 hii riba mbona kubwa sana.
 
Miaka 6×12= miezi 72, 72×257,728.04= 18556418.9 hii riba mbona kubwa sana.
===========================================================================
Kadri muda wa malipo unapoongezeka vivyo hivyo malipo ya mkopo yanakuwa makubwa ! Njia nzuri ni kupunguza muda wa kulipa mkopo kama uwezo wa kufanya hivyo upo ! Mfano ukichukua mkopo huo huo wa Tsh. 11,300,000/- kwa riba ya 18% kwa mwaka na kuamua kurejesha kwa muda wa miaka 3 badala ya 6 utatakiwa kurejesha Tsh. 408,522.07 kwa mwezi ambazo ni sawa na jumla ya Tsh. 14,706,794.50 kwa miaka 3 ya mrejesho !

Meaning: Hapa utakuwa umepunguza malipo ya Tsh. 18,556,418.90 - Tsh. 14,706,794.50 = Tsh. 3,849,624.40 kama utaamua kurejesha mkopo huohuo kwa kipindi cha miaka 3 badala ya 6.

Hope umeona tofauti kwa maana ya kuwa kadri muda unavyoongezeka marejesho nayo yanakuwa makubwa ingawaje utaona malipo kwa mwezi ni madogo.
===========================================================================
 
Ni bonge la uzi nimevuna mengi. Ila bado sijapata jibu nikope crdb au nmb au posta.
Mimi nataka nikope nijenge angalau kajumba ka vyumba vitatu sebule dining jiko na stoo. Je mkopo wa JIJENGE wa crdb utanifaa au nisawa na mikopo yao mingine?

ushauri wa bure ndugu! ukikopa hakikisha usijengee pesa yote jitahidi kwa buni ka mradi fulani weka mipango vizuri ukikopa tu kiasi cha ule mkopo ufamyie biashara itakayoingiza fedha karibia au sawa na ile unayokatwa. vinginevyo mkopo wa ujenzi unaumiza sana nilikopa nikajenga najua ilivyo! ukiwa nakabiashara haitakuumiza sana
 
Duuuh mi nataka nimkate sahivi ana mwaka
Mfanyie haina tatizo mkuu kama kaumbwa na maumbile madogo hata akikaa na govi lake hakuna kitakacho badirika ni kujidanganya tu.
NMB wasumbufu Sana. Maloan officer wanaringa, wasumbufu na wanapenda kuachiwa hela kidogo. Watabakia na wafanyakaz wachache Sana kwasababu hawataki kubadilika kuendana na ushindani wa kibiashara. Mtu unakopa ila unanyanyaswa unadhan unaomba msaada.
Ni kweli mkuu hasa maloan officer wa pale kisarawe yaan wako very slow watu sita mnashinda mmekaa siku nzima bado jamaa hawamalizi kuwahudumia, kiukweli mnaitia hasara benk mnatoa huduma hafifu kiasi kwamba benki inapoteza wateja kwa ajili yenu na uzembe wetu.
 
Mikopo mizuri ya wafanyakazi ipo Benki ya Posta.
pia kuna mikopo kama:
- YA VIKUNDI, just cha watu 5-10
-SACCOS
-VICOBA
-WASTAAFU wa PSPF,PPF,NSSF,GEPF,LAPF
-WAFANYAKAZI
-YA ELIMU KWA WANAOCHANGIA PSPF na GEPF
-YA KUANZA MAISHA KWA WANAOCHANGIA PSPF NA GEPF
-BIASHARA KUBWA
-BIASHARA NDOGO NDOGO
Pia,

mikopo ya wafanyakazi inatolewa hadi miaka 6 na kwa wastaafu hadi miaka 4

Riba zao ziko chini sana yaani wafanyakazi ni 13 kwa waajiri wazuri na 15 kwa waajiri wanaochelewesha makato.

Tembelea tawi la Benki ya Posta lililoko karibu kuthibitisha haya.
Mtu akikopa mil 9 kwa miaka 6 makato yanakuwa kiasi gani mkuu
 
kitu kingine unaambiwa ribs ni 18% kila ukicalculate inakuja kama 76% hivi wanatumia formula gani tujuzane hapo wataalamu wa hayo mambo
 
Ukiambiwa ukweli utaogopa kukopa.riba ni 18% kwa kila mwaka!hivyo nionavyo ni 18%×kiasi cha mkopo ×miaka 6
 
nilienda kuuliza bank mbili juzi. nikaanza na crdb wakaniambia kwa salari yangu maximum watanipa 11,300,000 kwa miaka 6 na watanikata 257,000. nikaenda nmb wakaniambia maximum watanipa 9,500,000 na watanikata 251,000. Kimsingi hakuna tofauti za riba
Hivi hayo makato wanakata kila mwezi hadi miaka sita iishe!?
 
Back
Top Bottom