Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

nilienda kuuliza bank mbili juzi. nikaanza na crdb wakaniambia kwa salari yangu maximum watanipa 11,300,000 kwa miaka 6 na watanikata 257,000. nikaenda nmb wakaniambia maximum watanipa 9,500,000 na watanikata 251,000. Kimsingi hakuna tofauti za riba
Upo taasisi gani mkuu?
 
jamNi wamesharudisha huduma, nackia kama mtu alishakopa akataka Ku top up anaweza, licha ya benk kusimamisha ukopaji, je ni kweli??? wajuvi tusaidiane aisssee
 
crdb inatoa mikopo mikubwa ila wana process ndefu hadi wakupatie.nmb wanamikopo midogo ila wanakupa ndani ya muda mfupi sana unaweza ukaanza process ndani ya siku tatu ukachukua mkopo. ukitaka mikopo yenye hela ndefu nenda EQUITY wanaweza kukupa hadi mil20 wanabranch yao mwenge na bagamoyo ila sijajua kwa mikoani.pia ukitaka kukopa inashauriwa nenda kakope mwezi wa sita maana benki nyingi huongeza viwango vya kukopesha.pia kama unataka kukopa bila riba unaweza kwenda kukopa PBZ ipo mtaa wa lumumba,karibu na ofisi ndogo ya ccm hapa dar es salaam,wanatoa mikopo mizuri hata kama mshahara wako unapitia kwenye benki nyingine ila wao hutaka wakukute kwanza kwa miezi mitatu ndo wakukopeshe unachotaka ukopeshwe.

Riba za EQUITY kwa mwaka ni asilimia ngapi !?
 
Acha kupotosha mkuu..
Riba ya CRDB kwa personal loans zote ni 18%(ikihusisha na 1% ya bima ndani yake) wala sio 24% kama unavodai.
Ila mkopo wowote wa Crdb kama ilivyo kwa benki nyingine lzm kuwepo na ada.
●Kwa CRDB iko ni 1.1% ya mkopo ni Loan application fee na minimum ni 110,000
●0.55% ya mkopo ni Loan processing fee na minimum ni 55,000
Kwa mfano mikopo yote inayoanzia 5,000,000 na kushuka had 1,500,000 ada yake ni 165,000 tu(minimum threshold) ambayo ni one-time fee.
●Na kuanzia mwezi Disemba mwaka CRDB inakopesha hadi miaka 6.
Huu ndo ukweli na huhitaji kujua mimi ni nani CRDB ili uniamini

Maelezo mazuri !! Naweza kuchukua mkopo CRDB huku nikiwa na mkopo benki ingine as long as msharaha unapitia CRDB !!??
 
Kama umechukua Mil 4.5
Wanakata 132,000 kwa miaka 5 yenye miezi 12
132,000*5*12=7,920,000
7,920,000-4,500,000=3,420,000
3,420,000/4,500,000*100=76%

Apo ni asilimia 76% apo unakuwa unaifanyia kazi benki
Asilimia kubwa ktk maesabu mabenki ayawaeleweshi vizuri watu

Absolutely !! Mkopo ni mzuri kama unauwezo wa kuurudisha kwa kipindi kifupi !!
 
Wakuu baada ya kufanya utafiti kidogo na kuongea na ma afisa mikopo wa hizi benki mbili nimefikia hitimisho CRDB ni bora labda sijajua kuhusu malalamiko ya kuchelewesha kuweka mkopo. Nmb wanaweka fasta ila wizi wao umekubuhu yani eti mkopo wa 10,700,000 wananipa 10,138,250 nyingne wanakata kama processing fee na bima.

Mkuu ulitakiwa uwe mdadisi wa kujua gharama zinginezo zinazohusiana/zinazoambatana na mkopo ili kufanya maamuzi sahihi !
 
Kigezo, inabidi utupe Kigezo maana wengineo wanasema kwamba Tanzania Postal Bank wapo vizuri sana

I doubt !! Mkopo wa TZS 9,500,000/- kwa miaka 3 kwa makato ya TZS 392,044.83 Vs TZS 343,447.76 kwa riba za 13% Vs 18% PER ANNUM respectively !! Hope umenipata !!!!!
 
Bado nina wasiwasi mkubwa na hizi bank. Inakuaje unaambiwa tuna riba 15%(Benki ya posta? lkn pesa wanayokupa ni ndogo kuliko wa anayekwambia riba ni 18%(NMB na CRDB)?
 
I doubt !! Mkopo wa TZS 9,500,000/- kwa miaka 3 kwa makato ya TZS 392,044.83 Vs TZS 343,447.76 kwa riba za 13% Vs 18% PER ANNUM respectively !! Hope umenipata !!!!!
Mkuu fafanua
 
Kama umechukua Mil 4.5
Wanakata 132,000 kwa miaka 5 yenye miezi 12
132,000*5*12=7,920,000
7,920,000-4,500,000=3,420,000
3,420,000/4,500,000*100=76%

Apo ni asilimia 76% apo unakuwa unaifanyia kazi benki
Asilimia kubwa ktk maesabu mabenki ayawaeleweshi vizuri watu
Men Lie.....Women Lie but NUMBERS DON'T LIE!!!!Sitaki Mkopo!!
 
Mkuu fafanua

Mkuu hujanipata !!!! Inaweza kuwa ni kutokana na matumizi ya "VIKOKOTOZI" tofauti !!! Hii mikopo unahitaji kuwa mdadisi na kutokuwa na haraka !!!
 
Makato ya 250,000 kwa mwezi kwa miaka mi5 nitapatiwa being gani kama mkopo nje na riba wadau...
 
Kuna mtu leo ameenda kuuliza mkopo CRDB akaambiwa sasa hivi ni hadi mshahara wako upitie kwao
 
Kuna mtu leo ameenda kuuliza mkopo CRDB akaambiwa sasa hivi ni hadi mshahara wako upitie kwao
Nahisi ni kwasbb ya hizi issue za uhakiki...wa watumishi...sasa hawana uhakika kama bado umo kwenye payrol ya serikali au ndo tayari yale mambo yetu....eeh...yah...u kno!
 
===========================================================================
Kadri muda wa malipo unapoongezeka vivyo hivyo malipo ya mkopo yanakuwa makubwa ! Njia nzuri ni kupunguza muda wa kulipa mkopo kama uwezo wa kufanya hivyo upo ! Mfano ukichukua mkopo huo huo wa Tsh. 11,300,000/- kwa riba ya 18% kwa mwaka na kuamua kurejesha kwa muda wa miaka 3 badala ya 6 utatakiwa kurejesha Tsh. 408,522.07 kwa mwezi ambazo ni sawa na jumla ya Tsh. 14,706,794.50 kwa miaka 3 ya mrejesho !

Meaning: Hapa utakuwa umepunguza malipo ya Tsh. 18,556,418.90 - Tsh. 14,706,794.50 = Tsh. 3,849,624.40 kama utaamua kurejesha mkopo huohuo kwa kipindi cha miaka 3 badala ya 6.

Hope umeona tofauti kwa maana ya kuwa kadri muda unavyoongezeka marejesho nayo yanakuwa makubwa ingawaje utaona malipo kwa mwezi ni madogo.
===========================================================================
mtu huweza ku topup baada ya muda gani tangu achukue mkopo? taratibu zipoje kama unajua lolote
natanguliza shukrani za dhati.
Madam Mwajuma
 
Back
Top Bottom