Mikopo na sera mbovu za ubinafsishaji ndizo zimetufikisha hapa, Mwaka 2000 exchange rate ilikuwa(1 Usd=Tshs 803.3)

Kama anataka kuondoka na dola basi afanye biashara ya kuingiza dola. Yaani export business. Unaalika mtu kuja kuendesha mwendokasi. Anaingiza Tsh halafu wakati wa kuondosha faida anabadilisha kuwa dola!! Mbona tunakuwa tunafanya biashara kichaa.
Hapo nimekupata
Ila bado kutakua na changamoto
Muwekezaji anakaa nchi ambayo haitumii shilingi
Ni lazima aibadili kua pesa inayotumika kwake
Huoni hapo haitowezekana ,
 
No kweli lakini tukubaliane na ukweli kuwa;-

Hali ya maisha ya Sasa sio sawa na zama hizo unazozisema!

Exchange rate haijatokea Tanzania pekee hata kwa wenzetu huko Hali ipo hivyo hivyo!!hakuna condition ambayo ni permanent static ulimwenguni Bali ni dynamic kote!
 
Juzi nimemsikia Barozi wa Tanzania aliepo UK alienda soko moja la kimataifa hapo UK kuangalia bidhaa zinazotoka Afrika na Tanzania kwa bidhaa za Tanzania alikuta ipo moja tu alishangaa sana kwa kuwa hajui changamoto za kupata vibali ambavyo vinalipiwa kwa usd hapa na usd yenyewe ndio hiyo inaenda kwa rate ya 2800 mpaka 3000...
 
Je, kama hao viongozi wa juu kabisa wanashirikiana na hao wanaowateua kuiba watasaini vipi kunyongwa?? Labda wasaini kunyongwa vidagaa. Hata kesi za uhujumu uchumi, kesi za rushwa na nyinginezo mahakamani ni za vidagaa. Hapo unafikiri kuna nia ya dhati?? Unafikiri tutatoboa!??
 
Yote yanawezekana tukipata Katiba mpya itakayopunguza madaraka ya Rais.
 
CCM imezeeka ndugu yangu, tukipumzishe haraka.
 
Sie tunaongelea Nchi yetu,

Hadi Nyerere anatoka madarakani 1usd ilibadilishwa Kwa Tshs 10 pekee.

Alipoingia Mwinyi na kuruhusu soko huria vitu vikaingia Kwa wingi nchini hivyo mahitaji ya Dollar yakiongezeka, viwanda vya ndani vikakosa soko kuuza bidhaa nje ya Nchi, exports zikashuka, hazina ya dollar ikashuka na kupeleka inflation kukua hivyo thamani ya pesa ikashuka,

Mwaka 1985, dollar ikapanda Toka ilivyokuwa 1usd Kwa 10 shs ikafika 1usd Kwa 230 Tshs.

Sasa ongezeko Hilo huoni Lina uhusiano na sera za kuruhusu imports kiholela bila kujali viwanda vya ndani?

Na katika kipindi hicho pia, Nchi ilikopa sana, hivyo kuongeza upungufu wa pesa za kigeni kulipia Riba na mikopo.

Awamu ya Mkapa vile vile, ikaruhusu viwanda kubinafsishwa Kwa wageni ambao wakahujumi vikafa kabisa, imports zikazidi exports hivyo kupunguza zaidi thamani ya Shilingi yetu.

Tuchambue Takwimu mwalimu.

Tafiti ipingwe Kwa tafiti!!


KaribuπŸ™
 
Tafsiri ni rahisi tuu,kama hutaki kukopa lipa Kodi zaidi.
 
Kama hutaki kukopa kopesha, uza Kwa majirani huko duniani upate hazina ya dollar!!

Nchi haiwezi KUPIGA hatua Kwa kuvuna wasichopanda!!
Tukopeshe nini? Utauza ambacho hujazalisha.

Mwisho mikopo sio msaada ni pesa italiowa inatumika kujenga base ya hayo unayoeleza hapo Juu.
 
Tukopeshe nini? Utauza ambacho hujazalisha.

Mwisho mikopo sio msaada ni pesa italiowa inatumika kujenga base ya hayo unayoeleza hapo Juu.
Lini mmewahi kukopeshwa wakulima Ili mjenge viwanda vya parachichi?

Sasa ukikopa Kisha ukajengea madarasa na matundu ya vyoo, Kuna biashara Gani shuleni itakayorudisha mkopo Ili kulipa deni?
 
Lini mmewahi kukopeshwa wakulima Ili mjenge viwanda vya parachichi?

Sasa ukikopa Kisha ukajengea madarasa na matundu ya vyoo, Kuna biashara Gani shuleni itakayorudisha mkopo Ili kulipa deni?
Ni wapi au Nchi gani wajinga na wapumbavu waliwahi leta maendeleo kwenye Nchi? Nitajie Moja tuu kabla ya kujiona hamnazo.

Mwisho Kwa hiyo Trilioni 26 zilizokopwa zimeelekwzwa kwenye madarasa na vyok au? Kichwani uko sawa sawa?
 
Ni wapi au Nchi gani wajinga na wapumbavu waliwahi leta maendeleo kwenye Nchi? Nitajie Moja tuu kabla ya kujiona hamnazo.

Mwisho Kwa hiyo Trilioni 26 zilizokopwa zimeelekwzwa kwenye madarasa na vyok au? Kichwani uko sawa sawa?
Ulichokiandika hapo juu umekielewa?

Wakulima wa parachichi, kahawa, nk nk ndio hao unaowaita wapumbavu?
 
Ulichokiandika hapo juu umekielewa?
Jibu swali,ni Nchi gani imewahi endelea Kwa kuendekeza wajinga na wapumbavu? Wewe si umesema haitakiwi kuwekeza kwenye Elimu au unajitoa ufahamu? πŸ˜‚πŸ˜‚

Pili ,Je 26 Trilioni zimewekezwa kujenga madarasa na vyok kama ulivyosema?

Leta majibu wewe nyumbu
 
Huna HOJA,

Huwezi kopa Ili ujengee vyoo na madarasa!!

Mkopo unatakiwa uende kufufua uchumi, watu, viwanda vipate mikopo ya Riba nafuu Ili mzunguko na Kodi iongezeke,

Makusanyo na faida baada ya kulipa Riba na mkopo ndio unajengea madarasa na vyoo.

Uchumi wa Nchi, ni sawa tu na Uchumi wa familia,

Nchi inapokopa kujenga vyoo, Haina tofauti na baba wa family anayekopa Ili kuongeza mke wa pili.

Ambapo katika uhalisia, mkopo ungetumika kuendelea biashara, angepata faidi na kukuza mtaji Kisha akatumia faida kununulia makochi nk nk.
 
Hoja ni kwamba umeshindwa kujibu swali langu la kunitajia Nchi iliyopata maendeleo Kwa kutegemea wajinga mfano wako bila.kuwekeza kwenye Elimu.So acha kujikanyaga kanyaga.

Pili Ukisikia neno Capital unaelewaje? Unayajua mawanda yake?
Mwisho hata ujenge Barabara sijui vitu gani kama una watu mbumbumbu wewe ni useless na inamwaga maji kwenye net,ndio maana sio tuu madarasa na vyok vinajengwa Bali Kila Mkoa kunajengwa Chuo Kikuu au Tawi la Chuo Kikuu Kupitia Mkopo wa WB kupitia mradi wa HEET

View: https://www.instagram.com/reel/C73nSbdswGw/?igsh=MTl6eTUxZmU1MDc4Yg==
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…