Mikopo na sera mbovu za ubinafsishaji ndizo zimetufikisha hapa, Mwaka 2000 exchange rate ilikuwa(1 Usd=Tshs 803.3)

Mikopo na sera mbovu za ubinafsishaji ndizo zimetufikisha hapa, Mwaka 2000 exchange rate ilikuwa(1 Usd=Tshs 803.3)

Tunaishi kwenye combination ya Monarchy mated with Oligarchy in stealth mode ila nchi inaitwa ni ya kidemokrasia mbele ya macho ya dunia.

Kuna mizee yenyewe imejikasimisha madaraka na inataka wao na vizazi vyao waendelee kuhodhi madaraka while the rest of us just toiling hard to make ends meet.

Option pekee naona ni umwagaji damu tu. Without it hakuna mabadiliko yatatokea. Ni hadi makundi haya mawili ya clash. Maskini wachoke kuburuzwa waamue kustrike iwe balaa.
Naunga mkono hoja
 
Zaidi ya 70% ya export yetu inatokana na Madini,ambayo yanachukuliwa hapa kwenda kuuzwa huko Ulaya-kwa maana hii hizi export ni kama namba tu ambazo hazina impact yyt kiuchumi ndani ya nchi.
Kama wanunuzi wangekuwa wanakuja kununua haya madini hapa Nchini basi wangenunua kwa fedha yetu na fedha yetu ingepanda thamani.Vilvile Kama hii migodi ingekuwa inamilikiwa na Wawezekazi wa ndani hata kama wangekwenda kuuza nje basi wangerudi ndani wakileta hizo USD zinazotokana na faida na mwishowe wangepandisha uchumi na shilingi ya Nchi.

The so called uwekezaji kwenye Nchi aina ya Tanzania yenye viongozi wala rushwa na wananchi wajinga ni utahira.
 
Uchumi wa nchi unapimwa kwa uzalishaji na ufanisi wa balance of trade.
Umetumia njia ndefu Sana kufika kwenye hili hitimisho ambalo hasa ndiyo linatakiwa kuwa kiini cha mjadala huu.

Jee udhaifu wa sarafu yetu unasababishwa na sababu Gani ya kiuchumi!??

Maana uimara ama udhaifu wa sarafu ya nchi yoyote ile duniani hautokei kusikojulikana, bali huwa na chanzo chake cha kiuchumi.

China inazalisha kwa wingi bidhaa mbali mbali tena kwa gharama ndogo kwa Teknolojia ya kisasa na bora kabisa.

Sisi tunazalisha ama tunauza nini kwenye soko la kimataifa. Urari wetu wa kibiashara (balance of payment/trade) kimataifa ukoje!?

Kwa mtazamo wangu badala ya kujikita kujadili thamani ya sarafu yetu kimataifa, basi tujadili kwanza thamani ya uchumi wetu kimataifa.
 
Hii nchi inatakiwa ipate kiongozi mzalendo atakaye amua kusimamia sheria.
Nimekuja kugundua wanao ikwamisha Tanzania ni Marais hao hao tunawachagu hapa kidogo mwenye ahueni ni Nyerere.wengine wote ni chanzo cha haya matatizo yote.Na mbaya zaidi kwa mfumo wa kiutawala wa hii Nchi Rais ndio kila kitu-yani ni mfumo wa hovyo kweli.

Viongozi na wananchi wote hawawezi kufikiria na hata wakifikiria lazim fikra zao ziakisi ambacho kitampendeza Rais-hivi nchi ya namna hii inaweza kuendelea vipi?????.huyo huyo Rais na wafanya uamuzi wenzake wamejiwekea kinga ya kikatiba wasishutakiwe either wakiwepo au wasipokuwepo madarakani-viongozi wa namna hii ambao hakuna sheria ya kumwawajibisha anaanzaje kuwaza namna ya kuipeleka Nchi mbele kwa 50 yrs to come.

Yani Tanzania ni zaidi ya upumbavu.
 
Umetumia njia ndefu Sana kufika kwenye hili hitimisho ambalo hasa ndiyo linatakiwa kuwa kiini cha mjadala huu.

Jee udhaifu wa sarafu yetu unasababishwa na sababu Gani ya kiuchumi!??

Maana uimara ama udhaifu wa sarafu ya nchi yoyote ile duniani hautokei kusikojulikana, bali huwa na chanzo chake cha kiuchumi.

China inazalisha kwa wingi bidhaa mbali mbali tena kwa gharama ndogo kwa Teknolojia ya kisasa na bora kabisa.

Sisi tunazalisha ama tunauza nini kwenye soko la kimataifa. Urari wetu wa kibiashara (balance of payment/trade) kimataifa ukoje!?

Kwa mtazamo wangu badala ya kujikita kujadili thamani ya sarafu yetu kimataifa, basi tujadili kwanza thamani ya uchumi wetu kimataifa.
Mbona nimeanza kulisema hilo awali kabisa kwa kutumia mfano hai kabisa wa China?

Kama nilivyosema awali, pesa ni bidhaa kama bidhaa nyingine, thamani yake, kimsingi, inapatikana kwa forces za demand and supply.

Sasa kama Tanzania ina import mpaka toothpicks, halafu exports zake ni chache, na hizo chache karibu zote ni unprocessed raw materials ambayo inaacha value kubwa sana kwa kuto export processed goods, currency yetu itapanda thamani vipi?

Sisi tuna import kuliko tunavyo export. Pesa zetu hazina demand sana kwa sababu watu wengi hawaji kununua vitu kwetu. Kuna wakati nilirudi New York City kutoka Tanzania, nikawa nimejisahau nimerudi na shilingi za Tanzania (nilibadili dola nyingi nikawa nimemaliza likizo kabla ya kumaliza shilingi, nikazisahau shilingi kwenye begi mpaka nikarudi nazo New York City). Kufika New York City, nikagundua nina shikingi za Tanzania, nikatafuta Bureau de Change inayoweza kuchukua shilingi za Kitanzania na kunioa dola za US, sikupata. Hela haina demand, thamani inapatikana kwenye demand, hela itapandaje thamani?
 
Mwalimu hakuwahi kuza uchumi wowote zaidi ya kutumia hazina aliyoachiwa na wakoloni akaitumia vibaya kutaka kumrejesha swahiba wake madarakani dhidi ya idi amini zingine akazitapanya kwenye ukombozi wa nchi za Africa
 
Hizi hadithi za kwenye vijiwe vya kahawa usilete kwenye mjadala wa mada makini kama hii.
 
Unawezaje kukopa ukajengee vyoo vya mashuleni?

Shule ni huduma Si biashara,

Ulitakiwa tukope kuwezesha mitaji kwenye MABENKI yashusge interest rates za mikopo Ili watu wapate mitaji Uchumi ukue Kisha Serikali ichukue pesa kiduchu Toka faida kujenga vyoo,

Sasa kukopa ukaenda kujenga, huo Si Uchumi.
Kwanza ujinga sana
Unakopa kujenga vyoo kweli ,halafu unakusanya tozo kununua VX ,si upumbavu huu jamani
Nchi hii inakera sana
 
Salaam shalom!!

Tulipopata Uhuru wa Nchi yetu, hatukuwa na wawekezaji wengi wa kuwekeza kwenye migodi, Serikali ilihodhi vitega Uchumi vyote na kusimamia, Hawa wawekezaji wa sasa, nionavyo Si HAKI kuwaita wawekezaji Bali waporaji, na uporaji huo unashirikisha viongozi wetu wa ndani. Tulipopata uhuru, Dola Moja ya kimarekani, ilibadilishwa Kwa Tshs 7 tu!!

Nisikuchoshe, hii hapa ni historia ya Exchange rate tangu Uhuru Hadi hii Leo, chama Cha MAPINDUZI kikiwa madarakani.

1961.
1usd=7 Tshs

1971
1usd= 7.14 Tshs

1981
1usd=8.2 Tshs

1991
1usd=219 Tshs

2001
1 Usd=876.4 Tshs

2005
1 Usd=1,128.9 Tshs

2010
1usd =1,434.7 Tshs

2012
1usd= 1,600Tshs

2015
1usd=2,037.1 Tshs

2020
1usd=2,330.5

2024
1usd= 2,615 Tshs.

Source: Google, average Exchange Rate, University of Pennsylvania.

Awamu ya kwanza ya utawala wa mwalimu Nyerere Kwa miaka yote 24 aliyokaa madarakani, Dalar halikuwahi kubadilishwa Kwa zaidi ya Tshs 10 pekee!! Na wakati huo, Aliendesha Uchumi Kwa KILIMO PEKEE!! Uchumi wetu ulitegemea zaidi KILIMO Cha biashara na chakula, Tuliuza millions ya tons za mazao ya KILIMO na biashara.

Mambo yameanza kuharibika pale tulipoamua kuingiza sera za ubepari Uchwara, Tukaanza kuruhusu waporaji kushika uchumi wetu Kwa mlango wa Uwekezaji. Alipoingia tu Mzee Ruksa, ikapaa Kutoka Sh 10- tsh 200 kubadili Kwa 1 Usd. Kumbe tulitakiwa tuunde na kuwajenga wazawa ndio wapewe mashirika ya umma kujenga Nchi na kubakiza pesa nchini.

Tungetegemea, Uchimbaji wa Madini usaidie kuimarisha pesa yetu na Uchumi, lakini Cha kushangaza, Dhahabu inachimbwa, lakini Serikali inakosa pesa ya kufadhili budget na kulazimisha kukopa nje, sasa hiyo migodi Si ingefungwa tujue Moja? Tusubiri wazaliwe Watanzania ambao watakuwa na uwezo wa kuchimba Dhahabu yetu wenyewe, ituzwe benki kuu baada ya kununuliwa na Serikali Toka Kwa wachimbaji hao. Pesa yetu irudi kuwa yenye nguvu tena kama zamani.

Nchi yetu tunawezaje kusema tuna wawekezaji ambao hawaleti mchango wowote kwenye kuimarisha pesa yetu na Uchumi wetu?

Iweje tuwape wageni Bandari zetu kwamba wakusanye mapato Kwa weledi mkubwa Kisha tukose pesa ya kufinance budget yetu Kwa mwaka Hadi tulazimike kukopa tena?

SOLUTION.

1. Turudi na kukaa kama nchi na kutafakari tena kuhusu sera zetu za kiuchumi, maana uwekezaji haujaleta TIJA yoyote muhimu zaidi ya kutufanya kuwa maskini zaidi, tunahitaji Sera ambazo ni Mixture ya Ujamaa na Ubepari. Na ubepari huo uwe wa kudeal na Wazalendo wa ndani ya nchi ,wafadhiliwe mikopo Ili waendeshe Uchumi wa Nchi yetu.

2. MIKOPO ya nchi yetu isimamishwe. Iundwe Taasisi huru kikatiba, Taasisi hiyo impore Rais mamlaka ya kujihusisha na mikopo ya nchi, Taasisi hiyo ichakate taarifa nyeti na kuona namna Bora ya kujitegemea wenyewe tukishirikisha matajiri wazawa wa nchini, Dhahabu yetu na Raslimali zetu zimilikiwe na wazawa, hao ndio wafadhili budget ya Uchumi wetu.

3. Tukipumzishe chama Cha MAPINDUZI kuongoza nchi, nasisitiza point hii no 3!!

Vyama vya upinzani pia viangaliwe UPYA, maana Sera na maono Yao kiuchumi ni Yale Yale ya kuamini kuwa tunaweza kuleta wawekezaji Toka nje Kisha tukapata faida za kiuchumi kupitia uwekezaji Uchwara tukiweka rehani raslimali zetu Kwa wageni, tunahitaji vyama vya upinzani vyenye sura ya kizalendo na kuwa na Political na Economical INDEPENDENCE!! Vyama vya siasa nchini visizidi VITATU PEKEE!!!

4. Tupate Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote. Nchi yetu tusiwape wageni kiutawala kupitia sera mbovu na RUSHWA Kwa viongozi wetu ilhali Uchumi na Raslimali za nchi zinazidi kuondoka mikononi mwetu.

5. Tuongeze hasira juu ya Wala RUSHWA!! Rais asione haya kusaini death sentence, watu Wala RUSHWA wa level zote na uhujumu Uchumi wanyongwe, wasiogope, ukinyonga Wala RUSHWA watu hawataisha nchini, Bali wataacha vitendo vya RUSHWA.!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni🙏
Weka account ya dollar upige hela.
Viongozi wenyewe hawana uchungu na nchi halafu wewe ndiyo una uchungu na nchi.
Piga hela angalia maisha yako na kizazi chako
 
Kwanza ujinga sana
Unakopa kujenga vyoo kweli ,halafu unakusanya tozo kununua VX ,si upumbavu huu jamani
Nchi hii inakera sana
Badala ukope Kisha Benki zipewe pesa hizo na kupunguza interest rates Ili sekta ya Uchumi ikue,

Faida na Kodi utayopata hapo ndio ikajenge madarasa na vyoo,

RUSHWA ni tatizo kubwa Nchi hii.
 
Upo sahihi. Tena afadhali wawekezaji wa migodini ambao bidhaa wanazizalisha zinaingiza dola. Fikiria tunaleta muwekezaji anazalisha bidhaa anazouza humu humu ndani au anachezesha kamari. Huyu anatuuzia bidhaa kwa Tsh halafu anapopeleka faida kwao anazibadili kuwa dola na kuondoka nazo. Matokeo yake mahitaji ya dola na thamani yake inazidi kupanda na Tsh inazidi kushuka.

Ilitakiwa muwekezaji asiruhusiwe kuondoka na dola zaidi ya anazozalisha kwenye business yake au alizokuja nazo kama mtaji.
Hutopata muwekezaji huyo
Sasa hapo atakua amefanya nini
Yaani aje na Dola 1M mathalani ,apambane apate faida halafu siku ya kuondoka aondoke na Dola 1M ile ile , we kuweza mkuu?
 
Rate ya Bank inasoma hivyo ila mtaani watu wanauziana 2882 ilikua juzi hii ukitaka kwa hiyo ya Bank hauwezi kupata kitu naona inakimbilia Tsh 3000 kwa 1 usd...
Wahusika wapo bize na campaigh. One thing nimejifunza kuna ka utamaduni, kiongozi (si wote) akijua kazingua anakaa kimya, wenyewe wanasema (upepo upite), aka mbongo asahau.
No uwajibikaji
 
Weka account ya dollar upige hela.
Viongozi wenyewe hawana uchungu na nchi halafu wewe ndiyo una uchungu na nchi.
Piga hela angalia maisha yako na kizazi chako
Ukiwa na akili za aina hiyo unaweza hata kufanya biashara haramu ya drugs,au hata kuuza viungo vya binadamu.

Kundi dogo la wezi halitakiwi kukufanya ukose Uzalendo.

Ninaipenda sana Nchi yangu nzuri Tanzania.

Tuipende Nchi yetu. Amen
 
Zaidi ya 70% ya export yetu inatokana na Madini,ambayo yanachukuliwa hapa kwenda kuuzwa huko Ulaya-kwa maana hii hizi export ni kama namba tu ambazo hazina impact yyt kiuchumi ndani ya nchi.
Kama wanunuzi wangekuwa wanakuja kununua haya madini hapa Nchini basi wangenunua kwa fedha yetu na fedha yetu ingepanda thamani.Vilvile Kama hii migodi ingekuwa inamilikiwa na Wawezekazi wa ndani hata kama wangekwenda kuuza nje basi wangerudi ndani wakileta hizo USD zinazotokana na faida na mwishowe wangepandisha uchumi na shilingi ya Nchi.

The so called uwekezaji kwenye Nchi aina ya Tanzania yenye viongozi wala rushwa na wananchi wajinga ni utahira.
Bado hata huko kwenye exportation bado tabu tupu
Ukiwa na maparachichi Yako unataka uyauze uingereza kupata export permit ni mzunguko
Ukiwa na mahindi Yako unataka uyapeleke Kenya au Ethiopia shughuli yake si mchezo
Ukiwa na ngozi za ng'ombe unataka uwapelekee Gucci au LV kupata kibali sahau
Kwa hiyo hata export inauliwa na hao hao wanaotorosha dhahabu sababu ya ukiritimba na roho mbaya, matokeo yake tunabakia hoi kama nchi
 
Hutopata muwekezaji huyo
Sasa hapo atakua amefanya nini
Yaani aje na Dola 1M mathalani ,apambane apate faida halafu siku ya kuondoka aondoke na Dola 1M ile ile , we kuweza mkuu?
Kama anataka kuondoka na dola basi afanye biashara ya kuingiza dola. Yaani export business. Unaalika mtu kuja kuendesha mwendokasi. Anaingiza Tsh halafu wakati wa kuondosha faida anabadilisha kuwa dola!! Mbona tunakuwa tunafanya biashara kichaa.
 
Bado hata huko kwenye exportation bado tabu tupu
Ukiwa na maparachichi Yako unataka uyauze uingereza kupata export permit ni mzunguko
Ukiwa na mahindi Yako unataka uyapeleke Kenya au Ethiopia shughuli yake si mchezo
Ukiwa na ngozi za ng'ombe unataka uwapelekee Gucci au LV kupata kibali sahau
Kwa hiyo hata export inauliwa na hao hao wanaotorosha dhahabu sababu ya ukiritimba na roho mbaya, matokeo yake tunabakia hoi kama nchi
Maparachichi njia rahisi ni kuyatoa kupitia Mombasa aisee yanatoka na box za Nairobi wakati yanatoka hapo Njombe na Moshi Nchi ngumu sana hii vitu vya kuingiza fedha za kigeni kupata vibali kama sijui unatoa kitu gani wakati SA ukitaka kufanya Export yeyote kibali ni siku moja kinafanyiwa kazi na unawaambia utatoa kwa mpaka upi ili ikiwezekana upewe na agent kabisa na vitu vyote ni bure kasoro gharama ya Agent huko Mpakani nilienda na Jamaa mmoja kutoka Iringa alidhani ile huduma tuliyopewa tunalipia kumbe ni free of charge harafu jamaa wapo serious kweli..
 
Ndio hapo ,Kwa hakika sisi watanzania tuna matatizo sana
Sijui tuna laana gani ,mtu anataka ahodhi kila kitu yeye ili abaki mwenyewe kana kwamba ataweza kutosheleza mahitaji ya soko la kimataifa
Mimi naamini hizi bidhaa za kilimo zingekua msaada mkubwa kwenye kuingiza pesa za kigeni na kuwainua wakulima ,bahati mbaya wenye maamuzi hawataki iwe hivyo
 
Back
Top Bottom