Mikopo ya Bajaj na Pikipiki kwa Vijana: Fursa au Mtego wa Umasikini?

Mikopo ya Bajaj na Pikipiki kwa Vijana: Fursa au Mtego wa Umasikini?

Unaongelea Serikali kama vile ndio ina huruma..., Bora hawa ni wafanyabiashara wala hawafichi, hawapo hapa kutoa msaada bali kujipatia faida (all the best to them)

Sasa je Serikali ambayo ipo pale kutoa huduma kwa mwananchi inamkopesha tena kwa kuringa, ili mtu eti akasome (kumbuka ni mkopo sio grant)..., Tena inawapa wachache wengine hawapati na wengi wao wakimaliza wala hakuna sehemu ya ujira hivyo kuanza maisha na madeni lukuki..., Na hawa wanajifanya eti wapo pale kuwatumikia wananchi... What a bunch of Hypocrites...

Tena bila ya hawa so called wanyonyaji (wakati wanyonyaji wa kweli huwasemi) wasingekuwepo watu tungekuwa tunakabana kitaa
 
bajaji kwa siku anaweza pata zaid ya elfu 50 mpka 70..
wewe utakubali umpe mtu 12milion ikae tu miaka mwili akupe 15mil au chini ya 20m tu?
Mbona Sasa hawana maisha ya maana hao vijana hivi unajua 50k-31k kwa siku ni 19000 Sawa na 589000 approx.. 500,000 Kwann wana maisha mabovu?
 
Mbona Sasa hawana maisha ya maana hao vijana hivi unajua 50k-31k kwa siku ni 19000 Sawa na 589000 approx.. 500,000 Kwann wana maisha mabovu?
Kuwa namaisha yamaana Hilo nijambo lingine,,
Watu wanakula mshahara mzuri nahawana maisha yamaana
 
Kwa muda mrefu sasa, kumeibuka makampuni yanayodai kuwawezesha vijana kwa kutoa mikopo ya bajaj na pikipiki. Kwa mtazamo wa nje, mpango huu unaonekana kama suluhisho kwa changamoto za ajira, lakini kwa undani wake, unaelekea kuwa mtego wa umasikini kwa vijana wengi. Cha kusikitisha zaidi, serikali inaonekana kukaa kimya huku vijana wakiendelea kuumizwa na mifumo hii yenye riba kubwa kupita kiasi.

Makampuni haya yanahitaji vijana kutoa kiasi fulani cha fedha kama malipo ya awali. Kwa mfano:

Kwa Bajaj:
Unatakiwa kuweka kianzio cha takriban shilingi milioni 1 na kisha kulipa shilingi 31,000 kila siku kwa miaka miwili. Hii inamaanisha baada ya miaka miwili, kijana atakuwa amelipa jumla ya takriban shilingi milioni 23, kwa bajaj yenye thamani halisi ya takriban shilingi milioni 12.

Kwa Pikipiki:
Unatakiwa kuweka kianzio cha shilingi laki 4 hadi 5, na kisha kulipa jumla ya shilingi milioni 4.5 kwa mwaka mmoja. Hii ni kwa pikipiki mpya ambayo thamani yake sokoni ni takriban shilingi milioni 3.

Riba hizi kubwa zinawafanya vijana kufanyia kazi vyombo hivi kwa muda mrefu bila kupumzika ili kufanikisha marejesho. Mwisho wa siku, wanapomaliza kulipa mikopo hiyo, bajaj au pikipiki hizo zinakuwa zimeshachakaa kabisa, na kijana hana nafasi ya kujijenga zaidi kiuchumi.

Tatizo ni Nini?
Kimsingi, tatizo si kuwawezesha vijana. Kuwawezesha ni jambo zuri sana, lakini riba kubwa na masharti magumu yanageuza fursa hii kuwa mzigo. Makampuni yanayofanya biashara hii, ikiwemo yale ya watu binafsi na taasisi maarufu kama Mo Credit, yanajipatia faida kubwa kwa kisingizio cha "uwezeshaji wa vijana."

Cha kusikitisha zaidi, haya makampuni mara nyingi yanamilikiwa na matajiri wakubwa wanaojitambulisha kama watu wa dini na wenye maadili. Lakini mfumo wao wa kibiashara unawanyonya vijana ambao tayari wanapambana kujitafutia maisha.

Rai kwa Serikali:
Serikali inapaswa kuingilia kati na kusimamia mfumo huu wa mikopo ili kuhakikisha haki kwa vijana. Hili linaweza kufanyika kwa:

1. Kupunguza Riba: Serikali iweke mipaka ya riba inayotozwa kwenye mikopo ya bajaj na pikipiki.

2. Kuhakikisha Usawa: Masharti ya mikopo yarekebishwe ili kuwa ya haki, ambapo kijana anaweza kurejesha bila kuathiri sana maisha yake ya kila siku.

3. Kusimamia Makampuni: Serikali iangalie kwa karibu makampuni haya na kuweka sera madhubuti za kudhibiti unyonyaji.

4. Kuunda Mifumo Mbadala: Serikali au taasisi za umma ziwe na mipango ya kuwasaidia vijana moja kwa moja kwa masharti nafuu.

Tunahitaji kuweka mazingira ambayo vijana watawezeshwa kwa njia inayowajenga badala ya kuwaangusha. Ni wakati wa serikali kusimama kidete kulinda maslahi ya vijana wa Tanzania. Fursa hizi zisigeuke kuwa mtego wa umasikini!
ufukara tu , ulishawahi kuona nchi zilizoendelea kuna hayo mapikipiki na bajaji kama vitu vya usafiri wa umma? Masikini tuna safari ndefu sana ,na bado tuendelee kusifiana tu hata limtu likinya lnasifiwa.likijaba nalo linasifiwa sisi mangozi meusi zero kabisa.
 
ufukara tu , ulishawahi kuna nchi zilizoendelea kuna hayo mapikipiki na bajaji kama vitu vya usafiri wa umma? Masikini tuna safari ndefu sana ,na bado tuendelee kusifiana tu hata limtu likinya lnasifiwa.likijaba nalo linasifiwa sisi mangozi meusi zero kabisa.
jisemee mwenyewe mkuu kua nizero
 
Back
Top Bottom