Mikopo ya benki ni wizi uliokomaa, nimetozwa riba ya 81% kwa miaka 6

Sema wewe haujawahi kukunufaisha. Lakini watafutaji wananufaika namikopo kila siku, inafikia kipindi benki na wewe mnajadiliana riba ya mkopo husika ili kupata rate itayokufaa!
Endeleeni kunufaisha ma bank
 
Sema wewe haujawahi kukunufaisha. Lakini watafutaji wananufaika namikopo kila siku, inafikia kipindi benki na wewe mnajadiliana riba ya mkopo husika ili kupata rate itayokufaa!
Hii Ni kwa wafanyabisshara wakubwa....sio sisi Wa mil 3
 
Kama wewe mfanyabiashara basi ungekuwa unajua njia tofauti tofauti ambazo benki ingeweza kujipatia faida. Sio Riba.

Zipo benki zinaendeshwa bila ya riba, ukiipita post yangu utaona nimeandika kwa ufupi njia benki inavoweza kufanya biashara.

Yaani wewe umeona mwajiriwa kuwa hawezi kuwa na akili ya kibiashara? una matatizo itakuwa wewe, unajuwa watu wa ngapi wametoka kimaisha na walikuwa wameajiriwa kwanza? Au wewe mwenzangu ni wale wa kurithishwa mali akisha ukajiona mjuaji kuliko alieajiriwa na kuanzisha biashara zake? Inavoonekana wewe ungekuwa umeajiriwa, usingeweze kufikiria kujiajiri.

By the way, unaweza ukawa na network ya watu wanaokuamini na still usipate hela kutoka kwao, huwezi jua na yeye unaemuomba hela ana matatizo gani ata akupe wewe tu. ishu inayozungmzwa apa ni riba kwenye mabenki, na wewe umekuja kuponda au niseme kutetea benki wanachofanya, na uku ukijifanya humanist!

Ni kweli Humanity ni pamoja na kuwa na common sense, sijui kama mwenzangu unayo lakini?

Kufanya biashara ushirika na mtu na kumnyonya mtu kupitia mkpo ulompa, ni upi ubinaadamu hapa itakuwa?
 

Naona unashindwa kutofautisha BANK, na MTU!!!! Bank siyo mtu, ni taasisi ambayo mtaji wake ni pesa na bidhaa yake ni pesa. Benki zote za KIBIASHARA lazima zitoze riba kwenye pesa wanayokupatia ufanyie biashara zako, usilalamikie model wanayotumia kupata faida, hiyo ndiyo biashara yao...sawa na wewe unavyonunua mpunga mpaka kuugeuza kuwa kilo ya mchele kwa 1200 shambani na kwenda kuiuza kwa walaji kwa elf 2200, mlaji hawezi kukulazimisha uuze 1500 eti kwa sababu umelipia nauli mia mbili hamsini na kukoboa shwa shilingi hamsini, faida yako utatengeneza kwenye kuuza pumba! Mikopo ni biashara kubwa kwa mabenki ya kibiashara, na ni chanzo kikubwa cha kukuza mitaji kwa wafanyabiashara. Ukiona hauna uwezo wa kuzalisha vya kutosha ili urudishe mkopo na riba na ubaki na faida acha tu ndugu utaumia kichwa.
 
Inaelekea hukusoma vile vimaneno vidogo vidogo ukakimbilia kutia sahihi tu upate hiyo pesa.. haujiamini..

Natumaini utakuwa umejifunza.. labda kwingine ingekuwa nafuu
Ili nikuelewe ni mpk labda nivute bangi+kunywa balimi nimalizie na ugoro labda.
 
Sio kweli kwamba benki zote za kibiashara lazima zitoze riba. Zipo benk ambazo hazitozi riba na zinakwenda vizuri.

Wewe kujiona mjuaji mfanyabiashara unajua mambo kuliko mwajiriwa kunakuponza.

Na mifano yako ulioitoa, Hivi wewe kwenda shambani kununua mpunga mpaka ukaugeuza kuwa mchele, hukuingia garama ata uuze sawa sawa na ulivonunua? Hivi wewe nambie Benki inaingia garama ipi kuchukua pesa za Mtu A na kumkopesha Mtu B?

Umekariri vibaya mkuu.

Kuna Bank kila mwisho wa mwezi wanakata hela kwenye akaunti yako, na kuna nyingine hawakati.

Riba haina kusudio la kukuinua zaidi ya kukuongezea deni. Mkopo sio lazima uwe na riba, nimekufahamisha kwenye post yangu ya mwanzo.

Mfano wewe unataka kufanya biashara ya kuagiza magari, mimi benki umenifata umenipa plan nzima na nimeikubali.

Basi mintakwambia sikiliza, nakupa milioni 100 uagize hizo gari uanze biashara, kwanza tunaanza biashara kinachopatikana unanilipa mkopo kidogo kidogo mpaka ukimaliza kuulipa basi tutakuwa share pamoja kwenye biashara kwa mda wa miaka 2, hasara au faida tunapata sote. <<---- huu ndo mkopo wenye lengo zuri. Mkopo wa riba hauna lengo la kumnufaisha mkopaji.
 
Huu mkopo nilionao ukiisha sitakaa nikopeeee riba ni 100% sio hizo 18%[emoji57][emoji57]
 
Hapo wamekuonea huruma ingekuwa CRDB ungelipa 120% kwa rate ya 20% per year
 
Benki zipo sahihi, wateja hatupo sahihi sana kuelewa zile hesabu za P+RT/100.
Mkopo huohuo wa 20m ndani ya mwaka mmoja unalipa jumla ya 22,003,198.3.
Faida ya benki kwa mwaka ni 2,003,198.3.
Jitahidini kuelewa maana ya " annual interest rate".
Sorry mkuu hio P,R na T ni nini?
 
Nilitamani kukopa, baada ya kuona wameleta tangazo la kuwa wanakopesha kwa riba ya 18%, kwenda ofisini kwao kupigiana hesabu nikaona inakua 50% nikawaambia nitarudi...nilivyo mchungu na mchumi wa hela zangu hapana.
Ndugu, mikopo ya benki ndivyo ilivyo. Na usipokopa maendeleo utayasikia tu unless uwe na mishahara ya UN au World Bank
 
Juzi nimeenda benk moja kutaka milion 30, kwa miaka 5, nikaambiwa nitalipa jumla na deni milion 54, nikarudi nyumbani kunywa chai.
Naomba nikutonye kitu mkuu, siku moja nilienda benki nikapiga hesabu kama wakinipa milioni 50 basi nitarudisha milioni 85 kwa kipindi cha miezi 84. Lakini kama una alternative ya kupata mtaji kwa ajili ya shughuli zako basi acha mikopo. Ila kama una shida ya hela na huna sehemu ya kuzipata utaenda benki tu. Trust me on this
 
Ni kweli benki biashara yao ni pesa. Ila kwa mazingira ya riba za namna hii ndiyo maana biashara zet nyingi zinafaidisha zaidi benki.

Anyway, nilitaka kukazia point kwamba mikopo ya benki ndio main line of business kwa benki yoyote. However, ninaamini ni wakati sahihi kwa benki kuu kufanya juhudi zaidi ikishirikiana na mabenki ili riba ishuke angalau ifike asilimia 10
 
Ndugu, mikopo ya benki ndivyo ilivyo. Na usipokopa maendeleo utayasikia tu unless uwe na mishahara ya UN au World Bank[/QUOTE

Vipo Vicoba Mkuu asilimia kumi tu kwa sasa tumefikia kukopeshana hata Milioni 30 kwa miaka 3 mtu akitaka.
 
Benki Kuu haijali sana kusimamia riba zinazotozwa wakopaji wa mabenki kwani inafaidika. Hata Jana inatoa taarifa ya kushusha riba to 5% kwa benki hizo haikutoa mwongozo wa riba kwa wakopaji toka mabenki hayo. Biashara bila mikopo kunyanyuka ni vigumu lakini si kwa riba yatozayo mabenki ya Tanzania. Mkopaji daima atabaki mtumwa wa mabenki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…