Hello
Awali ya yote hili si Tangazo, sihitaji pesa ya mtu hapa. Maana kuna watu humu wanarukia rukia mambo.
Mwaka jana sokumbuki tarehe nilikopa 42k app ya M loan, marejesho 56k kwa wiki. Nilikuwa nina dharura kidogo. Mimi ni mtumishi mwenye mshahara na posho sina shida kivile sema hii ilitokea tu.
Jamaa siku ya 5 wakataka pesa yao nikakombana nao kwa kuwaambia hawako fair. Nikawajibu nitawalipa siku nikipenda Mimi hata kama Kuna penalty nitailipa lakini ile siku sikuwa tayari kuwalipa maana siku 7 bado hazijatimia. Kama kuwalipa ni option yangu sio kunilazimisha. Kweli wale wadada ni washenzi, hawana utu.
Dk chache tu simu za ndugu, marafiki, workmates n k zikaanza kumiminika na kuulizwa vipi naona matapeli sijui wametuma sms kuwa unadaiwa. Phone book yangu ina majina karibu elfu 2 nikaona hapa nizime simu nikalipa deni . Ilichukua mwezi hivi kukaa sawa.
Nikasema ngoja nitumie hii mikopo kama fursa. Benki naweza kukopa millioni hata 20 ila mda wa kukopa benki sikukusudia uwe hivi karibuni.
Nikasema hii mikopo riba yake ni kubwa na Mimi kutunza fedha ni ngumu, kwakweli nina biashara fulani hapa mjini inanipa pesa nzuri ila matumizi mengi.
Nikasema ngoja nikope. Nakopa kwenye app fulani mbili kila wiki napata million hivi nafanyia jambo , narudisha pesa kiroho safi. Nimefanya mambo mengi ya future. Nimenunua viwanja 5 Dar es salaam kwa muda mfupi. Nikawa busy na kusaka pesa kuliko wakati wowote.
Hakuna dili taliacha salama.
Nimewapa faida kubwa hizi app 2 ila zimenichochea maendeleo.
Ikafika wakati deni kubwa pesa za biashara kidogo nikaanza kukopa huku kulipa kule huku nami nikiongeza pesa yangu. Ikawa mshahara ni kama tone la maji tu kwenye ndio, posho ikawa tone tu. Mshahara wa machi na April sikupata madeni ya online yakataka kunitoa roho. Jamaa wanakera.
Nikaomba mkopo benki nimalizane na Hawa jamaa hatua ya mwisho mkopo ukabuma, kulikuwa na tatizo kiufundi si mnajua mambo ya benki hata kikosa kiwe kidogo vipi pesa hupati. Nilipagawa aisee.
Deni likafika kama millioni 5 kasoro. Kila siku simu kama zote . Nikaanza kusoma YouTube jinsi ya kupambana na hawa online 🦈 sharks.
Nikawadhibiti. Nilifanya utafiti wa kutosha huku nikijua na wao wanajitahidi kupambana kwa njia mpya shilingi yao hata moja isipotee.
Mwisho wa siku nikawadhibiti.
Naishi kwa amani sasa. Aisee niliiona Dunia chungu. Hii mikopo isipodhibitiwa mapema watu watakuwa matahira, wengine watajinyonga.