Mikopo ya mitandaoni ilitaka iniue

Mikopo ya mitandaoni ilitaka iniue

Hello

Awali ya yote hili si Tangazo, sihitaji pesa ya mtu hapa. Maana kuna watu humu wanarukia rukia mambo.

Mwaka jana sokumbuki tarehe nilikopa 42k app ya M loan, marejesho 56k kwa wiki. Nilikuwa nina dharura kidogo. Mimi ni mtumishi mwenye mshahara na posho sina shida kivile sema hii ilitokea tu.

Jamaa siku ya 5 wakataka pesa yao nikakombana nao kwa kuwaambia hawako fair. Nikawajibu nitawalipa siku nikipenda Mimi hata kama Kuna penalty nitailipa lakini ile siku sikuwa tayari kuwalipa maana siku 7 bado hazijatimia. Kama kuwalipa ni option yangu sio kunilazimisha. Kweli wale wadada ni washenzi, hawana utu.

Dk chache tu simu za ndugu, marafiki, workmates n k zikaanza kumiminika na kuulizwa vipi naona matapeli sijui wametuma sms kuwa unadaiwa. Phone book yangu ina majina karibu elfu 2 nikaona hapa nizime simu nikalipa deni . Ilichukua mwezi hivi kukaa sawa.

Nikasema ngoja nitumie hii mikopo kama fursa. Benki naweza kukopa millioni hata 20 ila mda wa kukopa benki sikukusudia uwe hivi karibuni.
Nikasema hii mikopo riba yake ni kubwa na Mimi kutunza fedha ni ngumu, kwakweli nina biashara fulani hapa mjini inanipa pesa nzuri ila matumizi mengi.

Nikasema ngoja nikope. Nakopa kwenye app fulani mbili kila wiki napata million hivi nafanyia jambo , narudisha pesa kiroho safi. Nimefanya mambo mengi ya future. Nimenunua viwanja 5 Dar es salaam kwa muda mfupi. Nikawa busy na kusaka pesa kuliko wakati wowote.

Hakuna dili taliacha salama.
Nimewapa faida kubwa hizi app 2 ila zimenichochea maendeleo.
Ikafika wakati deni kubwa pesa za biashara kidogo nikaanza kukopa huku kulipa kule huku nami nikiongeza pesa yangu. Ikawa mshahara ni kama tone la maji tu kwenye ndio, posho ikawa tone tu. Mshahara wa machi na April sikupata madeni ya online yakataka kunitoa roho. Jamaa wanakera.

Nikaomba mkopo benki nimalizane na Hawa jamaa hatua ya mwisho mkopo ukabuma, kulikuwa na tatizo kiufundi si mnajua mambo ya benki hata kikosa kiwe kidogo vipi pesa hupati. Nilipagawa aisee.

Deni likafika kama millioni 5 kasoro. Kila siku simu kama zote . Nikaanza kusoma YouTube jinsi ya kupambana na hawa online 🦈 sharks.

Nikawadhibiti. Nilifanya utafiti wa kutosha huku nikijua na wao wanajitahidi kupambana kwa njia mpya shilingi yao hata moja isipotee.

Mwisho wa siku nikawadhibiti.
Naishi kwa amani sasa. Aisee niliiona Dunia chungu. Hii mikopo isipodhibitiwa mapema watu watakuwa matahira, wengine watajinyonga.
Muongo. Huwezi kuja tapeli mtu unajichanganya tu kwenye maelezo sababu u kilaza. Na huelewi hata namna ya kutapeli. Huna lolote kibaka kilaza. Shule hamjafungua? Hata kuandika ku make sense hujui.
 
Mtu kama wewe una pepo la umaskini ukitajirika niite mbwa
.kutajirika kuna kanuni zake mojawapo ni kukopa na kulipa bila longolongo au 8janja ujanja
Hivi unaweza kutajirika Kwa 20K?
Kweli wewe mmbwa ulie katwa mkia,nani amekuambia nahitaji utajiri?
Tukileta thread za kufanywa fulsa (kupigwa) mnatuona mandezi ila kinyume chake mnaanza kuleta pigo za kutia huruma
Kuna mikopo ya kukopa mfano Bank lkn hivi vya mtandaoni mtakoma wenyewe
 
Hivi hawa wanao kopesha watu mitandaoni wako sawa kiakili? Unampa mtu hela hujui atarudisha vip?

Ukibadilisha laini?
Ndo maana riba ni kubwa kwa sababu ni ina risk kubwa.

Hii ni mikopo ya dharura na inabidi itumike hivyo kama dharura. Inatakiwa ilipwe kwa mida mfupi kama siku 7 au 14. Na inabidi iwe ni kwa kiasi kidogo kama buku 10 hadi laki.

Mimi nawashauri watu wakope mtandaoni pale tu wanapokuwa na dharura na wana uhakika wa kurejesha. Kwa mfano ni tarehe 18, mshahara unatoka tarehe 23 au 24 unahitaji 50,000 ya nauli kwa siku zilizobakia, au unaumwa unahitaji dawa ambazo haziko kwenye bima na una uhakika utapata mshahara utarejesha.

Usikope mtandaoni kufanya biashara. Mikopo ya biashara ipo na ina riba ndogo na ya muda mrefu. Tusichanganye mambo.

Mimi kwa mfano hizi songesha zinanisaidia sana wala sina malalamiko. Nakopa nalipa, nakopa nalipa, maisha yanasonga.
 
Ndo maana riba ni kubwa kwa sababu ni ina risk kubwa.

Hii ni mikopo ya dharura na inabidi itumike hivyo kama dharura. Inatakiwa ilipwe kwa mida mfupi kama siku 7 au 14. Na inabidi iwe ni kwa kiasi kidogo kama buku 10 hadi laki.

Mimi nawashauri watu wakope mtandaoni pale tu wanapokuwa na dharura na wana uhakika wa kurejesha. Kwa mfano ni tarehe 18, mshahara unatoka tarehe 23 au 24 unahitaji 50,000 ya nauli kwa siku zilizobakia, au unaumwa unahitaji dawa ambazo haziko kwenye bima na una uhakika utapata mshahara utarejesha.

Usikope mtandaoni kufanya biashara. Mikopo ya biashara ipo na ina riba ndogo na ya muda mrefu. Tusichanganye mambo.

Mimi kwa mfano hizi songesha zinanisaidia sana wala sina malalamiko. Nakopa nalipa, nakopa nalipa, maisha yanasonga.
Usipo walipa wanakufanyaje? Si hawajui kwako unawablock?
 
Hamieni Tigo
 

Attachments

  • Screenshot_20240802-094813.png
    Screenshot_20240802-094813.png
    148.6 KB · Views: 10
Baadhi ya watanzania ndio hata taasisi za fedha ngumu kuwaamini kuwakopesha
Mhindi akiingia benki kukopa mdani ya nudu saa hata akikopa mabilioni anapewa sababu ni walipaji wazuri

Mswahili ujanja mwingi Kukopa akope yeye kukopa harusi kulipa matanga

Huwezi kopa bila kusoma masharti na kukubaliana na masharti iwe mikopo ya mitandaoni au nje ya kusajikiwa au mtaani

Sasa mtu masharti anakubali ukimkopesha kulipa anaanza kupiga chenga

Ndio maana hata mitaani kuna mtu aweza zunguka mtaa mzima au akapigia ndigu wote au kazini wamkopeshe elfu 10 tu hapati

Hii tabia ya kukopa na kuwa mkorofi kwenye kulipa sio nzuri

Mleta mada na wenye mawazo kama yako hamko sahihi.
Wewe utakuwa mojawapo mtumishi wa hizi kampuni za kitapeli za online
 
We wakope tu songesha utawalipa hata 2030 ukipata pesa ya usimamiz wa uchaguzi mkuu hawanaga shida hawa wanangu nawapenda sana Riba unajipangia uwalipe ikifika ngapi🤣
 
Back
Top Bottom