Mikopo ya online: Rais Samia wachunguze Mkurugenzi Mkuu TCRA, Gavan BOT na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Mikopo ya online: Rais Samia wachunguze Mkurugenzi Mkuu TCRA, Gavan BOT na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Rais Samia, kwanza nashukuru umemuondoa Nape Nnauye kwasababu TCRA na Tume ya Ulinzi wa Taaifa Binfsi(PDPC), ni taasisi zilikuwa chini yake na mpaka anaondoka, hatuijaona hizi taasisi zikiwa serious katika kuchukua hatua(sijaona wala kusika waliokamatwa kwa kudhalilisha watanzania).

Naomba ikikupendeza, muondoe na Mwigulu anaeisimamia BOT ambayo nayo inapaswa kuhusika katika kusimamia na kudhibiti biashara ya kukopesha.

Mhe. Raisi, haya makampuni hayafanyi biashara hii kwa kificho kwani wanajitangaza mitandaoni mfano facebook na zaidi na ambacho ni cha kushangaza, makampuni haya ya kukopesha mitandaoni yanatoa mikopo na kupokea marejesho yao kupitia mitandao ya simu ya humu nchini halafu eti wahusika wanashindwa kukamatwa!

Ukiacha udhaliolishaji wa kusambaza taarifa za wakopaji, riba wanazotoa ni kubwa mno na sijui kama zinaendana na riba elekezi ya BOT ya asilimi 3.5 kwa mwezi na sijui kama wana leseni. Pia muda wa kulipa denii sio rafiki kabisa na zaidi wana lugha mbaya sana. Hayo ni machache tu.

Mhe, Raisi,malalamiko yamekuwa mengi na hata Spika wa BUnge, Mhe. Tulia Ackson, alililamika Bungeni kutumiwa sms za mtu anaedaiwa wakati yeye hahusiki kwa namna yoyote ile. Mbali na Spika, hata wabunge kadhaa nao wamelakamikia hii mikopo ya kausha damu kwa muda sasa lakini sijawahi ona au siki kuna watu wamekamatwa kwa tuhuma za kufanya hii biashara kinyume na sheria badala yake hizi taasisi kila siku zinaongelea habari ya kutoa elimu kwa umma.

Mhe. Raisi, kweli inaangia akilini kwa hizi taasisi kushindwa kuthinbiti hizi App za kukopesha mitandaoni?Binafsi malalamiko hapa JamiiForums nimeanza kuyasoma hivi karibuni lakini yapo tangu mwaka jana ila mpaka leo sijui kama kweli kuna walio wahi kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za kudhalilisha watu na kufanya biashara hii bila kuwa na leseni na makosa mengine.

Najiuliza, hivi viongozi wa hizi taasisi hawawezi kuweka mitego kuwakamata hawa watu? Mbona kama sheria inawaruhusu?

Viongozi wa hizi taasisi hawajawahi kupokea malalamiko rasimi kutoka kwa wananchi?

Tufanye assumption kuwa hakuna malalimiko yalioyowasilishwa kwa kwa njia rasimi. Je, ndio watakaa ofisini kusuburi malalamiko rasimi ndio wachukue hatua?

Kama hawapokei au kusikia malalamiko, press release wanazotoa mara kwa mara katika website yao za kuonya kuhusu hii biashara, udhalilishaji, n.k, msingi wake huwa ni nini kama sio malalamiko ya wananchi?

Na je, TCRA wameshindwa kuagiza makampuni ya simu kusitisha mara moja mitandao yao kutumika kibisahara na taasisi zinazokiuka sheria?

Mhe. Raisi, maswali ni mengi, lakini yote yanaonyesha udhaifu wa hizi taasisi. Hivyo, nakushauri ufanye uchunguzi na ukibaini kuna uzembe, basi viongozi wakuu wa hiizi taasisi wawajibike.

Kilichonisukuma leo kuleta hii mada ni hili bandiko la Mdau mmoja(Mwanasheria) hapa JamiForums ambalo nakuomba na wewe Mhe. Raisi ulisome. Yako mabandiko mengi tu kwani watu hawajaanza kulalamika leo wa jana.

[/URL]

Hebu tusome majukumu ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kama nilivyoyasoma katika bandiko moja hapa JF.

1721937853985.png
 
Yawezekana wana Leseni,lakini pia kwanini tujiingize kukopa fedha za watu...?
Mikopo mitandaoni uwa nafananisha na wenye kulalamikia namna wanavyolizwa na Makanisa ya kileo...🤣🤣😜😜😜
 
Wasitumie umasini na shida wa watu kama njia ya kuwanyonya na kuwadhalilisha.
Ni bora kubaki maskini kuliko kujifanya Tajiri kwa kukopa fedha za watu,unapozichukua unakubali masharti.
Kuna wakati Serikali inabidi ijiepushe na wananchi wanafanya vitu visivyo sawa,kwa kutegemea mbeleko ya kusaidiwa.
 
Sasa kuna haja gani ya Bunge kukaa na kutunga sheria na kisha Raisi kusaini ili iwe sheria kamili kudhibiti haya mambo?

Kama ni hivyo, tuache na wauza madawa ya kulevya nao wafanye bisashara yao kwa uhuru.
 
Bahati mbaya ni kampuni za Wachina. Karibia zote, sidhani kama kuna Mbongo mwenye udhubutu huo.

Kuna moja ya Maisha Finance yake Deus Manyenye. Nayo niliona.

Tukiachana na uhalisia wa riba mlima, unapewa 200k urudishe 300k ndani ya wiki moja. Ila je, taarifa za wananchi wake zipo salama kiasi gani zikiwekwa chini ya watu wa mataifa mengine?

ephen_ alikopa. Maskini ya Mungu ni jobless. Akashindwa kurejesha. Kila siku natumiwa sms za kumsihi arejeshe hela ya watu.

Naombeni kwa pamoja TUMSIHI arejeshe hela ya watu jamani.
 
Kwani unalazimishwa kukopa...vigezo vyao na masharti kabla ya kukopa wanasoma au ndio tamaa ya fedha? Hapa watz ndio mbumbumbu...wacha wazalilishwe kwanza walikubali wenyewe kuzalilishwa...unakopaje mtandaoni...
 
Awatumbue Haraka Haraka Ni Majipu Hayo Yameshaiva Asiogope Usaha Kuruka
 
Bahati mbaya ni kampuni za Wachina. Karibia zote, sidhani kama kuna Mbongo mwenye udhubutu huo.

Kuna moja ya Maisha Finance yake Deus Manyenye. Nayo niliona.

Tukiachana na uhalisia wa riba mlima, unapewa 200k urudishe 300k ndani ya wiki moja. Ila je, taarifa za wananchi wake zipo salama kiasi gani zikiwekwa chini ya watu wa mataifa mengine?

ephen_ alikopa. Maskini ya Mungu ni jobless. Akashindwa kurejesha. Kila siku natumiwa sms za kumsihi arejeshe hela ya watu.

Naombeni kwa pamoja TUMSIHI arejeshe hela ya watu jamani.
Hivi Mtanzania unaweza kwenda China na ukafanya huu uhuni kwa wachin na serikali ikawa inakuangalia tu?
 
Sasa kuna haja gani ya Bunge kukaa na kutunga sheria na kisha Raisi kusaini ili iwe sheria kamili kudhibiti haya mambo?

Kama ni hivyo, tuache na wauza madawa ya kulevya nao wafanye bisashara yao kwa uhuru.
Kuthibiti ni sawa,lakini na sisi kama jamii sio kila tutegemea usaidizi wa Serikali,masuala mengine ni kuwa na tahadhali nayo.
Ni sawa sawa na Vijana wanaojiingiza katika Betting au kamali za Bonanza.
Suala la ajira pengine ndio sababu ya vijana wengine kuamua kujiajili kupitia hicho ulichosema.
Vipi kuhusu uwepo wa madalali kwenye biashara kubwa....?
 
Kwani unalazimishwa kukopa...vigezo vyao na masharti kabla ya kukopa wanasoma au ndio tamaa ya fedha? Hapa watz ndio mbumbumbu...wacha wazalilishwe kwanza walikubali wenyewe kuzalilishwa...unakopaje mtandaoni...
Wewe utaona uko sawa nyumba yako kuhifadhi bangi halafu mtoto wa jirani akaingia akachukua bangi akavuta..utasema kwa nini ameingia nyumbani mwako bila wewe kuwepo?
Swali, hawa wakopeshaji wana leseni kukopesha? Mbona riba zao ni kinyume na sheria..mtu kukopa ni matokeo ya mlaghai kuruhusiwa kuibia watu kwa ulaghai!
 
Kuthibiti ni sawa,lakini na sisi kama jamii sio kila tutegemea usaidizi wa Serikali,masuala mengine ni kuwa na tahadhali nayo.
Ni sawa sawa na Vijana wanaojiingiza katika Betting au kamali za Bonanza.
Suala la ajira pengine ndio sababu ya vijana wengine kuamua kujiajili kupitia hicho ulichosema.
Vipi kuhusu uwepo wa madalali kwenye biashara kubwa....?
Sio usaidizi, ni WAJIBU wa serikali kulinda raia wake dhidi ya uhalifu wa aina yoyote, popote..! Kufanya biashara ya Kukopesha bila leseni, riba kinyume na sheria na uvamizi wa taarifa za watu ni UHALIFU!
 
Na sisi WAJIBU wetu ni kujiepusha na vitendo vilivyo viovu eti kwa sababu ipo Serikali ya kutusaidia wakati na sisi tuna wajibu wa kujilinda dhidi ya Uhalifu.
Otherwise labda kama kuna syndicate mahala...🤣🤣😇😇
 
Back
Top Bottom