Rais Samia, kwanza nashukuru umemuondoa Nape Nnauye kwasababu TCRA na Tume ya Ulinzi wa Taaifa Binfsi(PDPC), ni taasisi zilikuwa chini yake na mpaka anaondoka, hatuijaona hizi taasisi zikiwa serious katika kuchukua hatua(sijaona wala kusika waliokamatwa kwa kudhalilisha watanzania).
Naomba ikikupendeza, muondoe na Mwigulu anaeisimamia BOT ambayo nayo inapaswa kuhusika katika kusimamia na kudhibiti biashara ya kukopesha.
Mhe. Raisi, haya makampuni hayafanyi biashara hii kwa kificho kwani wanajitangaza mitandaoni mfano facebook na zaidi na ambacho ni cha kushangaza, makampuni haya ya kukopesha mitandaoni yanatoa mikopo na kupokea marejesho yao kupitia mitandao ya simu ya humu nchini halafu eti wahusika wanashindwa kukamatwa!
Ukiacha udhaliolishaji wa kusambaza taarifa za wakopaji, riba wanazotoa ni kubwa mno na sijui kama zinaendana na riba elekezi ya BOT ya asilimi 3.5 kwa mwezi na sijui kama wana leseni. Pia muda wa kulipa denii sio rafiki kabisa na zaidi wana lugha mbaya sana. Hayo ni machache tu.
Mhe, Raisi,malalamiko yamekuwa mengi na hata Spika wa BUnge, Mhe. Tulia Ackson, alililamika Bungeni kutumiwa sms za mtu anaedaiwa wakati yeye hahusiki kwa namna yoyote ile.
Mhe. Raisi, kweli inaangia akilini kwa hizi taasisi kushindwa kuthinbiti hizi App za kukopesha mitandaoni?Binafsi malalamiko hapa JamiiForums nimeanza kuyasoma hivi karibuni lakini yapo tangu mwaka jana ila mpaka leo sijui kama kweli kuna walio wahi kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za kudhalilisha watu na kufanya biashara hii bila kuwa na leseni na makosa mengine.
Najiuliza, hivi viongozi wa hizi taasisi hawawezi kuweka mitego kuwakamata hawa watu?
Viongozi wa hizi taasisi hawajawahi kupokea malalamiko rasimi kutoka kwa wananchi?
Tufanye assumption kuwa hakuna malalimiko yalioyowasilishwa kwa kwa njia rasimi. Je, ndio watakaa ofisini kusuburi malalamiko rasimi ndio wachukue hatua?
Kama hawapokei au kusikia malalamiko, press realese wanazotoa mara kwa mara katika website yao za kuonya kuhusu hii biashara, udhalilishaji, n.k, msingi wake huwa ni nini kama sio malalamiko ya wananchi?
Na je, TCRA wameshindwa kuagiza makampuni ya simu kusitisha mara moja mitandao yao kutumika kibisahara na taasisi zinazokiuka sheria?
Mhe. Raisi, maswali ni mengi, lakini yote yanaonyesha udhaifu wa hizi taasisi. Hivyo, nakushauri ufanye uchunguzi na ukibaini kuna uzembe, basi viongozi wakuu wa hiizi taasisi wawajibike.
Kilichonisukuma leo kuleta hii mada ni hili bandiko la Mdau mmoja wa hapa JamiForums ambalo nakuomba na wewe Mhe. Raisi ulisome. Yako mabandiko mengi tu kwani watu hawajaanza kulalamika leo wa jana.
Bashir Yakub, WAKILI. +255 714 047 241. Swali la msingi ni kuwa hawa wanaokopesha wanapata wapi namba za ndugu zako, jamaa, na marafiki ambazo wanazitumia ujumbe kuwataarifu kuwa unadaiwa, umeshindwa kulipa mkopo,na maneno mengine yasiyo na staha. Fikiria mkopeshaji ambaye si tu hajawahi hata...
Ni hivi salary slip..uzito wa serikali kudhibiti uhalifu kwenye mitandao ni km wa kukusudia, inaonekana serikali na makampuni ya simu wananufaishana kwa namna moja ama nyingine, ndio maana unaweza kuona kampuni yenye wateja zaidi ya million 16 haijawahi kuwa mlipa kodi bora toka waanze biashara! wakati hapo jirani Kenya kampuni hiyo hiyo ya simu mara kadhaa imekuwa ndiye mlipa kodi namba moja mfululizo ikiwa na wateja million 7 tu.. kwa nini kampuni hiyo hiyo iwe ya kwanza Kenya halafu hapa Tanzania hata kwenye watatu bora haimo wakati ina wateja mara mbili zaidi ya wale wa Kenya..! Case hii inatoa signal kwamba serikali imeachia wahalifu waibie watu sababu wao serikali wanajua wanachopata gizani kutoka kwa wahalifu hawa..!
Na sisi WAJIBU wetu ni kujiepusha na vitendo vilivyo biovu eti kwa sababu ipo Serikali ya kutusaidia wakati na sisi tuna wajibu wa kujilinda dhidi ya Uhalifu.
Otherwise labda kama kuna syndicate mahala...
Jiulize kuna ugumu gani kwa serikali kuagiza makampuni ya simu kutotumika na haya makampuni?
Transaction zao zote za kotoa mikopo na kupokea marejesho ni kwa kupitiia mitandao ya simu ya humu nchini ambayo inadhibitiwa na TCRA. Sasa nini kinawashinda TCRA kutoa agizo la kukataza makampuni ya simu kufanya biashara na haya makampuni ya kitapeli?
Ni hivi salary slip..uzito wa serikali kudhibiti uhalifu kwenye mitandao ni km wa kukusudia, inaonekana serikali na makampuni ya simu wananufaishana kwa namna moja ama nyingine, ndio maana unaweza kuona kampuni yenye wateja zaidi ya million 16 haijawahi kuwa mlipa kodi bora toka waanze biashara! wakati hapo jirani Kenya kampuni hiyo hiyo ya simu mara kadhaa imekuwa ndiye mlipa kodi namba moja mfululizo ikiwa na wateja million 7 tu.. kwa nini kampuni hiyo hiyo iwe ya kwanza Kenya halafu hapa Tanzania hata kwenye watatu bora haimo wakati ina wateja mara mbili zaidi ya wale wa Kenya..! Case hii inatoa signal kwamba serikali imeachia wahalifu waibie watu sababu wao serikali wanajua wanachopata gizani kutoka kwa wahalifu hawa..!
Uko sahihi kabisa. Nadhani serikali inapata tozo kwenye hizi transactions na makampuni ya simu nayo yanafanya biashara ndio maana hakuna hatua za maana zinazochukuliwa zaidi ya unafiki na hadaa za kutoa press release za kutimiza tu wajibu.
NI kwa vile tu haiwezekani kupata nafasi yoyote huko serikalini ila ingepatikana ningefanya ufisadi ambao haujawahi kutokea, kama ni wizara nakomba bajeti yote nikafie nje ya nchi yaani mgenisoma kwenye mtaala wa Historia na Uraia😁
Achani kulaumu serikali kwa vitu ambavyo kila mtu ana control navyo. Umedownload app mwenyewe bila kulazimishwa, umesoma vigezo na masharti na umeamua kukopa, si ulipe hela za watu?
Achani kulaumu serikali kwa vitu ambavyo kila mtu ana control navyo. Umedownload app mwenyewe bila kulazimishwa, umesoma vigezo na masharti na umeamua kukopa, si ulipe hela za watu?
Ni bora kubaki maskini kuliko kujifanya Tajiri kwa kukopa fedha za watu,unapozichukua unakubali masharti.
Kuna wakati Serikali inabidi ijiepushe na wananchi wanafanya vitu visivyo sawa,kwa kutegemea mbeleko ya kusaidiwa.
Hapa ishu si kukopa. Hakuna aibu kwenye kukopa. Ishu ya mleta mada ni, taasisi zinazokopesha zimesajiliwa na kufata taratibu za nchi? Au kuna watu wapo juu ya hizi sheria tunazozipitisha bungeni?
Na sisi WAJIBU wetu ni kujiepusha na vitendo vilivyo viovu eti kwa sababu ipo Serikali ya kutusaidia wakati na sisi tuna wajibu wa kujilinda dhidi ya Uhalifu.
Otherwise labda kama kuna syndicate mahala...🤣🤣😇😇
Nitajiepushaje wakati mhalifu ana ujasiri wa kuniibia mchana kweupe..ni sawa na mtu amevaa sare za askari wakati si askari akakukwida na kuanza kukusachi, utakuwa na ujasiri wa kusema mwizi..hata ukisema una hakika utapata msaada? Kampuni inatangaza mikopo mtandaoni, mimi nitajuajuje wana leseni au hawana? Kama hawana leseni anayepaswa kujua uhalali wao ni mimi au mtoa leseni..kabla ya wao kunifikia mimi kunilaghai mtoa leseni alipaswa akabiliane nao kwanza na si kuachia mimi nijiepushe nao..
Achani kulaumu serikali kwa vitu ambavyo kila mtu ana control navyo. Umedownload app mwenyewe bila kulazimishwa, umesoma vigezo na masharti na umeamua kukopa, si ulipe hela za watu?
Upo sahihi kabisa. Ukikopa lipa. Ishu hapa ni hizi sheria za BOT za riba hazifanyi kazi kwa raia wote? Yaani kuna watu wanaweza chaji riba wanavyotaka wazi wazi na hakuna wa kuwahoji si ndio? Serikali imeufyata watu wanapita juu ya taratibu na miongozo ya BOT.
cha kutibiwa serikalini kuepuka huduma mbovu, acha kusomesha watito serikalini kuepuka elimu mbovu, acha kutumia umeme wa Tanesco kuepuka mgao, acha kupanda mwendokasi kuepuka kubanana. Ndo akili zetu hizi. Kama ni hivyo sheria na kiongozi ni kwaajili ya nani?
Nitajiepushaje wakati mhalifu ana ujasiri wa kuniibia mchana kweupe..ni sawa na mtu amevaa sare za askari wakati si askari akakukwida na kuanza kukusachi, utakuwa na ujasiri wa kusema mwizi..hata ukisema una hakika utapata msaada? Kampuni inatangaza mikopo mtandaoni, mimi nitajuajuje wana leseni au hawana? Kama hawana leseni anayepaswa kujua uhalali wao ni mimi au mtoa leseni..kabla ya wao kunifikia mimi kunilaghai mtoa leseni alipaswa akabiliane nao kwanza na si kuachia mimi nijiepushe nao..
Mkuu kuna ujumbe unatolewa na BoT kila siku kuhusu watu kukopa sehemu zilizosajiliwa sasa kwanini tunajiingiza kukopa sehemu zisizo rasmi.....
SEMA tu labda kuna namna ya kuangalia kama hizo microfinance zina credibility ya kutoa huduma.
Hapa ishu si kukopa. Hakuna aibu kwenye kukopa. Ishu ya mleta mada ni, taasisi zinazokopesha zimesajiliwa na kufata taratibu za nchi? Au kuna watu wapo juu ya hizi sheria tunazozipitisha bungeni?
Nimeelewa vyema, SEMA tu nilihitaji kuwithdraw ili tu kwa kina tatizo hili,yawezekana kuna mianya either ya uzembe au kutokujali kwenye kunafaisha kikundi cha watu.
Nakumbuka kina hoja ya kuhoji kwa nini Waziri anakuwa na Makampuni ya simu, pengine sio ila ipo alternative ya kuvuna noti kinyume na Sheria za Nchi.
cha kutibiwa serikalini kuepuka huduma mbovu, acha kusomesha watito serikalini kuepuka elimu mbovu, acha kutumia umeme wa Tanesco kuepuka mgao, acha kupanda mwendokasi kuepuka kubanana. Ndo akili zetu hizi. Kama ni hivyo sheria na kiongozi ni kwaajili ya nani?
Yawezekana wana Leseni,lakini pia kwanini tujiingize kukopa fedha za watu...?
Mikopo mitandaoni uwa nafananisha na wenye kulalamikia namna wanavyolizwa na Makanisa ya kileo...🤣🤣😜😜😜
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.