Mikopo ya online: Rais Samia wachunguze Mkurugenzi Mkuu TCRA, Gavan BOT na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Ni hivi salary slip..uzito wa serikali kudhibiti uhalifu kwenye mitandao ni km wa kukusudia, inaonekana serikali na makampuni ya simu wananufaishana kwa namna moja ama nyingine, ndio maana unaweza kuona kampuni yenye wateja zaidi ya million 16 haijawahi kuwa mlipa kodi bora toka waanze biashara! wakati hapo jirani Kenya kampuni hiyo hiyo ya simu mara kadhaa imekuwa ndiye mlipa kodi namba moja mfululizo ikiwa na wateja million 7 tu.. kwa nini kampuni hiyo hiyo iwe ya kwanza Kenya halafu hapa Tanzania hata kwenye watatu bora haimo wakati ina wateja mara mbili zaidi ya wale wa Kenya..! Case hii inatoa signal kwamba serikali imeachia wahalifu waibie watu sababu wao serikali wanajua wanachopata gizani kutoka kwa wahalifu hawa..!
 
Na sisi WAJIBU wetu ni kujiepusha na vitendo vilivyo biovu eti kwa sababu ipo Serikali ya kutusaidia wakati na sisi tuna wajibu wa kujilinda dhidi ya Uhalifu.
Otherwise labda kama kuna syndicate mahala...
Jiulize kuna ugumu gani kwa serikali kuagiza makampuni ya simu kutotumika na haya makampuni?

Transaction zao zote za kotoa mikopo na kupokea marejesho ni kwa kupitiia mitandao ya simu ya humu nchini ambayo inadhibitiwa na TCRA. Sasa nini kinawashinda TCRA kutoa agizo la kukataza makampuni ya simu kufanya biashara na haya makampuni ya kitapeli?
 
Uko sahihi kabisa. Nadhani serikali inapata tozo kwenye hizi transactions na makampuni ya simu nayo yanafanya biashara ndio maana hakuna hatua za maana zinazochukuliwa zaidi ya unafiki na hadaa za kutoa press release za kutimiza tu wajibu.
 
NI kwa vile tu haiwezekani kupata nafasi yoyote huko serikalini ila ingepatikana ningefanya ufisadi ambao haujawahi kutokea, kama ni wizara nakomba bajeti yote nikafie nje ya nchi yaani mgenisoma kwenye mtaala wa Historia na Uraia😁
 
Achani kulaumu serikali kwa vitu ambavyo kila mtu ana control navyo. Umedownload app mwenyewe bila kulazimishwa, umesoma vigezo na masharti na umeamua kukopa, si ulipe hela za watu?

Kwani uliambiwa hizo hela zinagawiwa bure?
 
Achani kulaumu serikali kwa vitu ambavyo kila mtu ana control navyo. Umedownload app mwenyewe bila kulazimishwa, umesoma vigezo na masharti na umeamua kukopa, si ulipe hela za watu?

Kwani uliambiwa hizo hela zinagawiwa bure?
Kwani kuna mtu analazimishwa kuvuta bangi au kutumia madawa ya kulevya? Kwanini serikali inaingilia kati?Serikali haina wajibu wa kulinda raia wake?
 
Ni bora kubaki maskini kuliko kujifanya Tajiri kwa kukopa fedha za watu,unapozichukua unakubali masharti.
Kuna wakati Serikali inabidi ijiepushe na wananchi wanafanya vitu visivyo sawa,kwa kutegemea mbeleko ya kusaidiwa.
Hapa ishu si kukopa. Hakuna aibu kwenye kukopa. Ishu ya mleta mada ni, taasisi zinazokopesha zimesajiliwa na kufata taratibu za nchi? Au kuna watu wapo juu ya hizi sheria tunazozipitisha bungeni?
 
Na sisi WAJIBU wetu ni kujiepusha na vitendo vilivyo viovu eti kwa sababu ipo Serikali ya kutusaidia wakati na sisi tuna wajibu wa kujilinda dhidi ya Uhalifu.
Otherwise labda kama kuna syndicate mahala...πŸ€£πŸ€£πŸ˜‡πŸ˜‡
Nitajiepushaje wakati mhalifu ana ujasiri wa kuniibia mchana kweupe..ni sawa na mtu amevaa sare za askari wakati si askari akakukwida na kuanza kukusachi, utakuwa na ujasiri wa kusema mwizi..hata ukisema una hakika utapata msaada? Kampuni inatangaza mikopo mtandaoni, mimi nitajuajuje wana leseni au hawana? Kama hawana leseni anayepaswa kujua uhalali wao ni mimi au mtoa leseni..kabla ya wao kunifikia mimi kunilaghai mtoa leseni alipaswa akabiliane nao kwanza na si kuachia mimi nijiepushe nao..
 
Achani kulaumu serikali kwa vitu ambavyo kila mtu ana control navyo. Umedownload app mwenyewe bila kulazimishwa, umesoma vigezo na masharti na umeamua kukopa, si ulipe hela za watu?

Kwani uliambiwa hizo hela zinagawiwa bure?
Upo sahihi kabisa. Ukikopa lipa. Ishu hapa ni hizi sheria za BOT za riba hazifanyi kazi kwa raia wote? Yaani kuna watu wanaweza chaji riba wanavyotaka wazi wazi na hakuna wa kuwahoji si ndio? Serikali imeufyata watu wanapita juu ya taratibu na miongozo ya BOT.
 
Acha kukopa kuepuka kudhalilishwa. Mambo mengine yapo tu ndani ya uwezo wetu ila tunajitoa ufahamu.
 
A
Acha kukopa kuepuka kudhalilishwa. Mambo mengine yapo tu ndani ya uwezo wetu ila tunajitoa ufahamu.
cha kutibiwa serikalini kuepuka huduma mbovu, acha kusomesha watito serikalini kuepuka elimu mbovu, acha kutumia umeme wa Tanesco kuepuka mgao, acha kupanda mwendokasi kuepuka kubanana. Ndo akili zetu hizi. Kama ni hivyo sheria na kiongozi ni kwaajili ya nani?
 
Mkuu kuna ujumbe unatolewa na BoT kila siku kuhusu watu kukopa sehemu zilizosajiliwa sasa kwanini tunajiingiza kukopa sehemu zisizo rasmi.....
SEMA tu labda kuna namna ya kuangalia kama hizo microfinance zina credibility ya kutoa huduma.
 
Hapa ishu si kukopa. Hakuna aibu kwenye kukopa. Ishu ya mleta mada ni, taasisi zinazokopesha zimesajiliwa na kufata taratibu za nchi? Au kuna watu wapo juu ya hizi sheria tunazozipitisha bungeni?
Nimeelewa vyema, SEMA tu nilihitaji kuwithdraw ili tu kwa kina tatizo hili,yawezekana kuna mianya either ya uzembe au kutokujali kwenye kunafaisha kikundi cha watu.
Nakumbuka kina hoja ya kuhoji kwa nini Waziri anakuwa na Makampuni ya simu, pengine sio ila ipo alternative ya kuvuna noti kinyume na Sheria za Nchi.
 
Reactions: Tsh
Wewe kopa ukitarajia kiongozi aje kukusaidia wakati wa kudaiwa. Utangoja sana
 
Yawezekana wana Leseni,lakini pia kwanini tujiingize kukopa fedha za watu...?
Mikopo mitandaoni uwa nafananisha na wenye kulalamikia namna wanavyolizwa na Makanisa ya kileo...🀣🀣😜😜😜
Wewe una kampuni ya kukopesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…