Mikosi au wakati wetu haujafika?

Mikosi au wakati wetu haujafika?

Pole sana mkuu. Jaribu kutafuta connection na hao hao waliofanikiwa nawe utatoka tu kimaisha wala hata usiwe na papara hata kidogo.

Kuna kipindi nilipitia kama unayopitia ila mwisho wa siku mambo yalienda tu vizuri. Kilichokuwa kinaniboa na kuumia ni pale wazazi walipokuwa wakinipigia simu kuniambia kuhusu mafanikio ya vijana tuliokuwa nao pamoja na kufika mbali zaidi na kunilaumu kuwa nachezea pesa kwa sababu siendi kujenga nyumbani bila kujua hali nilikuwa nayo na nilikuwa napitia nini kwa wakati huo.

Kila nilipowapigia simu ni kulaumu na kunitupia vijembe bila kujua kwa wakati ule nilikuwa napitia nini katika pambano la kuukimbia umasikini.

Kwa vile nilikuwa napenda amani ya moyo wangu na afya ya akili yangu niliwablock katika simu yangu ili kulinda afya ya akili yangu. Mambo yalipokaa sawa nikawafungulia. Sikuwablock kwa nia mbaya bali ukiona kitu kinaharibu afya ya akili yako ni bora ukakaa nacho mbali maana usipofanya hivyo utapata depression au stress bure.

Nimeipenda hii
 
Pole sana. Ebu ongea vizuri na wakurugezi wako then rudi hapa baada ya mwaka tupe mrejesho. Kama huwajui njoo pm
 
Na bado mkuu,, kadri siku zinaenda utazidi kushangazwa..

InShort Duniani lazima wapo waliofanikiwa zaidi yako,, na wapo uliofanikiwa zaidi yao... so hata ukiwa na Maisha waliokuzidi hawawezi kuisha watakuwepo tu..

Muhimu pambana na hali yako
 
kaka pole sana katika maisha usiwahi ogopeshwa na watu walio toka kimaisha na hasa ambao hujui wametoka toka vipi, sababu ya kuandika hivi ni kutokana na ukweli kuwa baadhi ya watu wanaotuumiza vichwa baadhi yao wanakuwa wametoka katika namna ambazo si sahihi yani wanakuwa wametumia njia chafu kupata mitaji ama hela, pili wengine wanatumia nguvu za giza kutoboa kimaisha.
umizwa kichwa na mtu ambaye umefanikiwa kujua namna alivyotoka kimaisha tuuu hao wengine wasikuumize kichwa maana unaweza kujinyima sana ili uwe kama yeye ilihali ni kitu kisichowezekena.
Furahia na rizika na maisha ulonayo tia jitihada kadri ya vile inawezekana, mkumbuke Muumba wako katika kukutia ulinzi wake na nguvu zake tuuuu
 
[emoji2][emoji2] af kwa kuwa ulikuwa kipanga darasan, ukafaulu kila unaekutana nae anajua una bonge la kaz pahara lazma aulize, wengine masnich tu anajua kila kitu bt anakuuliza makusud akutibue.

Mie naamin kufanikiwa kupo tu, Kama sio leo kesho.
Mie nmekuwa nkipata Hera tatzo haztunzik, zkija ndio macho yako yanaona vi Heineken na nyama choma. Nmeamua kukatilia mbali kila aina ya starehe nione ndan ya mwaka ntakuwa wapi?
Mwanangu wee kama mimi asee 😂💪😂
 
Kufanikiwa ni jambo la ajabu unaweza ukajaribu vitu vingi usifanikiwe ila unaweza jaribu kitu kimoja ukafanikiwa na ndio ikawa shughuli/ kazi yako.

Ukweli ni kwamba drop out kutoka shule wengi wanakua wamepiga hatua maana wanakua wanajua wafanye nini kwa jamii wapate pesa. Wana taarifa zote kuhusu soko na bidhaaa.

Kufanikiwa kunaitaji watu, wakupe maarifa, wakupe bidhaa, wakupe wateja. Changamoto ni watu hao unawapata vipi basi.
 
Robert kiyosaki ameliongelea sana jambo hili kwenye kitabu cha "Be rich & happy",
Na ameelezea kwa nin wasomi wana mafanikio ya kawaida ukilinganisha na drop out students

Pia, cha msingi uendelee kupambana kwa bidii na uzidi kumuomba mungu akusaidie

Lakini mwisho wa siku inabidi kumshukuru mungu, kwa sababu yeye ndo anajua kwa nin amekunyima ww na kampa yule
 
Robert kiyosaki ameliongelea sana jambo hili kwenye kitabu cha "Be rich & happy",
Na ameelezea kwa nin wasomi wana mafanikio ya kawaida ukilinganisha na drop out students

Pia, cha msingi uendelee kupambana kwa bidii na uzidi kumuomba mungu akusaidie

Lakini mwisho wa siku inabidi kumshukuru mungu, kwa sababu yeye ndo anajua kwa nin amekunyima ww na kampa yule

Ameen
 
Mkuu huwezi amini asee nikikosa hela nakuwa mzee wa mipango miji ila nikizipata tu gari langu linajua kabisa huyu chizi leo ataniendesha vibaya [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23] siku utakuta linapata tu hata hitilafu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
POLE SANA, SHUKURU UNA AFYA NJEMA NA UNA MDA WA KUPAMBANA ZAIDI. KUJITUMA KWA BIDII NI WAJIBU WAKO ILA MAFANIKIO NI MUNGU MWENYEWE ANA AMUA NANI ATANGULIE NA NANI AFATE BADAE..
CHUKUA HII: KUFANIKIWA KATIKA MAISHA NI KAMA MBIO KUZUNGUKA UWANJA MARA 12, KWENYE ROUND YA 3 AU YA 4 HUWEZI KUSEMA UMESHINDWA, FAINALI MIAKA 40 BRO. UKIFIKISHA UMRI HUO KAMA BADO HUJAPATA NDIO IMELALA YOOO... SAIVI RUDI VITANI MTALAM
 
Mkuu huwezi amini asee nikikosa hela nakuwa mzee wa mipango miji ila nikizipata tu gari langu linajua kabisa huyu chizi leo ataniendesha vibaya 😂😂😂
Aisee ume nichekesha sanaa, maana hapo pub zotee una hudhuria after week wese liter mbili mbili 😂😂😂😂😂
 
Kusoma ndio njia ya uhakika na sahihi kwa mafanikio kwa sisi tuliotoka familia masikini japokuwa kila kitu anapanga mungu, mimi nina mjomba wangu alisoma IT bachelor alikaa kitaa miaka minne ila alikuja kupata ajira ndani ya muda mfupi alinunua gari, kiwanja (kajenga mpaka kwenye linta bonge lajumba) ana mke na watoto kiufupi yupo vizuri kwa hyo ndugu yangu usikate tamaa mungu kila mtu kamuwekea njia yake katika maisha ya kufanikiwa.

just move on every thing will be ok
 
Kusoma ndio njia ya uhakika na sahihi kwa mafanikio kwa sisi tuliotoka familia masikini japokuwa kila kitu anapanga mungu, mimi nina mjomba wangu alisoma IT bachelor alikaa kitaa miaka minne ila alikuja kupata ajira ndani ya muda mfupi alinunua gari, kiwanja (kajenga mpaka kwenye linta bonge lajumba) ana mke na watoto kiufupi yupo vizuri kwa hyo ndugu yangu usikate tamaa mungu kila mtu kamuwekea njia yake katika maisha ya kufanikiwa.

just move on every thing will be ok

Poapoa kaka
 
Back
Top Bottom