Mikumi: Basi Standard Coach lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam lapata ajali

Poleni sana wote mliopata ajari lakini ili BUS ni bovu jamani nilivyoliona pale Mbezi stendi ,nilishangaa kuona mamlaka husika wakishindwa kulizuia ili Bus lisiendelee kutoa huduma kutokana na uchakavu na ubovu.
 
Mti umetulia ila gari limechakaa daah!!
Poleni sana wahanga. Kumbe ndio maana watu hung'ang'ania seat za upande wa dereva.
Ndio shida ya Body za kisasa ambazo asilimia kubwa ni Fiberglass.
 
Poleni Sana,
Hapo naona dreva Kama kawaida kaamua kasukumizia upande usio wake
 
@Mshana jr. [emoji12][emoji1787][emoji1787]
 
Huo mti utatoweka kama yule fisi wa Tabora kufikia kesho utachimbwa hadi mizizi.
Hahaaa, nauona unafaa kutibu nguvu za kiume..! Umebaki umesimama dede na michubuko kidogo licha ya gari kuharibika vibaya na abiria kuvuja damu.
 
Aisee,

Nimeona taarifa STANDARD bus ikitokea Iringa kwenda Dar imepata ajali Iyovi leo saa 3 asubuhi ikihusisha lori lililoingia site ya basi bila tahadhari na basi likakwepa na kwenda kugonga mti.

Kwa mujibu wa shuhuda hakuna vifo bali kuna majeruhi. Taarifa rasmi nadhani tapatikana kwa mamlaka husika.

Wenye ndugu na jamaa waliosafiri na basi hilo au kutoka Iringa kuelekea Dsm siku ya leo wanashauriwa kufuatilia kujua hali ya ndugu zao huko barabarani.

 
Duh jamaa kaitoa upande wao......! Alichofanyiwa na lori ndio huwa wanatufanyia wenye magari madogo. Tunawaombea majeruhi wapone haraka.
 
iyo takataka nilsishawahi kuipanda, inanuka hadi kunuka ndani humo. ni basi 3rd class kabisa na wanachelewaga kuondoka na njiani wanakimbia, waliturush akwenye matuta sitasahau.
 
iyo takataka nilsishawahi kuipanda, inanuka hadi kunuka ndani humo. ni basi 3rd class kabisa na wanachelewaga kuondoka na njiani wanakimbia, waliturush akwenye matuta sitasahau.
Mkuu umechefukwa!
 
iyo takataka nilsishawahi kuipanda, inanuka hadi kunuka ndani humo. ni basi 3rd class kabisa na wanachelewaga kuondoka na njiani wanakimbia, waliturush akwenye matuta sitasahau.
Upendo/Standard inabidi wajitathimini kwenye ubora wa mabasi yao. Mabasi mazuri yamekuwa ya kubahatisha. Abiria unakata tiketi kwa nauli ya semi luxury lakini unakuta gari halina hadhi hiyo isipokuwa viti tu ndiyo 2x2.
 
Umefika wakati ambapo mtu kabla hajapewa leseni ya kuendesha magari apimwe akili. Haiwezekani kila siku wataalamu wa masuala ya barabarani wanaongelea jambo hilohilo lakini watu hawaelewi. Hakuna tofauti na kumpigia mbuzi gitaa.

Mbaya zaidi, watu wanaona kazi ya udereva ni ya kukimbilia kila mtu; labda wanaona kuwa ni kazi rahisi kuliko kazi zingine, lakini ukweli ni kwamba kazi ya udereva sio rahisi kama watu wanavyofikiria, na ndio maana wanashindwa kuelewa sheria za barabarani.

Vyombo vinavyohusika na usalama barabarani, wapelekeni watu wanaohitaji leseni kwenye mamlaka husika ku-test uwezo wao wa kufikiri, vinginevyo ajali hazitaisha. Msiishie kuwaangalia viwango vya pombe tu, kwani ni dhahiri wengine hawapaswi kuendesha vyombo vya moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…