Mikutano inayozungumzia mikataba haitokuwa na maana bila kutaja MOU ya Serikali na kanisa

Naona Miungu wenu wa Kiarabu wanaitaka Tanganyika kwa Udi na Uvumba.

Mwambieni ukweli kwamba Tanganyika haiwezi kuwa Islamic state
Itakuwa Christian State??
 
Unajua Kanisa linaidai sirikali vyuo na shule ngapi ambazo Nyerere (mkatoliki mzuri) alitaifisha miaka ya 60 kwa lengo moja tu la kuwaokoa waislamu wasije wakaachwa nyuma mno na wakristo kimaendeleo? Unajua historia hiyo?
Bado mnataka kujilimbikizia tu.Hamtosheki ?
 
Mnashangaa hospitali za kanisa kuwalipisha wananchi gharama za huduma, lakini hamshangai serikali inayochukua kodi na tozo toka kwa mwananchi huyo huyo bado analipishwa gharama za huduma.

Kama mnaona hizo hospitali za kanisa gharama ipo juu, nani aliyewalazimisha muende huko? au aliyewakata msiende pengine? tatizo hapa sio serikali wala kanisa, ni ujinga wenu wenyewe.

Kwanza mna hakika hizo pesa za kusaidia huwa wanatoa zote kwa makanisa kama walivyokubaliana? serikali huwa haitoi pesa zote, ni hayo makanisa ndio yanajiongeza ili kufidia pengo la gharama linalojitokeza.

Mwisho, bandari zetu watanganyika mtazitema tu, msituletee ujinga wa udini ili kukwepesha malengo, hakuna anayedanganyika, mkataba wa hovyo wa bandari lazima uvunjwe, hatuwezi kugeuzwa watumwa ndani ya nchi yetu.
 
Ni hoja ya kijinga na ji upuuzi mtupu,mie juzi nilipeka binti yangu bugando,anashida ya kansa,nimetumia tsh 1732000/= laki 700000/.ni ruzuku ya serikali.kwa maana nimepewa dawa bure na serikali.hospital ya bugando inaongozwa kwa ubia na serikali. Sijui kwa mtizamo wako serikali pale imeuza nn cha wananchi?
 
Hapo kwenye tozo ni padogo sana.Watu yawezekana wanaona lakini wanavumilia kwa sababu pesa inaingia mfukoni kwa serikali na kwa namna moja au jengine mwishowe tutafaidika sote.Kwenye MOU ni kanisa peke yake na kujitanua
 
Pamoja na madudu ya mkataba wa bandari lakini ukweli usemwe, Huu mkataba wa Kanisa na serikali ambapo serikali imegeuka mtoa mtaji wa biashara za kanisa ni upendeleo wa wazi kinyume cha katiba inayokataza upendeleo kwenye matumizi ya resources za nchi.

Laiti huu mkataba ungekuwa ni kati ya serikali na taasisi za Kiislamu Kanisa lisingekubali

Kibaya Zaidi Kanisa halitaki serikali ijenge hospitali zake yenyewe mahali ambapo kanisa tayari lipo ili liendelee kutumia kodi za wananchi wote kustawisha baishara zake za huduma za afya. Hii ni kujaraibu kuinyang'anya serikali kuexert mamlaka ya sovereignty katika nchi kitu ambacho hakikubaliki.
 
Hospitali za misheni ndizo zilizowakuza bila hizo mngezaliwa kwenye majani ,serikali kwasasa ina hosptali nyingi hivyo kuna ulazima wa kureview hiyo MOU na kubakiza sehemu ambazo serikali haina hospital au ina huduma mbovu.
 
Kanisa linajimegea maeneo ndani ya nchi halafu linaitunishia serikali isisogelee.
 
Kwani ni bure ?

Lengo la serikali kuingia mikataba na makanisa kwasababu hospitali nyingi zilikuwa za Misheni(Missionaries) lilikuwa ni lengo zuri sana , waarabu walivyokuja walijenga masinagogi tu ,kwakuwa mzungu alikuwa na akili nyingi alijenga shule ,hospitali na makanisa akawapiga bao waarabu.(ambao walijenga misikiti tu).

Waislam wengi walisoma shule za misheni na kubadili majina ,hata JKIkwete alisoma shule za kikristo.

Kwahiyo serikali kuwalipa TEC kwasababu ya kutumia miuondombinu yao siyo tatizo ,kama waislamu wanaona nongwa basi na wao wajenge hospital nao wapate fedha.
 
Naunga mkono hoja 100%
 
Akili za wazungu ndio hizo hizo za kanisa,kufisidi vya wenzao halafu kufanya vya kwao ndio mwisho wa kila kitu.Wazungu wana akili gani kuwazidi waislamu.
Kwa mara ya mwanzo walipokuja ukanda wa Afrika mashariki walishangaa kuona waislamu wako mbali sana wana madrasa zilizoenea kila sehemu(Kumbuka madrasa zilifanya kazi inayolingana na shule).Walikuta watu wanajua kusoma na kuandika na ilibidi wawatumie waislamu kukushanya kodi wakiandika kwa herufi za kiarabu. Mara walipojiimarisha kifedha wazungu chini ya ukristo wakawapiga chini waislamu.Hali ni hiyo hiyo wakati wa siasa za kupigania uhuru.
Waislamu waliposoma shule za misheni ilikuwa ni katika tabia zao za kupenda kujifunza na kufuata kuliko na haki zao hata zikiwa mbali.Ilibidi wafanye hivyo baada ya kunyang'anywa vyao na wazungu kwa hila Sio kwamba walifanya kwa kupenda.
 
Bilioni 36,huwezi linganisha na uuzwaji wa bandari,kama vipi waislamu na nyie mjenge zenu,msilete mambo ya tukose wote

Jengeni na nyie


"Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?"
 
Jengeni na nyie hizo hospitali
 
Naona Miungu wenu wa Kiarabu wanaitaka Tanganyika kwa Udi na Uvumba.

Mwambieni ukweli kwamba Tanganyika haiwezi kuwa Islamic state
Kwani hiyo ardhi ya Tanganyika imeumbwa na nini?Kwani kwenye huo mkataba wa Bandari kuna sehemu inasema Dangayika itakuwa nchi ya kiislamu? Au malkia Elizabeth ndio alileta udongo kuka Uingereza na kuifukia bahari na kuifanya Tanganyika? Hiyo ni Tanganyika au Danganyika?Mikataba mingapi mibuvu na ya kitapeli imeshasainiwa tangu enzi za mchonga meno kwa hao mabwana zenu wazungu na kuwaacha Wadanganyika wengi katika dimbwi la umasikini wa kutupwa.Mbona hampigi kelele Kwa rasimali zilizopo huko Tanganyika zinaporwa na wazungu toka enzi na enzi.
 
incredible story.
1992 Rais alikuwa Mwnyi ambaye alikuwa na nguvu zote za kimamuzi na katika utaratibu wa kawaida serikali haikuwa na namna kwa vile ilikuwa ni muhimu sana huduma za kijamii ķama hospitali kufika kwa wananchi na nguvu ya serikali kufanya hivyo ilikuwa ndogo lakini ndio namna pekee ya kushirikisha sekta binafsi.
Hiki ndio kipindi tulianza kutoka kwenye mfumo wa kijamaa na kuanza kusambaza huduma za kijamii kwa kasi na katika ule mkataba serikali haina resources control kwani haya makanisa hununua wenyewe. Serikali inachangia sehem kama kulipa mishahara baadhi ya watumishi.
Kuweka kumbukumbu sawa hawa viongozi wa kitaifa wamekuwa wakijihusisha na shughuli zote bila kujali dhehebu/dini ndio maana hizo hospitali watu wanapewa huduma kwa usawa. Na ajira zilizopo kwenye hayo makanisa kwa watu wa dini zote.
...............................................................................................
Nchi hii haina udini wote kwa pamoja we share the same interest tupunguze mihemuko tutafute maisha.
 
Baba wa Taifa letu alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana sawa sawa na kula nyama ya kula mtu. Mmeanza ubaguzi, mmeanza na Tanganyika na Zanzibar sasa mmekuja kweli udini, mtaenda kwenye ukabuila mtafika mpaka kwenye koo na sidhani km mtaishia hapo. Mimi naishauri serikali yangu iwe tu imara kuwadhibiti watu wapumbavu km wewe.
 
Kwa kifupi ungependa hospitali za misheni ziwahudumie wamisheni peke yao kwa sababu hizo hospitali zilijengwa kutokana na sadaka za wamisheni? Au ungependa wamisheni walipe kidogo na wengine walipie gharama halisi?

Unawatajaje viongozi waliohusika na hiyo MoU halafu ukamuacha bosi wao ambae alikuwa ni Rais Ali Hassan Mwinyi?

Utazungumziaje ESCROW bila kumtaja Rais muislamu Kikwete ambae aliyetuhakikishia kuwa zile pesa sio zetu? Hao maaskofu unaozungumzia walipewa pesa na mkatoliki mwenzao ambae tuliambiwa na Rais muislamu kuwa zile pesa ni zake? Mkatoliki huyo aliyetoa hizo pesa alitiwa ndani na Mkatoliki mwenzake lakini hatimae aliachiwa chini ya utawala wa Rais wa kiislamu!

Kwa nini unazungumzia hospitali peke yake? Zungumzia pia shule ambazo wamisheni walirudishiwa na wahimize waislamu wasipeleke watoto wao kwenye shule hizo?
Unamlaumu Askofu Mndolwa kwa "kuilaumu" serikali kwa kujenga hospitali sehemu ambapo ipo tayari hospitali ya kanisa inayotoa huduma bila kuelewa kuwa alichokuwa anasema ni bora hiyo hospitali ingejengwa mahali ambapo hamna kabisa hospitali ya aina yeyote. Sehemu hizo ziko nyingi tu katika nchi yetu.

Unashindwa kuelewa kuwa watu wataendelea kupeleka wagonjwa wao katika hospitali za misheni hata kama kuna hospitali za serikali zilizo karibu zaidi. Watu wako tayari kusafiri masaa sita kufuata hospitali ya wamisheni wakati hospitali ya serikali iko umbali wa mita mia kutoka anakoishi.

Wavunje hiyo MoU halafu uone ni watu gani watasomea udaktari katika hospitali za Bugando, KCMC na hata ya Kariuki ambayo sio ya kanisa.

Ukweli ni kuwa ukiingiza udini katika kila kitu utawaharibia zaidi waislamu wenzako ambao wanahudumiwa bila kubaguliwa katika hizi hospitali za wamisheni. Hii ni kwa sababu wamisheni wamejenga hospitali nyingi zaidi katika maeneo mengi ya nchi yetu kuliko taasisi za kiislamu.

Watu kama wewe mnasikitisha sana. Mnabomoa kuliko kujenga kwa sababu tuu mnadhani ummah ni muhimu kuliko taifa letu.

Amandla....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…