Mikutano inayozungumzia mikataba haitokuwa na maana bila kutaja MOU ya Serikali na kanisa

Mikutano inayozungumzia mikataba haitokuwa na maana bila kutaja MOU ya Serikali na kanisa

Jengeni na nyie za kwenu
Wazo zuri ingekuwa ni kuvunjwa MOU kwanza au kugawana hizo hospitali zilizojengwa kwa kodi na zetu pia.Lakini kama hamtapenda hilo dunia ni pana sana hilo halitushindi.Muhimu tukianza tusisikie kelele kama zile za askofu eti DP World watajenga misikiti.Kama DP World wakijenga msikiti Mbeya kwa sasa hauna uhusiano na mkataba wa bandari na tayari mumeshaanza kulalamika.Kwa vile DP World wala hawajaanza shughuli Tanzania.
Kumbuka rasilimali nyingi duniani ziko kwenye maeneo yanayomilikiwa na waislamu hivyo tukiwafuata watujengee vya kwetu na hivyo vya kwetu sote tukawawachia nyinyi basi musifanye nongwa.
 
Wazo zuri ingekuwa ni kuvunjwa MOU kwanza au kugawana hizo hospitali zilizojengwa kwa kodi na zetu pia.Lakini kama hamtapenda hilo dunia ni pana sana hilo halitushindi.Muhimu tukianza tusisikie kelele kama zile za askofu eti DP World watajenga misikiti.Kama DP World wakijenga msikiti Mbeya kwa sasa hauna uhusiano na mkataba wa bandari na tayari mumeshaanza kulalamika.
Kumbuka rasilimali nyingi duniani ziko kwenye maeneo yanayomilikiwa na waislamu hivyo tukiwafuata watujengee vya kwetu na hivyo vya kwetu sote tukawawachia nyinyi basi musifanye nongwa.
Acha mboyoyo,jengeni kwanza Kisha ulete mada yako
 
Kwahiyo ni serikali inapambana na kanisa katoliki au ni nini zaidi? Kama unapambana na kanisa wala. Usijali majibu yapo na idadi ya wakristo inajulikana ukubwa wake tutaungana ili mpambano uwe mzuri uchaguzi ujao
 
Kwa kifupi ungependa hospitali za misheni ziwahudumie wamisheni peke yao kwa sababu hizo hospitali zilijengwa kutokana na sadaka za wamisheni? Au ungependa wamisheni walipe kidogo na wengine walipie gharama halisi?

Unawatajaje viongozi waliohusika na hiyo MoU halafu ukamuacha bosi wao ambae alikuwa ni Rais Ali Hassan Mwinyi?

Utazungumziaje ESCROW bila kumtaja Rais muislamu Kikwete ambae aliyetuhakikishia kuwa zile pesa sio zetu? Hao maaskofu unaozungumzia walipewa pesa na mkatoliki mwenzao ambae tuliambiwa na Rais muislamu kuwa zile pesa ni zake? Mkatoliki huyo aliyetoa hizo pesa alitiwa ndani na Mkatoliki mwenzake lakini hatimae aliachiwa chini ya utawala wa Rais wa kiislamu!

Kwa nini unazungumzia hospitali peke yake? Zungumzia pia shule ambazo wamisheni walirudishiwa na wahimize waislamu wasipeleke watoto wao kwenye shule hizo?
Unamlaumu Askofu Mndolwa kwa "kuilaumu" serikali kwa kujenga hospitali sehemu ambapo ipo tayari hospitali ya kanisa inayotoa huduma bila kuelewa kuwa alichokuwa anasema ni bora hiyo hospitali ingejengwa mahali ambapo hamna kabisa hospitali ya aina yeyote. Sehemu hizo ziko nyingi tu katika nchi yetu.

Unashindwa kuelewa kuwa watu wataendelea kupeleka wagonjwa wao katika hospitali za misheni hata kama kuna hospitali za serikali zilizo karibu zaidi. Watu wako tayari kusafiri masaa sita kufuata hospitali ya wamisheni wakati hospitali ya serikali iko umbali wa mita mia kutoka anakoishi.

Wavunje hiyo MoU halafu uone ni watu gani watasomea udaktari katika hospitali za Bugando, KCMC na hata ya Kariuki ambayo sio ya kanisa.

Ukweli ni kuwa ukiingiza udini katika kila kitu utawaharibia zaidi waislamu wenzako ambao wanahudumiwa bila kubaguliwa katika hizi hospitali za wamisheni. Hii ni kwa sababu wamisheni wamejenga hospitali nyingi zaidi katika maeneo mengi ya nchi yetu kuliko taasisi za kiislamu.

Watu kama wewe mnasikitisha sana. Mnabomoa kuliko kujenga kwa sababu tuu mnadhani ummah ni muhimu kuliko taifa letu.

Amandla....
Angalia basi unapomtaja raisi Ali Hassan Mwinyi kwamba alikuwepo wakati wa kutiliana saini makataba wa MOU utaona kuwa viongozi waislamu wanapolelekwa wazo la kuendeleza huduma za kijajmii husahau ubaguzi.
Kwa upande wenu mkataba wa bandari mumesahau yote na kuingiza udini na ukabila kwa raisi muislamu japokuwa mkataba hauhusiani kabisa na Uislamu bali dira yake ni maendeleo ya taifa na kuwahi kunyang'anywa shughuli za bandari na mataifa yasiyokuwa na bandari.
 
Inabidi tuanze kujibu kwa maandishi maana huwezi kulinganisha mkataba mbovu wa bandari eti upate kibali kisa kuna Mou na kanisa uzwazwa uliopitiliza
 
TEC wameshajibu vunjeni mkataba na wao na wale watumishi walioajiriwa na serikali kwenye hospitali zenu watoeni wao watajiendesha vizuri na mambo yataenda kikubwa mkataba wa bandari ni haufai hata kwa bure
 
TEC inasema serikali iuvunje mkataba wake hata leo wao hawawezi kunyenyekea mtu milele
 
Kama kuna mikutano inayozungumzia mikataba mibovu basi kusiwe na ubaguzi.Muda umefika sasa wa kuitaja mmoja mmoja. Mengine irekebishwe na mingine ipo haja ya kuvunjwa mjoja kwa moja

Mpaka sasa wale wanaokosoa mkataba wa bandari naona wamekaa kimya kwa mkataba ule wa kanisa na serikali wa mwaka 1992.Si lazima wausome wote hata kutaja tu udhaifu wa hoja za wale wanaotilia shaka mkata huo ingetosha kusawazisha hoja za utetezi wa zinazoonekana kasoro za mkataba wa DP World.

Naamini wote walikuwa wanaujuwa na kama ilikuwa bado basi wamesikia kelele za walalahoi.Kelele hizo ni kama hizi kwenye bandiko hapo chini :

WAKATI MNAPAMBANA KUONDOA KIFUNGU HEWA CHA MKATABA WA MILELE (ambacho hakipo) WEKENI NA AKIBA YA MANENO.

TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.

Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika …
Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.
MOU za ndani ya nchi sio shida sana zinamaslahi kwa watanzania bila kujali dhehebu wala dini issue ni hizo za kimataifa nitatizo sana.
 
Ami

Hakuna jawabu la maana hapa utakalopatiwa. Zaidi umeona wanatetea. Ila ingelikuwa kinyume chake Waislamu ndiyo wamepewa hiyo fursa ungeliwaona kelele zao.
Chuo kimoja tu MUM kilichotokana na kodi zetu sote imekuwa nongwa na masimbulizi kila siku.Kumbe lile ni tone tu kati ya kodi za waislamu.
 
Chuo kimoja tu MUM kilichotokana na kodi zetu sote imekuwa nongwa na masimbulizi kila siku.Kumbe lile ni tone tu kati ya kodi za waislamu.
Na kupiga kelele kote huko kwa maaskofu si huwa wanapitisha vitu vyao bandarini wakisema misaada ya kidini.

Sasa akikabadhiwa mwengine wao watafaidika wapi? Hilo ndilo linalowasumbua na wala si kingine!

Laiti kungelikuwa na maslahi yao wasingelipiga kelele hawa na maaskofu wao.
 
Hapo kwenye tozo ni padogo sana.Watu yawezekana wanaona lakini wanavumilia kwa sababu pesa inaingia mfukoni kwa serikali na kwa namna moja au jengine mwishowe tutafaidika sote.Kwenye MOU ni kanisa peke yake na kujitanua
Nilijua tu una upeo mdogo ndio maana ukaleta hili andiko hapa. Kanisa linatanuliwa kwa sadaka na michango makanisani, ndio maana wakawa wa kwanza kujenge hospitali na mashule mpaka serikali ikavutiwa kuwapa nguvu.

Unaposema pesa ya kodi inaingia mikononi mwa serikali, hivyo kwako ni sawa kugharamia huduma nyingine za serikali kama hospitali, kwanini usigharamie huduma za hospitali za kanisa, kama hamtaki nanyi jengeni mahospitali yenu serikali iwasaidie, lakini sio mnalia kwa kukosa uwezo.

Tatizo upeo, ndio maana mnatumika kirahisi na serikali kuficha madudu ya mkataba mbovu wa bandari.
 
Pamoja na madudu ya mkataba wa bandari lakini ukweli usemwe, Huu mkataba wa Kanisa na serikali ambapo serikali imegeuka mtoa mtaji wa biashara za kanisa ni upendeleo wa wazi kinyume cha katiba inayokataza upendeleo kwenye matumizi ya resources za nchi.

Laiti huu mkataba ungekuwa ni kati ya serikali na taasisi za Kiislamu Kanisa lisingekubali

Kibaya Zaidi Kanisa halitaki serikali ijenge hospitali zake yenyewe mahali ambapo kanisa tayari lipo ili liendelee kutumia kodi za wananchi wote kustawisha baishara zake za huduma za afya. Hii ni kujaraibu kuinyang'anya serikali kuexert mamlaka ya sovereignty katika nchi kitu ambacho hakikubaliki.
Hili la kusema kanisa halitaki serikali ijenge hospitali zake yenyewe tuwekee ushahidi hapa..

Huo mtaji serikali inayoutoa unatosha kugharamia hizo huduma? una hakika serikali huwa inatoa pesa zote?

Na unapoandika kama hizo hospitali zingekuwa za misikiti, makanisa yasingekubali, una uhakika au ushahidi upi?

Kwanini basi hiyo misikiti isijenge mashule na hospitali zao ili nao wapate hiyo misaada mnayoililia, kuliko kusema ifutwe halafu gharama za huduma zizidi kupanda?

Punguzeni mihemko kwenye kujadili haya mambo.
 
Back
Top Bottom