Mikutano inayozungumzia mikataba haitokuwa na maana bila kutaja MOU ya Serikali na kanisa

Napenda sana viongozi wa madhehebu ya kikristo
Ni watu makini wana elimu ya kawaida na elimu ya dini
Na ata nyie mashia mnaruhusiwa kujenga hospitali na kuingia mkataba na serikali kama kanisa lilivyofanya.
Hatutaki jasho letu kunufaisha kanisa au msikiti,ni unyonyaji, mkataba uvunjwe
 
Interesting thread...
Utaona hakuna ataejibu hoja zaidi ya matusi .. surprisingly Chadema na Wakatoliki huwa wamoja kwenye anything against Muslims... against Islam....

Na wote humshambulia Kwa matusi
Umesema chadema na wakatoliki,wote hao ni wakiristo!!..ni heri mlokole,kkkt anavumilika,hufanya alama ya msalaba kuliko muislam/uislam
 
Hatutaki jasho letu kunufaisha kanisa au msikiti,ni unyonyaji, mkataba uvunjwe
Hamna jasho nyie, wacha kujitutumua hapa, mngekuwa nalo mngeshajenga hospitali na mashule yenu, kisha serikali iwape misaada mnayoililia.

Nyie mna midomo tu, ya kupiga kelele kila siku, na machozi ya kulia lia kila siku.
 
Hamna jasho nyie, wacha kujitutumua hapa, mngekuwa nalo mngeshajenga hospitali na mashule yenu, kisha serikali iwape misaada mnayoililia.

Nyie mna midomo tu, ya kupiga kelele kila siku, na machozi ya kulia lia kila siku.
Akili huna..kodi zetu hatutaki ziende kanisani,toka mkoloni anakusanya Kodi kwa wote anawapa kanisani peke yao,hatutaki Kodi zetu kuwa mitaji ya biashara za kanisa,wajitegemee
 


Hiyo tumekuachia wewe utuwakilishe
 
Sasa jibu swali,
Hizo hospitali watu hutibiwa bure ?
 
Kwa hilo unataka kutuambia kuwa marais wa Kiislamu ni dhaifu kiasi kuwa wanaburuzwa tu na wamisheni? Marais kama Shein na Kikwete walitumwa na wakatoliki kuwatia ndani ma shehe wa kiislamu?

Mnaouingiza dini ni nyinyi katika hili suala la Zanzibari kwa sababu hamuwezi kutenganisha uzanzibari, uarabu na uislamu. Hao hao unaowasema kuwa wanaingiza udini katika mjadala huu hawakusita kumpigia kelele rais mkatoliki katika miradi yake ya ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, ununuzi wa ndege n.k. Hao hao wamekuwa msitari wa mbele kuisema serikali kuhusu kesi za mashehe wenu hata katikasuala la utaifa wa Zanziba. Wengi wao wamelipa gharama kubwa kwa sababu ya msimamo wao. Unalalamika kuhusu watu kuzungumzia kabila ya Rais wa sasa wakati watu wakizungumzia Sukuma Gang unakaa kimya.

Kama unaona mkataba huu una manufaa katika maendeleo ya taifa hilo utetee kwa hilo na sio uwatuhumu wote wanao ukosoa kuwa hawana uzalendo na ni wadini. Ni haki ya wakristu na waislamu kukosoa mkataba na utendaji wa kiongozi yeyote wa kitaifa bila kujali dini yake.

Magufuli alisemwa sana lakini sikuwahi kuwasikia wamisheni wakiwakataza waislamu kumkosoa. Sijawahi kumsikia mtu akisema kuwa Zitto alikuwa anampinga JPM kwa sababu alikuwa mkatoliki. Wakati Mbowe ametiwa ndani hamna mmisheni aliyesema kuwa alifanyiwa vile kwa sababu ni mkristu na rais ni muislamu.

Mnakotaka kutupeleka siko. Uzuri ni kuwa waislamu wengi wamewastukia na hawako tayari kuingia kwatika mtego wenu wa udini. Mko peke yenu kwenye hili.

Amandla...
 
KKe
Kelele zoote hizi kumbe hata GOVI umekatwa hosp. Za misheni
 
Watu hao wanahisi kubaguliwa na kutengwa kutokana na ukosefu wa maarifa muda mwingi wanaupoteza kudai haki ambayo wao wenyewe hawajui.. wamedanganywa Adui wanapambana na adui ambaye sio ..
Nduguzangu Muslims adui ni ujinga na magonjwa na sio mkristo.. sasa msikaze mafuvu yenu kuwaza namna ya kupambana na mkristo kwa namna yoyote.. sisi sote ni ndugu kumbuka izo dini zilkuja na mashua... hapa kikubwa tuzilinde rasilimali zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ndugu zangu waislam bado hamjajua nguvu ya Kanisa Catholic kwenye Dunia hii,Kila siku mnakaa kulalamikia kanisa Catholic kuhusika ktk mapinduz mashariki ya kati,kuanzishwa kwa Bakwata,kunyimwa MOU n.k!Kiufupi hili kanisa ndilo linatawala Dunia baada TU ya Roma Empire kusambaratika!!Jiulizeni kwanini Maalim Seif baada ya kupokwa ushindi na Jecha aliandika barua kwa Papa kuomba aingilie kati mgogoro wa Zanzibar????
 
Serikali ya Mkapa ilichukua Chuo Kikuu cha Taasisi ya Serikali kilichokuwa Morogoro na kuwapa waislamu watumie kama Chuo Kikuu chao na hamna mmisheni aliyelalamika. Na tuambie kama waislamu wanasoma bure katika hicho Chuo Kikuu chenu.

Huu Mkataba unaopigia kelele ulihusu shule na hospitali zilizojengwa na taasisi za kidini ambazo serikali ilitaifisha . Tuambieni ni taasisi ngapi za kiislamu ambazo hospitali zao zilitaifishwa na serikali?

Kanisa halina mamlaka au nguvu za kuizuia serikali kujenga hospitali sehemu yeyote wanayotaka. Wanachofanya ni kutoa ushauri kuwa ni bora serikali itumie resources zake kujenga hospitali mahali ambapo hakuna kabisa hospitali kuliko kujenga mahali ambapo tayari kuna hospitali ambayo inatoa huduma hizo kwa gharama nafuu. Kama hauoni mantik ya ushauri huu basi hauwatakii mema watanzania ambao hadi leo wanasikia huduma za hospitalikwenye redio tu. Hii MoU imewawezesha watanzania wengi bila kujali dini zao kupata huduma bora na kwa gharama ndogo kuliko ambavyo serikali ingeweza kutoa kwa kutegemea tu resources zake yenyewe.

Amandla...
 
Kwani tunaongelea hospitali Za serikali au Za kanisa , ambazo hulipiwa na serikali ?
Za serikali hazijengwi kwa kodi yako? kama ni hivyo kwa nini utake hospitali za kimisheni peke yake zitoe huduma bure kwa sababu tu serikali inachangia uendeshaji wake?

Amandla...
 
Ishaurini serikali sikivu irudishe kwa kanisa hospitali nyingi nchini za kanisa ili ziwahudumie walengwa na ziwe private.
Kuna hospitali za KCMC na Bugando na nyingine nyingi tu.
Na tusiishie katika mahospitali.
Shule za Misheni na za makanisa ni bora zirudi tu kwa wenyewe.
 
Ukileta udini baba , hii nchi hatokuja kutokea Tena Rais Muislamu, Mana takwimu waislamu ni Asilimia 30%tu, Sasa nakushauri jikite kwenye Hoja, achana na udini
 
Kule Maweni Moshi hospitali tunatumia pesa kutibiwa na kule Kcmc tunatumia pesa kutibiwa. Kule Ifakara hospital na Pale St Francis tunatumia Pesa kutibiwa na wala haulizi dini . Tuache kujadili kilimbukeni . Kwenye hiyo miradi bado tunaofaidika ni sisi Wananchi . Nyie subirini hukumu ya mahakama mbeya.
 
Bado mnataka kujilimbikizia tu.Hamtosheki ?
Siku zote tangu uhuru waislam wanatendewa kwa upendeleo kama walivyo wamasai na wengine. Sasa ni ufike wakati mambo hayo yakome.
 
Sasa jibu swali,
Hizo hospitali watu hutibiwa bure ?

Nadhani somo la civics lilikupita ,hivi unajua gharama za hospital za binafsi na serikalini? Fanya utafiti kisha uje kuuliza swali lako....inaonekana haujui kazi ya serikali kwenye kutoa huduma kwenye jamii huwa wanafanya kitu gani....Kama Serikali inawapa mabilioni makampuni ya simu wajenge minara ku serve wateja wao ndiyo unashangaa serikali kuwapa TEC fedha?
 
Bado mnataka kujilimbikizia tu.Hamtosheki ?
Halafu acheni dhana potofu kuwa Serikali inasadia uendeshaji wa hospitali za Kanisa,hizi hospitali zilikuwepo muda mrefu kabla ya 1992.Kilichotokea ni kwamba Serikali iliwapeleka watumishi wake kule kwa hiyo inawalipa mishahara yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…