Mikutano Miwili ni maua ya demokrasia yanayochanua katika ardhi ya China

Mikutano Miwili ni maua ya demokrasia yanayochanua katika ardhi ya China

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Mikutano Miwili Mikubwa ya China, ambayo ni Mkutano wa Bunge la Umma la China na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China inafanyika hapa Beijing, na wajumbe zaidi ya 5,000 wanakutana na kujadili masuala ya mbalimbali ya kitaifa.

Kama njia muhimu ya kutekeleza demokrasia ya kisoshalisti yenye sifa za Kichina, mikutano hiyo miwili inayofanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi Machi ni vigumu kupata mfano mwingine katika vitabu vya demokrsia vya nchi za magharibi. Hii ni matokeo ya uzoefu wa utawala wa Chama cha Kikomunisti cha China, na ni maua ya demokrasia yanayochanua katika ardhi ya China.

China ina desturi ya kidemokrasia tangu zama za kale. Kutoka “Mkutano wa Kitaifa wa Umma” katika Enzi ya Zhou Magharibi miaka 3000 iliyopita hadi “Mkutano wa Chumvi na Chuma” katika Enzi ya Han zaidi ya miaka 2000 iliyopita, kutoka mfumo wa kisiasa wa majimbo matatu na wizara sita katika Enzi ya Tang miaka 1400 iliyopita hadi mfumo wa baraza la mawaziri katika Enzi za Ming na Qing mamia ya miaka iliyopita, tangu mwanzo siasa ya kushauriana na kujadiliana inapitia historia ya ustaarabu wa China. Ingawa mifumo hiyo ina dosari mbalimbali, lakini imetoa chachu kwa mfumo wa kisasa wa kisiasa nchini China.

Tangu kuanzishwa kwake, Chama cha Kikomunisti cha China kimejikita katika kutafiti mfumo wa kidemokrasia unaoendana na hali ya kitaifa. Kuitishwa kwa mkutano wa kwanza wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China mwaka 1949, kuliashiria kuzaliwa kwa mfumo mpya wa kisiasa wa kidemokrasia nchini China.

Tangu kutekelezwa kwa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, mfumo wa mikutano miwili umeendelea kuboreshwa. Chaguzi za moja kwa moja za wajumbe wa bunge la serikali za mitaa umepanuliwa kutoka vijijini hadi wilaya na miji, huku uwakilishi wa wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa pia umepanuliwa.
Mikutano Miwili ina uwakilishi mkubwa.

Kati ya wajumbe 2,977 wa Bunge la 14 la Umma la China, asilimia 16.69 ni wafanyakazi na wakulima wanaofanya kazi katika mstari wa mbele, asilimia 21.3 ni wataalam na wasomi, asilimia 14.85 wanatoka makabila madogo, na makabila madogo yote 55 nchini China yana wawakilishi wao kwenye Bunge la Umma.

Muundo huu wa uwakilishi unahakikisha kwamba maslahi ya makundi mbalimbali yanaweza kuonyeshwa katika jukwaa la juu zaidi la kisiasa nchini China.

Mfumo wa kidemokrasia wa mikutano miwili pia umeonesha ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa mkakati wa maendeleo ya kitaifa. Kuanzia Mpango wa kwanza wa Miaka Mitano hadi Mpango wa 14 wa Miaka Mitano, kiwango cha utekelezaji wa mipango hiyo kimezidi asilimia 90. Pia, kupitia mipango hiyo, China imepata maendeleo makubwa.

Katika vita dhidi ya umaskini, wajumbe wa Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa walitoa mapendekezo karibu 50,000 muhimu, na hatimaye watu wote maskini milioni 98.99 nchini China walifanikiwa kuondokana na umaskini.

Anuwai ya staarabu za kisiasa ni msukumo wa maendeleo ya binadamu. Hekima ya kisiasa inayoonyeshwa na mfumo wa Mikutano Miwili ya China imeleta nguvu mpya kwa maendeleo ya ustaarabu wa kisiasa duniani.
 
CCM na wenyewe huwa wanasema demokrasia inakua nchini nyie wakomunisti na chawa wenu wa huku mna vituko kweli.
 
Back
Top Bottom