Mikutano Miwili ya China yazingatia kulinda haki na maslahi ya wanawake

Mikutano Miwili ya China yazingatia kulinda haki na maslahi ya wanawake

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111372224163.jpg


Pili Mwinyi

Kwa miaka mingi China imekuwa ikiimarisha sheria na kanuni zake zinazomhusu mwanamke, kukuza sera za umma, kufanyia kazi mipango ya maendeleo na kuendeleza masuala ya usawa wa kijinsia na maendeleo ya wanawake.

Katika mikutano miwili inayofuatiliwa sana nchini China, ulinzi wa haki na maslahi ya wanawake ni mambo ambayo yanaendelea kuwekewa mkazo mkubwa na kuzingatiwa kila mwaka, lakini kwa mwaka huu yanafuatiliwa zaidi. Sababu kubwa ni kwamba kuanzia mwishoni mwa mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu, Sheria ya Kulinda Haki na Maslahi ya Wanawake yaani Rasimu ya Marekebisho, ilikusanya maoni ya umma, ambapo watu zaidi ya 80,000 walitoa maoni yao zaidi ya laki 4.2, kiasi ambacho kinaongoza rasimu nyingine za marekebisho ya sheria ya safari hii.

Miongoni mwa wajumbe waliotoa mapendekezo yao kwenye mikutano hiyo kwa niaba ya wananchi, wanawake wanachukua nafasi kubwa zaidi, wakiwa ni pamoja na wanasheria, wasomi, waandishi wa filamu n.k. Wajume hao walikusanya maoni ya wanawake, wakaonesha matatizo na kadhia mbalimbali zinazowakabili wanawake, na kufanya kila liwezekanalo kuhimiza utatuzi wa matatizo yanayowakabili.

Matatizo hayo ni pamoja na magenge haramu yanayouza wanawake, matatizo ya afya hasa saratani ya shingo ya kizazi, udhalilishaji wa wanawake n.k.

Kwa mujibu wa takwimu, mwaka 1999 watuhumiwa wa kesi zaidi ya 6,800 waliofanya biashara haramu ya kuuza wanawake na watoto walikamatwa nchini China, wakiwa na jumla ya wanawake 7,600, na kati ya mwezi Aprili na Juni mwaka 2000, wanawake 43,527 waliokolewa.

Mjumbe wa Bunge la Umma la China Jiang Shengnan alipendekeza kuongeza kiwango cha adhabu kwa watu wanaonunua wanawake au watoto wanaouzwa ama kusafirishwa, pamoja na kuhusisha tathmini ya kazi za serikali katika ngazi mbalimbali na mapambano dhidi ya biashara haramu ya watu.

Anasema sababu kuu inayofanya magenge ya wahalifu hao kushughulikia biashara haramu ya wanawake ni kutokana na mahitaji ya wanunuzi. Hivyo anashauri kwamba hadi pale soko la manunuzi litakapodhibitiwa, ndio uhalifu huu utakapotokomezwa kabisa.

Saratani ya shingo ya kizazi umekuwa ugonjwa unaosumbua sana wanawake duniani. Ili kuhakikisha afya ya wanawake, mikutano hii pia iliangalia kwa jicho la tahadhari ugonjwa huu. Wahenga wanasema afya ni uhai, na nyumba yenye mwanamke mwenye afya njema basi daima itakuwa na furaha. Nchini China saratani ya shingo ya kizazi inashika nafasi ya pili katika vifo vya wanawake watu wazima wenye umri wa miaka 25-59, kukiwa na wagonjwa wapya 110,000 kila mwaka. Wakati huo huo, saratani ya shingo ya kizazi ni ugonjwa ambao unaweza kuzuilika na kutibika, kwani kuna chanjo inayoweza kuzuia kutokea kwa saratani ya aina hiyo.

Hivi sasa chanjo ya HPV inaweza kutolewa kwa hiari hapa China, hata hivyo ukweli ni kwamba kuweka nafasi ya kwenda hospitali kupatiwa chanjo hiyo ni ngumu sana, tena gharama zake ni kubwa. Pia kiwango cha wasichana wenye umri unaofaa kupatiwa chanjo ya HPV kiko chini ya asilimia 1. Kwa kuzingatia hilo, Mjumbe wa Bunge la Umma la China Xu Ping anapendekeza mwaka huu kueneza chanjo ya HPV bila malipo kwa wanawake wenye umri unaofaa kupatiwa chanjo.

Mjumbe wa Bunge la Umma la China Zhai Meiqing naye pia ametetea wanawake kwenye mikutano hiyo, akipendekeza kuimarisha kazi ya utoaji wa huduma za umma za serikali, ili kuwawekea sera na hatua nyingi zaidi wanawake hasa wale waliojifungua, kama vile kwenye maeneo yenye watoto wachanga au wadogo, ujenzi wa mitaa inayotoa huduma husika, na kutoa msaada kwa wingi zaidi wa maisha kwa familia zenye watoto wawili hata watatu.

Ni jambo zuri kuona kuwa haki na maslahi ya wanawake yanafuatiliwa katika Mikutano Miwili ambayo ni muhimu sana nchini China. Bila shaka, pamoja na hayo, cha muhimu zaidi ni kuona kwamba baada ya mikutano hii, masuala yote haya yanatekelezwa kwa ufanisi. Aidha tunatumai kuwa zitakuwepo sera nyingi zaidi zitakazonufaisha wanawake, huku ukianzishwa utaratibu wa ulinzi wa wanawake katika sekta muhimu, ili kutoa msaada wa kisheria, na kuadhibu vikali zaidi vitendo vinavyowadhuru wanawake.
 
Back
Top Bottom