Mil.800 mpaka bil.1 mshahara na marupurupu ya mbunge,si upinzani wala fisiemu wanalizungumzia

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
368
Reaction score
556
Habari wakuu

Sijsikia viongozi wa upinzani wakiliongelea hili kwa nguvu,wala fisiemu

Marupurupu kuwa makubwa yasio akisi hali ya wanaotuwakilisha ni chanzo cha kuwa na vibaraka sio tuu wa kuacha serikali ifanye inavyotaka,lakini kuwa muhuriwa mambo ambayo hayana maslahi kwa nchi yetu au yanayotuumiza wananchi mathalani mikataba mibovu ya kimataifa na kitaifa

Wanakuwa ni wahalalishaji wa mambo ya hovyo wa viongozi wapumbavu wanaoweka maslahi yao mbele badala ya taifa

Ni kweli wako vijana ambao hao watawala wameshawaharibu akili kwa makusudi,wanafikiria kwa turbo,hao tusiwatusi ni victims of the circumstance

Kuna logic ipi ya kumlipa mbunge pesa yote hiyo kwa miaka mitano tuu?

Kwa mwezi mbunge anakusanya mpaka mil.22,hii inalipa madaktari wangapi ngazi ya degree na kuna hospitali ngapi na vituo vya afya tunalalamika hatuwezi kupeleka watumishi mpaka USAID watusaidie?Trump abarikiwe popote alipo

Walimu wengi madai yao hayazidi hata mil 2...wengine wamezunguka na bahasa mpaka wamekufa na pesa zao zimeliwa

Hao hao watu wanakuja wanawaambia wao ni watetezi wenu,wawakilishi wenu,hivi tuna akili timamu kweli?

Acha niishie hapa
 
Msikilizeni Tupac Amaru Shakur
 
Naomba MUNGU aamshe akili zetu watanzania ili kwanza tutake maslahi ya wanasisa wote yapunguzwe , maana hata wapinzani hawasemi Hilo kwenye ilani zao !
 
Habari wakuu

Sijsikia viongozi wa upinzani wakiliongelea hili kwa nguvu,wala fisiemu

Marupurupu kuwa makubwa yasio akisi hali ya wanaotuwakilisha ni chanzo cha kuwa na vibaraka sio tuu wa kuacha serikali ifanye inavyotaka,lakini kuwa muhuriwa mambo ambayo hayana maslahi kwa nchi yetu au yanayotuumiza wananchi mathalani mikataba mibovu ya kimataifa na kitaifa

Wanakuwa ni wahalalishaji wa mambo ya hovyo wa viongozi wapumbavu wanaoweka maslahi yao mbele badala ya taifa

Ni kweli wako vijana ambao hao watawala wameshawaharibu akili kwa makusudi,wanafikiria kwa turbo,hao tusiwatusi ni victims of the circumstance

Kuna logic ipi ya kumlipa mbunge pesa yote hiyo kwa miaka mitano tuu?

Kwa mwezi mbunge anakusanya mpaka mil.22,hii inalipa madaktari wangapi ngazi ya degree na kuna hospitali ngapi na vituo vya afya tunalalamika hatuwezi kupeleka watumishi mpaka USAID watusaidie?Trump abarikiwe popote alipo

Walimu wengi madai yao hayazidi hata mil 2...wengine wamezunguka na bahasa mpaka wamekufa na pesa zao zimeliwa

Hao hao watu wanakuja wanawaambia wao ni watetezi wenu,wawakilishi wenu,hivi tuna akili timamu kweli?

Acha niishie hapa
Mie naona hatuna akili timamu mkuu. Kuanza kwenye msoto wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura mpk kwenda kupiga kura yenyewe ya kuchagua watu wa kutudhulumu maisha yetu yote...
Lkn sasa nini kifanyike, kukaa na kusikitika tu inatosha!?
 
Serious mkuu unajua gharama za kuupata ubunge na maisha ya kibunge?
Mifumo mibaya ya serikali...ubunge uba nini special kutengewa fedha zote hizo
Mie naona hatuna akili timamu mkuu. Kuanza kwenye msoto wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura mpk kwenda kupiga kura yenyewe ya kuchagua watu wa kutudhulumu maisha yetu yote...
Lkn sasa nini kifanyike, kukaa na kusikitika tu inatosha!?
Hapana.

Tukatae hii mifumo inayohalalisha upigaji wao...kama chaguzi hizi za maigizo
 
Serious mkuu unajua gharama za kuupata ubunge na maisha ya kibunge?
Gharama za kupata kitu chochote halali chenye manufaa kwa jamii husika ni jambo jema...lah inapo maanisha kinyume chake,ni upumbavu...ndiposa akina Trump hutukejeli kuwa sisi tumefanana tuu na binadamu lakini sisi sio binadamu
 
Je unajua Trump ametumia gharama kiasi gani kuupata urais?

Tena watunga sera na Sheria na wakilishi wa wananchi wanastahili maslahi Bora ili wasitumike kijasusi na mataifa mengine.

Hoja nahisi ilitakiwa ijikite ni namna gani tutaongeza maslahi ya watumishi wengine
 
Sijsikia viongozi wa upinzani wakiliongelea hili kwa nguvu,wala fisiemu

Marupurupu kuwa makubwa yasio akisi hali ya wanaotuwakilisha ni chanzo cha kuwa na vibaraka sio tuu wa kuacha serikali ifanye inavyotaka,lakini kuwa muhuriwa mambo ambayo hayana maslahi kwa nchi yetu au yanayotuumiza wananchi mathalani mikataba mibovu ya kimataifa na kitaifa
Aliliongelea Zitto wakamzodoa
 
Je unajua Trump ametumia gharama kiasi gani kuupata urais?

Tena watunga sera na Sheria na wakilishi wa wananchi wanastahili maslahi Bora ili wasitumike kijasusi na mataifa mengine.

Hoja nahisi ilitakiwa ijikite ni namna gani tutaongeza maslahi ya watumishi wengine
Kama hoja ni kulinda uaminifu katika utumishi,mbona kuna kada nyeti kama za afya au ulinzi nazo mishahara ni mibovu?

Tunaangalia hiyo keki tunagawanaje,sio suala la kuwaboreshea wengine ...kutoka wapi...?
 
Ndo maana nmekwambia ilitakiwa kulilia maslahi Kwa kada nyingine na sio kulalamika kwanini wengine wanalipwa vizuri
 
Mimi nashangaaga sana watu wanapigana au kushupaza shingo kwa wanasiasa, haijalishi awe wa upinzani au tawala. Hakuna mwanasiasa duniani yupo kwa ajili ya wananchi.
Hakuna, narudia tena HAKUNA. Kila mwanasiasa yupo kwa maslai yake. Uongo wa kusema wapo kutuwakilisha na kusemea shida zetu haupo. Ndio maana hata huwezi kukuta katoa hata mia yake ya mshahara agawane na aliowawakilisha kujengea hata shimo la choo.
Ndio maana wapo tayari kuua, kuumiza wengine ili waendelee kujinufaisha kwa mgongo wa kutuwakilisha.
 
Back
Top Bottom