Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Baada Agosti 27, 2024 mahakama kutoa hukumu ya kesi tukio kuuawa kwa Milembe Maunga, na watuhumiwa watatu kukutwa na hatia, wakihukumiwa kunyongwa, kwa sasa napata fursa ya kulielezea tukio hilo kwa kina namna lilivyokuwa.
Yatakuwa maelezo marefu kidogo, ila nitajitahidi kulielezea lote kwa awamu hadi nifikie mwisho. Hivyo, nitakuwa nikiendelea kwenye eneo la maoni.
Naanza...
Mauaji ya Siri: Mapenzi, Wivu, na Kifo
USIKU ulikuwa umetulia sana huko Mwatulole, wilaya ya Geita, mnamo Aprili 25, 2023.
Milembe Suleiman Hungwe alikuwa amepanga mipango ya siku inayofuata, lakini hakujua kwamba huo ulikuwa usiku wake wa mwisho duniani.
Akilini mwake, hakukuwa na wasiwasi wowote. Kila kitu kilionekana kikiwa kawaida, lakini nyuma ya pazia, jambo kubwa lilikuwa linapangwa dhidi yake.
Ndani ya kuta za nyumba isiyoisha kujengwa, yaani pagale, iliyomilikiwa na Milembe, palikuwa na siri nzito. Siri iliyogubikwa na wivu wa kimapenzi.
Twende pamoja
Milembe, ni mwanamama imara aliyefanikiwa sana kazini kwake, nyuma ya maisha yake ya siri kulikuwa na jambo moja alilolificha kwa uangalifu mkubwa—uhusiano wake wa kimapenzi.
Milembe na Dayfath Suleiman Maunga hawakuwa tu marafiki wa kawaida. Kwa muda mrefu, walikuwa wapenzi wa jinsia moja (lesbian), uhusiano ambao waliishi nao kwa siri kubwa.
Katika jamii yao, uhusiano kama huo ulikuwa kinyume katika mila na desturi, jambo lililowalazimu kuficha hisia zao.
Dayfath alikuja kwenye maisha ya Milembe kwa njia ya kawaida—alianza kama mfanyakazi wake katika biashara ya duka la vipodozi la Milembe.
Lakini muda ulivyopita, hisia za kimapenzi zilianza kuchanua kati yao. Wakianza kuishi kinyumba maeneo ya Usagara, Mwanza, wakiishi na mama yake Milembe, msaidizi wa kazi za nyumbani, na baadhi ya ndugu.
Ulimwengu wao ulikuwa ni wa siri sana, lakini ni ulimwengu ambao siku moja binti wa Milembe, Grace Evarist Gervas, aligundua kitu kuhusu mama yake na Dayfath ambacho kilimshangaza sana.
Itaendelea...
Ova