Sehemu ya Nne;
Ndoa ya Siri yawa Shimo la Kifo
Maisha ya Milembe na Dayfath yalikuwa ni mafumbo. Uhusiano wao ulikuwa umevunjika, lakini hisia zilitawala zaidi.
Upendo wa Dayfath kwa Milembe ulibadilika kuwa wivu usio na mipaka. Alianza kuhisi kuwa Milembe anamwacha, akihofia kuwa alikuwa akipoteza nafasi yake.
Lakini badala ya kuachilia, alichukua uamuzi mgumu—wa kutafuta njia ya kumtoa Milembe kwenye maisha yake, kwa njia ya giza na kifo.
Baada ya majibizano na wivu uliokomaa, Dayfath alizungumza na Safari Lubingo, rafiki yake wa zamani, na wakapanga kutafuta wauaji.
Safari akampata Genja na Mussa—watu waliokuwa na mikono ya damu. Walipanga na kuamua kuwa siku ya tarehe 25 Aprili, 2023 ingekuwa ndiyo mwisho wa Milembe.
Baada ya kufika kwenye "site", Milembe aliagana na wanaume hao watatu; Genja, Mussa, na Safari, wakiwa wamejiandaa kwa kazi yao ya mwisho.
"Nitawaita baadaye, baada ya kumaliza mazungumzo." Milembe alisema, akiwa na matumaini kwamba kila kitu kitatendeka kama kawaida.
Lakini, asilokuwa akilijua, tayari mawimbi ya hatari yalikuwa yameanza kupiga chini ya maji, yasiyoonekana.
Muda ulipofika, Milembe aliwapigia simu. Wakajitokeza kwa kasi na kuingia kwenye eneo la ujenzi. Na ghafla kitu cha ajabu kikatokea.
Itaendelea...
🙂🙂🙂🙂🙂