Milembe Alivyouawa Kwenye Pagale

Milembe Alivyouawa Kwenye Pagale

Uandishi bora kabisa huu, story Ina mpangilio mzuri sana hakuna makosa ya mkato wala nukta wala nini.

Umeandika kisomi, wengi wanapaswa kuweka story zao kwenye uandishi kama huu.

Swali: huyu dada alikuwaga na uhusiano na binti fulani mdogo wake aliyekua waziri shonza na zile video zao wakipeana utamu zilitrend sana. Je ilikua ni kabla au baada ya huyo dayfath?
 
Habari hii ni ya Ukweli au ni kisa cha kutunga ili kuwatoa Watu kwenye reli?
Ni kweli kwamba hiyo ndiyo sababu iliyopelekea mauaji ya huyo mtu au wewe umetumwa ili kuwapoteza Watu maboya?? Just a spining propaganda?
Umenikumbusha issues ya piddy. Tisii ya mchongo walishusha pumzu KESI ya kibao
 
Baada Agosti 27, 2024 mahakama kutoa hukumu ya kesi tukio kuuawa kwa Milembe Maunga, na watuhumiwa watatu kukutwa na hatia, wakihukumiwa kunyongwa, kwa sasa napata fursa ya kulielezea tukio hilo kwa kina namna lilivyokuwa.

Yatakuwa maelezo marefu kidogo, ila nitajitahidi kulielezea lote kwa awamu hadi nifikie mwisho. Hivyo, nitakuwa nikiendelea kwenye eneo la maoni.

Naanza...

Mauaji ya Siri: Mapenzi, Wivu, na Kifo

USIKU ulikuwa umetulia sana huko Mwatulole, wilaya ya Geita, mnamo Aprili 25, 2023.

Milembe Suleiman Hungwe alikuwa amepanga mipango ya siku inayofuata, lakini hakujua kwamba huo ulikuwa usiku wake wa mwisho duniani.

Akilini mwake, hakukuwa na wasiwasi wowote. Kila kitu kilionekana kikiwa kawaida, lakini nyuma ya pazia, jambo kubwa lilikuwa linapangwa dhidi yake.

Ndani ya kuta za nyumba isiyoisha kujengwa, yaani pagale, iliyomilikiwa na Milembe, palikuwa na siri nzito. Siri iliyogubikwa na wivu wa kimapenzi.

Twende pamoja
Milembe, ni mwanamama imara aliyefanikiwa sana kazini kwake, nyuma ya maisha yake ya siri kulikuwa na jambo moja alilolificha kwa uangalifu mkubwa—uhusiano wake wa kimapenzi.

Milembe na Dayfath Suleiman Maunga hawakuwa tu marafiki wa kawaida. Kwa muda mrefu, walikuwa wapenzi wa jinsia moja (lesbian), uhusiano ambao waliishi nao kwa siri kubwa.

Katika jamii yao, uhusiano kama huo ulikuwa kinyume katika mila na desturi, jambo lililowalazimu kuficha hisia zao.

Dayfath alikuja kwenye maisha ya Milembe kwa njia ya kawaida—alianza kama mfanyakazi wake katika biashara ya duka la vipodozi la Milembe.

Lakini muda ulivyopita, hisia za kimapenzi zilianza kuchanua kati yao. Wakianza kuishi kinyumba maeneo ya Usagara, Mwanza, wakiishi na mama yake Milembe, msaidizi wa kazi za nyumbani, na baadhi ya ndugu.

Ulimwengu wao ulikuwa ni wa siri sana, lakini ni ulimwengu ambao siku moja binti wa Milembe, Grace Evarist Gervas, aligundua kitu kuhusu mama yake na Dayfath ambacho kilimshangaza sana.

Itaendelea...

Ova

Usitutake kusogelea telegram tu.
 
Ko ulijua utaondoka hujaacha mkwanja....ulinipendea uchafu? Toa sadaka nikapendeze tena unipende na kesho🤒
Hahaha...................Tena Siku hizi bei ya kusuka nywele imepanda, bila 50k Bibie hajasuka 🙌

Bora Bibi zenu Mwaka 47 walikuwa wanasuka twende kilioni tu, Mwanaume unatoa shilingi 150 tu Kwa Msusi kumpendezesha Mkeo
 
Huwa nashangaa sana anayeshiriki deal ya kuua, kwa nini afanye hivyo wakati hakuna namna ambavyo hatajulikana na kudakwa. Sijui unakuwa umepewa kiasi gani mpaka kurisk maisha yako
Si ndo hapo Mtu anaanza kutanga tanga na kutokula kuku kitaa na totozi anaenda kuishia Jela.
Ni basi tu watu roho za kishetani zinakua zimewavaa hakuna namna wanaweza kujiokoa.
 
Back
Top Bottom