Tetesi: Milestone International Co. Ltd iliyolipwa Milioni 866.6 ni kampuni ya Mbowe inayosimamiwa na shemejiye Kineneko Mtei

Tetesi: Milestone International Co. Ltd iliyolipwa Milioni 866.6 ni kampuni ya Mbowe inayosimamiwa na shemejiye Kineneko Mtei

Status
Not open for further replies.
Hauna maana kabisa..
*ukisema eti ’kodi tanzania’ unamaanisha kuwa makusanyo ya mapato yanapelekwa Chadema?Nini uhusiano wa mapato kusanywa(kodi) na Chadema wewe?
*Hiyo ni miradi yao binafsi na si Fedha za ‘ruzuku ya vyama’ kama inavyotazamwa hapa...siyo kama “chama cha kijani” kinachotegemea vijisenti na wahisani kujiendesha..
Ruzuku za CDM ni pesa za walipakodi kachotewa Kineneko Mtei.
 
Naona mmekuja na single ya kufukia ulaji wa hela za wastaafu na chama chao kitukufu. Pia hamtaki kusema ukweli kwamba nchi haikopesheki tena, mkulu ndani ya mwaka mmoja wa fedha ameongeza deni la taifa kwa 12%? Je akikaa miaka mitano hatutauzwa?
 
Si vyema kupambana na ccm chama hovyo na huku tunafanya mambo yanayofanana na ccm.

Wahusika wajitathimini.
Kwanza naomba kwa heshima na taadhima, admin msiunganishe uzi huu na mwingine.

Ndugu wanajukwaa, kama wote tupendavyo, juhudi za kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya kodi za watanzania ni endelevu na popote pesa hizo zinapokwenda sisi watozwa kodi lazima tuhoji.

Nimeona uzi huku ndani
Hivi ndivyo Freeman Mbowe na genge lake anavyotafuna pesa za CHADEMA!

unaozungumzia ripoti ya CAG kwa mwaka 2016/17ambayo pamoja na mambo mengine inazungumzia pesa zilizolipwa M/S Milestone International Co. Ltd kiasi cha 866,600,000. Kumbuka malipo haya ni kwa mwaka mmoja wa 2016, hatujui miaka mingine ya nyuma, na 2017 na 2018.

Nilichotaka kuonyesha ni kuwa kampuni hii mmiliki wake ni Freeman Mbowe, na Managing Director ni Shemeji yake wa kike aitwaye, Kineneko Mtei mdogo wake Dr. Lilian Mtei, mke wa ndoa wa Freeman Mbowe.

Kwanza hapa kuna mgongano wa maslahi na harufu ya rushwa, haya machache ni kwa mujibu wa ripoti ya msajiri pale penye mashaka, kwa kweli CHADEMA kuna ufisadi, otherwise wangeweka wazi ripoti yao ya fedha wazi tuone matumizi yao kwa ujumla na wanaofaidika na kulipwa pesa hizo.
 
Kwa hiyo huyu shemeji wa Mbowe hana uwezo wa kufungua Kampuni au kila mtu ambae ndg yake au shemeji yake anafanya siasa basi huyo mtu hatakiwa kabisa kufanya Biashara mana mtasema ni za huyu ndugu.

Hivi hii nchi mbona ina watu wapuuzi namna hii?? Mtei alikua Gavana kweli alishindwa kusomesha mtoto aweze kufungua Biashara kweli?? Tumieni akili kuwaza kusaidia nchi mnawaza upuuzi tuuuuu
Jina (Kineneko Mtei) tu limembeba kufanya biashara na chama cha baba na shemeji yake. Hapo kuna Conflict of interest mkuu,toa vibanzi usoni kama tunataka kurekebisha makando kando toa uchama.

Hii kwa nchi zilizoendelea bonge la SKENDO tungesikia Mwenyekiti anajiuzuru kwa kulinda heshima ila kwa vile tupo kwenye nchi za ufia chama kwanza wananchi baadae basi tuhalalishe tu kwa vile CCM wanafanya.
 
Subiri uone watakavyomtetea Mbowe. CHADEMA kama sikio la kufa, hawajiulizi ni kwanini chama kimekuwa katika madeni yasiyoisha wakati hata ofisi hakuna. Kuwa na deni siyo dhambi ila madeni ya CHADEMA fedha zinaenda wapi? Ofisi hakuna, kila siku wanachangishana kulipia nini sijui? Na hapo hujataja zile fusso chakavu walizouziwa.
Ndio vile vile mnavyo tetea ujinga wa kujizulu na kugombea tena,huku mabilion ya pesa yakiteketea.
 
Subiri uone watakavyomtetea Mbowe. CHADEMA kama sikio la kufa, hawajiulizi ni kwanini chama kimekuwa katika madeni yasiyoisha wakati hata ofisi hakuna. Kuwa na deni siyo dhambi ila madeni ya CHADEMA fedha zinaenda wapi? Ofisi hakuna, kila siku wanachangishana kulipia nini sijui? Na hapo hujataja zile fusso chakavu walizouziwa.
Majitu mengine sijui akili ziko sehemu gani?
ATCL nayo anaiongoza Mbowe?
Mbona inanuka madeni?
Serikali nayo inadaiwa zaidi ya tshs.trilion 40 hamlioni hilo mnakesha na hela ya mboga hiyo!
 
Kila mtu anakula kwenye office yake au wewe ulitakaje labda
 
Subiri uone watakavyomtetea Mbowe. CHADEMA kama sikio la kufa, hawajiulizi ni kwanini chama kimekuwa katika madeni yasiyoisha wakati hata ofisi hakuna. Kuwa na deni siyo dhambi ila madeni ya CHADEMA fedha zinaenda wapi? Ofisi hakuna, kila siku wanachangishana kulipia nini sijui? Na hapo hujataja zile fusso chakavu walizouziwa.
Bila kusahau walitaka kuwaingiza raia choo cha kike kwa mtaji wa michango na matibabu ya TL! Mchaga noma! Jamaa hatari sana huyu, bado tetesi ya kuuza chama kwa mzee EL, bado fedha zinavyotoka na kutumika bila rekodi, ila jamaa kawapata kweli, sishangai hawamuondoi, chama ni chake, binafsi, cha familia, atakayepiga kelele asishangae yatakayomkuta, rekodi zipo kwa waliofanyiwa unyama..
 
Majitu mengine sijui akili ziko sehemu gani?
ATCL nayo anaiongoza Mbowe?
Mbona inanuka madeni?
Serikali nayo inadaiwa zaidi ya tshs.trilion 40 hamlioni hilo mnakesha na hela ya mboga hiyo!
Kwaiyo mmeamua kujichotea mapema na nyinyi?

Umeeleweka mkuu.
 
Ruzuku za CDM ni pesa za walipakodi kachotewa Kineneko Mtei.
Mkuu,hapa ndipo tofauti ya fikra nyeusi na nyeupe inapotokea..
*mtanzania gani/shirika lipi leo lisilojua na kutekeleza sheria ya usimamizi wa matumizi ya kiserikali ambayo inawataka kuwasiliaha ‘ripoti iliyokaguliwa’ juu ya fungu la fedha husika ilioyengewa..!
*iweje leo,mnasema “Kaneneko mtei” kala fedha...nini ‘thamani ya Chadema na uhusiano wa watajwa,fedha za ruzuku na serikali’...lets be good,tusiwatakie wenzetu mabaya tu kila siku
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom