Milion 10 inatosha kuanzisha biashara ya Baa?

Unatatizo kichwani yaani mimi nianza kuandika template hapa km unataka naweza kukukuandikia dodoso ili ufanye utafiti, mimi ni muelimishaji elimu ya ujasiriamali na nimebobea kwenye eneo Hilo hata hiyo biashara nimewahi kufanya
Onyesha kwa kutumia numbers, utaanzishaje biashara ya bar kwa mtaji wa milioni 10.
Mimi pia naweza nikasema I'm so and so but that doesn't mean s#!t.
Numbers hommie, numbers ....
 
Mkuu
Mkuu wa wakuu Benny Haraba tafadhali usichanganye sana hiyo lugha nyingine wenzio hatuelewi tuko hapa kukufuatilia pia Kaka yangu
 
Onyesha kwa kutumia numbers, utaanzishaje biashara ya bar kwa mtaji wa milioni 10.
Mimi pia naweza nikasema I'm so and so but that doesn't mean s#!t.
Numbers hommie, numbers ....
Narudia mpanga wa biashara unafaniyiwa utafiti kulingana na eneo husika vs ushindani uliopo na aina ya wateja , ( social demographics variables) aina ya watu wanao izunguka biashara Yako, elimu zao, shughuli za vyote hivyo huchagiza baisha Yako mfano wagonga mawe, waendesha bodaboda, vyuo km vipo, wafanya biashara mbalimbali
 
Mkuu

Mkuu wa wakuu Benny Haraba tafadhali usichanganye sana hiyo lugha nyingine wenzio hatuelewi tuko hapa kukufuatilia pia Kaka yangu
Sawa nimekuelewa, and sorry for my over reactions I also know that ,here we have different level of understanding, (interpretation) humu kuna wadau wenye uwezo tofauti wa kutafsiri mambo ama maandiko
 
wewe uliyesema mil 10 haitoshi ndo ulitakiwa utoe mchanganuo wa biashara ya bar ili tuamini maneno yako.
 
ni kweli Dar umafia mwingi nataka nikaifanye hiyo biashara mkoa wa pwani, mziki mkubwa heavy duty na size ya kati bei gani?
 
Mkuu uko sahihi. Lakini hapa unaweza kutukanwa ukisema hivi. Jinsi alivyouliza tu tayari kuna possibility kubwa ya kufeli kama atafanya. Kwa nini? Hajazingatia uliyomwambia.
 
Ushauri mzuri lakini sio hitaji la jamaa na inawezekana ashayafanya hayo yote.. Anachotaka kujua ni kama milioni 10 aliyonayo inaweza kutosha.
 
maneno machache ila umempa ushauri wa maana sana aanzie hapa "anza kidogo" .....infact ni biashara hujawai fanya
 
bar ni jiko mkuu, utundu wa mtu wa jikoni ni hirizi tosha. mziki inategemea aina ya wateja walioko hilo eneo, kama ni watu wazima sana hawapendi makelele. level ya uchumi wa wateja wako pia inaamua uweke vinywaji vya aina gani na status gani.
 
10m kwa bar usijaribu, ndogo sana ,,, pengine unaweza kodi frem sehemu ambayo kuna kaeneo flani kwa mbele,,, then hio frem jenga kikaunta cha kishkaji, kwa nje weka tent lenye kukaa meza kama 4 na viti vyake,,, alafu hapo ndani kaunta zikae walau meza 2, nunua sub woofer , nunua TV 2 size kati tu weka ndani na nje, nunua fridge moja isiyo ya kampuni ili uweze kuweka vinywaji vyote bila bughudha,,, jenga kakibanda ka chips na mishikaki pembeni,,,, anza na bia kreti 20, soda 5, maji katon 5, pombe kali pc kadhaa kadhaa tu ,,, tafuta dada mmoja wa nje na kaunta mmoja anza mdogo mdogo "
 
bar ni jiko mkuu, utundu wa mtu wa jikoni ni hirizi tosha. mziki inategemea aina ya wateja walioko hilo eneo, kama ni watu wazima sana hawapendi makelele. level ya uchumi wa wateja wako pia inaamua uweke vinywaji vya aina gani na status gani.
vip kuhusu wahudumu wanawake wazuri wazuri wenye mvuto!
 
kuliko kunishusha ni bora ukatoa ushauri kulingana na matakwa yangu, ulipaswa kusema ongeza mil 5 au 10 ingine au fanya ivi na vile ili utimize lengo ivyo ulivyosema ni bora niache na kuacha siwezi vile nimeamua mpango utimie.
 
Mkuu uko sahihi. Lakini hapa unaweza kutukanwa ukisema hivi. Jinsi alivyouliza tu tayari kuna possibility kubwa ya kufeli kama atafanya. Kwa nini? Hajazingatia uliyomwambia.
theory nyingi sana! sina uzoefu na bar ila nina uzoefu wa biashara zingine iyo ni tofauti na mtu ambaye hajawai fanya biashara kabisa.
 
10m kwa bar usijaribu, ndogo sana ,,, pengine unaweza kodi frem
kuliko kunishusha ni bora ukatoa ushauri kulingana na matakwa yangu
Samahani, unaonekana una kiburi na dharau na unapenda kubishana na hutaki ushauri!

Tuanzie hapa kwenye mziki 'heavy duty', hapa nilivyokuelewa unataka disco kwa kifupi unataka wenye bar wengine waufyate!

Chukua hiyo milioni kumi nenda nayo pale congo (Kariakoo) ulizia full package ya disco sound bei ya chini ni kiasi gani! Kitachobaki kafungulie bar!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…