DOKEZO Milioni 100 alizotoa Makonda, ni za kwake, Serikali au za Nani? TAKUKURU mna jibu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Awamu ya tano ambayo kiongozi wake anasema haoni sababu ya kuondoka kwani Barbara hazitajengwa, ndege hazitanunuliwa wala SGR haitajengwa.
Na wapo wehu badala ya kuzomea wanashangilia
 
Hela za umma zina kanuni zake za matumizi. Ninaposikia mambo yanayowapata wanaotumia vibaya hela za umma, hasa wakati wa Ziara za Rais na Waziri Mkuu, nashindwa kuelewa watumishi wa serikali wenye tabia hizo wanafikiri nini?
Hakuna kwenye immune kama atavunja sheria. Tanzania inabadilika. Haya tunayoanza kuona ni dalili kwamba hela za serikali sio tena ziendelee kuchukuliwa kama hela za bure.
I hope everybody knows that, including people in Dar Es Salaam
 
Fedha zinatolewa na wafanyabiashara wanamkabidhi Makonda Ili wapate upendeleo Kama kukwepa kodi,kukwepa Sheria nk.
Kama zamani tu Ila zamani walikuwa wanamkabidhi mfalme sasa hivi wanamkabidhi mtoto wa mfalme.

Mfanya biashara gani anayetoa hizo hela? Kwanini ampe hizo hela? Hiyo ni rushwa
 
Mshahawa wake bei gani? Amefanya kazi miaka mangapi? Juzi Juzi tu alikuwa anasomeshwa na wasamalia wema, leo hii eti kawa doni...nchi hii inaliwa saana.

Hapa ndipo nazidi kumwelewa Lissu.
 
Usiamishe magoli, wapi kasema ni zake au sio zake?
Yaani kila kitu unataka kutetea!! Sasa kama si zake, ina maana unataka kusema yeye ni mjumbe tu!! Kama ndivyo, huyo aliyempa kutoa "kwa niaba yake" ni kwanini asizitoe mwenyewe na kwa uwazi na badala yake anamtumia Makonda kwa siri?
 
Alishasema wanaompa Ni wadau wa maendeleo na wanaomuunga mkono katika jitihada zake za kuijenga dar mpya.

Rejea maelezo yake alipompa Juma Kaseja m10.
Kwahiyo akisema tu kwamba anapewa na wadau wa maendeleo, tayari ndo ishakuwa kauli inayopaswa kuchukuliwa uzito?!
 
Mkuu ni kweli 100 au umesahau ni 10 ukaongeza hapo 0
 
Anapata pesa kwa wafadhili, kwa makubaliano ya kutowataja au kuwaweka wazi...


Cc: mahondaw
 
Ma deal yote kwasasa yapo chini ya Daudi.
Sembe aliyokuwa akipigapiga kelele ilikuwa nikutafuta Monopoly on the hand.Upigaji,dhuluma na utapeli vyote chini ya Daudi.Mbaya Baba Daudi anafahamu na yawezekana kuna baraka kutoka kwake.

Pole sana ndugu yangu Quality Manjy,Pole sana G.S.Mohammed. Pole sana Metle.Poleni sana wapigaji wote tuliopigwa pini AWAMU hii.
 
Umeonyesha uko kumpinga Makonda basically sababu waijua mwenyewe. Wewe mwenyewe unasema hajasema pesa ni zake au laa ila umeamua kuhitimisha kuwa ni zake kisa hajasema ni zake au laa ili tu ujenge msingi wa hoja yako dhaifu.
Ni mtumishi wa serikali na analipa kodi (PAYE) kwenye mshahara wake, TRA inauwezo wa kufumbua kitendawili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…