Milioni 150 Rais Samia kaipata wapi?

Milioni 150 Rais Samia kaipata wapi?

Ukiwa rais wa JMT si unajichotea tu mifweza
Mahali popote..t3na hyo mln 150 mbn ndogo sana angegawa mabilion kwa mabilion

Ova
 
Naona picha ya Mbowe hapo, sasa Mbowe anahusikaje na hiyo m 150 ya rais?
Ni kanisa la nyumbani kwa Mbowe na yeye amekuwa mbele kwenye kutafuta uchangiaji. Unadhani ametoa hizo fedha kwa bahati mbaya? Nimesoma comments za watu hapa na inaonyesha Tanzania wananchi wengi uelewa wetu ni mdogo sana. 1. Rais hana kisima cha fedha na hii inaonyesha katiba yetu ilivyo mbovu. 2. Wengi wanadhani mwanzisha thread hataki makanisa yachangiwe kumbe anaona mbali zaidi. 3. Mbowe ni kiongozi wa upinzani na hizi fedha zinaweza kuchukuliwa kama ni hongo
 
Halafu baada ya kuhoji kuna mabadiliko yoyote?
Hii nchi ukishakuwa top ww ni mfalme
Kuhoji ni lazima. Mabadiliko yanaanza kwa kuhoji. Ukiridhika na kusema etu mtu akishakuwa top ni sawa na mfalme inaonyesha mtu aliyekata tamaa na hajui afanye nini kuleta mabadiliko. Huu ufalme wa rais unaiangamaza nchi na ni jukumu letu sote kuhoji na kuleta mabadiliko. Hilo kanisa ni kanisa la nyumbani kwa Mbowe na hizo fedha hazijapelekwa kwa bahati mbaya.
 
Kwani yeye hawezi kuwa nazo akatoa kutoka mfukoni mwake,,?
Hawezi kuwa nazo (kihalali). Rais anafanya biashara gani? Unacheza na sh milioni 150? Na hata kama amechangiwa na marafiki, hao wachangaji wanategemea kupata nini kama reward? Rais wa nchi mi mtu anayestahili kuishi akiwa clean. Vyanzo vyake vya mapato na zawadi ni lazima vijulikane ili kuondoa uwezekano wa rais kushawishiwa kutenda fadhila kwa baadhi ya watu.
 
We Raisi unamchukulia ni kama mjomba wako anaekula Methadone kwa foleni pale Temeke hospitali au?
 
Hizi pesa zote Mil.150 Rais kapatia wapi za kugawa hovyo ?
View attachment 2858754

Moja ya kazi ya Rais wa JMT ni kusaidia kusambaza dini ?
Kwamba ni jambo baya sana amefanya?? kwamba amefanya jambo la kuvunja amani?
Mbona kama vile ni wivu kama siyo chuki binafsi?

akishakuwa Rais harahisiwi kufanya tena jambo zuri la kijamii na lenye kumfurahisha yeye nafsi??

Na kwa kama utauliza kwamba anapata wapi hiyo pesa je kazi anayofanya haimpi kipato? na je wewe unafahamu kipato chake na hata akiba yake??

Ningeshauri tuyaangalie mambo yenye msingi na ambayo yatalisaidia taifa na siuo jambo la mshangao kwa Rais wa nchi kutoa 150 mln kuisaidia taasisi ya watu weengi na tena taasisi iliyopo ndani ya nchi anayoiongoza.
 
Hizi pesa zote Mil.150 Rais kapatia wapi za kugawa hovyo ?
View attachment 2858754

Moja ya kazi ya Rais wa JMT ni kusaidia kusambaza dini ?
Rais yoyote ana fungu la kuchangia ustawi wa jamii kama vile vituo vya yatima nk, kwenye dini ni taasisi muhimu kwa utulivu na amani ya nchi, hata Magufuli alichangia hadi misikiti dhana kuu ni nyumba za ibada hurahisisha serikali kutawala amani ikiwepo
 
akipeleka msikitini mdini, akipeleka kanisani katoa wapi
 
Hizi pesa zote Mil.150 Rais kapatia wapi za kugawa hovyo ?
View attachment 2858754

Moja ya kazi ya Rais wa JMT ni kusaidia kusambaza dini?
===
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 150 kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT la Bethel Usharika wa Nshara Machame Mkoani Kilimanjaro anakosali Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Akizungumza leo katika ibada ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo, Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye husali katika Kanisa hilo awapo nyumbani Machame amesema alishirikisha Watu mbalimbali kuhusu kuchangia ambapo miongoni mwao ni Rais Samia.
Hapo mlevi mbowe kimyaaa
 
Samia siyo maskini km mamako. Umeona hiyo hela ni nyingi? Tena kwa mtu km rais? Umaskini ni mbaya sana, pambana bwanamdogo upunguze huo ufukara wako maana umeingia mpaka kwenye ubongo
 
Kwani rais mshahara wake ni sh ngapi.
Alafu tambua kwa kawaida hasa Africa mwanamke mshahara wake hauna hasa akiwa ni mke wa mtu.

Mume ndio anahusika na gharama za maisha ya familia.

So mama pesayake anaweza kutumia vyovyote atakavyo.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Mbona mnaongea pumba sana, ofisi ya raisi ikulu wana budget yao na hii ni miongoni kwa kazi zake na haikaguliwi na CAG
 
Back
Top Bottom