Milioni 200 inatosha nyumba na magari mawili?

Milioni 200 inatosha nyumba na magari mawili?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Hajawahi kumiliki nyumba wala gari lake binafsi. Kwa zaidi ya miaka kumi aliyokuwa kwenye ajira alikuwa akiishi na kutumia gari la taasisi.

Sasa anataka kuachana na ajira ili asimamie kwa karibu miradi yake. Ametenga milioni 200 kwa ajili ya nyumba na magari mawili.

Anataka magari mawili kwa sababu miradi yake itamuhitaji kusafri mara kwa mara hivyo anataka gari moja la masafa marefu na gari dogo kwa mizunguko ya mjini.

Ushauri wangu kwake:
1. Atenge milioni tatu kwa ajili ya pango la nyumba kwa miezi sita. Katika kipindi hicho cha miezi sita ahakikishe nyumba yake inakamilika.

Yeye alitaka kuinunua iliyokwishajengwa (kuna inayouzwa milioni tisini) lakini nimemshauri kuwa ya kujenga mwenyewe ni bora zaidi hasa ikizingatiwa kuwa atakapoacha kazi atakuwa na muda mzuri wa kuisimamia kwa karibu.

2(A). Anunue gari dogo (sedan) lisilozidi mililioni thelathini: AUDI, BENZ, BMW, n.k. Akikosa ya bei hiyo show room atafute kwa watu binafsi.

2(B). Anunue gari la masafa marefu lisilozidi milioni sabini. Mashaka yangu ni uwezekano wa kupata gari bora nchini kwa hiyo bajeti, hasa ikizingatiwa kuwa gari lake pendwa la masafa marefu ni LAND CRUISER PICK UP! Lakini sina uhakika kama ataweza kupata "zima" kwa bei hiyo.

Ingelikuwa ni wewe ungemshaurije?
 
Hajawahi kumiliki nyumba wala gari lake binafsi. Kwa zaidi ya miaka kumi aliyokuwa kwenye ajira alikuwa akiishi na kutumia gari la taasisi.

Sasa anataka kuachana na ajira ili asimamie kwa karibu miradi yake. Ametenga milioni 200 kwa ajili ya nyumba na magari mawili.

Anataka magari mawili kwa sababu miradi yake itamuhitaji kusafri mara kwa mara hivyo anataka gari moja la masafa marefu na gari dogo kwa mizunguko ya mjini.

Ushauri wangu kwake:
1. Atenge milioni tatu kwa ajili ya pango la nyumba kwa miezi sita. Katika kipindi hicho cha miezi sita ahakikishe nyumba yake inakamilika.

Yeye alitaka kuinunua iliyokwishajengwa (kuna inayouzwa milioni tisini) lakini nimemshauri kuwa ya kujenga mwenyewe ni bora zaidi hasa ikizingatiwa kuwa atakapoacha kazi atakuwa na muda mzuri wa kuisimamia kwa karibu.

2(A). Anunue gari dogo (saloon) lisilozidi mililioni thelathini: AUDI, BENZ, BMW, n.k. Akikosa ya bei hiyo show room atafute kwa watu binafsi.

2(B). Anunue gari la masafa marefu lisilozidi milioni sabini. Mashaka yangu ni uwezekano wa kupata gari bora nchini kwa hiyo bajeti, hasa ikizingatiwa kuwa gari lake pendwa la masafa marefu ni LAND CRUISER PICK UP! Lakini sina ukika kama ataweza kupata "zima" kwa bei hiyo.

Ingelikuwa ni wewe ungemshairije?
Kila kitu kinawezekana na kìla kitu kinaweza kisiwezekane.
Swali lako lingejibika kirahisi kama
Ungesema eneo atapofanyia ujenzi.
Pia masafa hayo ni ndani ya mkoa au mikoani.

Ila kwa budget hiyo anaweza kukamilisha kwa 75 asilimia ya vitu vyake.
 
Sasa anataka kuachana na ajira ili asimamie kwa karibu miradi yake. Ametenga milioni 200 kwa ajili ya nyumba na magari mawili.
Huo usimamizi wa miradi yake unahitaji kumiliki nyumba na gari mbili? Cha maana yeye asimamie miradi yake na kuwekeza pesa kwenye huo usimamizi wa miradi (sababu kama maswali haya kwake ni magumu kuyajibu huenda huo usimamizi katika miradi yake ukawa mgumu hivyo awaze mara mbili mbili kuacha ajira yake ambayo mpaka sasa ndio imempatia hizo seed money)

He knows best about his case than me and you...
 
Huo usimamizi wa miradi yake unahitaji kumiliki nyumba na gari mbili ? Cha maana yeye asimamie miradi yake na kuwekeza pesa kwenye huo usimamizi wa miradi (sababu kama maswali haya kwake ni magumu kuyajibu huenda huo usimamizi katika miradi yake ukawa mgumu hivyo awaze mara mbili mbili kuacha ajira yake ambayo mpaka sasa ndio imempatia hizo seed money)

He knows best about his case than me and you...
Gari moja ni la kazi - safari za "mashambani" na "mikoani". Gari la pili ni dogo kwa mizunguko ya mjini na safari fupi.
 
Kila kitu kinawezekana na kìla kitu kinaweza kisiwezekane.
Swali lako lingejibika kirahisi kama
Ungesema eneo atapofanyia ujenzi.
Pia masafa hayo ni ndani ya mkoa au mikoani.

Ila kwa budget hiyo anaweza kukamilisha kwa 75 asilimia ya vitu vyake.
Nyumba itajengwa Mwanza.
Shughuli zake: Njombe, Kigoma, Simiyu, kuna kusafiri kwingi.
 
Nini ameshidwa? anunue gari ya 25m gari ya 100m... milion 50 anapata kamyumba kazuri cha kuishi
Why awekeze hela nyingi hizo kwenye magari (liability) badala ya kuwekeza?!
Kwanini masafa asitumie public transport km ndege nk, hiyo hela aache kwenye mzunguko, bora hata aweke kwenye T bond, izalishe some amount, awe na gari 1 tu!

Nyumba pia inaweza kusubiri, km siyo lazima hiyo hela ya kujenga azalishe mara 2, halafu ndiyo ajenge.
 
Nini ameshidwa? anunue gari ya 25m gari ya 100m... milion 50 anapata kamyumba kazuri cha kuishi
Hajashindwa, lakini anapopata mawazo ya wengi humchangamsha ufahamu katika kufanya maamuzi sahihi. Tunatofautiana uzoefu na katika kuona mambo kutokea "angle" tofauti.
 
Why awekeze hela nyingi hizo kwenye magari (liability) badala ya kuwekeza?!
Kwanini masafa asitumie public transport km ndege nk, hiyo hela aache kwenye mzunguko, bora hata aweke kwenye T bond, izalishe some amount, awe na gari 1 tu!

Nyumba pia inaweza kusubiri, km siyo lazima hiyo hela ya kujenga azalishe mara 2, halafu ndiyo ajenge.
Ameomba ushauri kupata nyumba na gari mbili kwa bajeti ya 200m
 
Gari moja ni la kazi - safari za "mashambani" na "mikoani". Gari la pili ni dogo kwa mizunguko ya mjini na safari fupi.
Kwahio hivyo ni vitendea kazi vyake katika shughuli zake na wala havina majadala kwahio atafute vya bei nafuu na vinavyoweza kuhimili hizo kazi sababu akinunua ambacho kila siku anashinda garage au hawezi kubeba mzigo wa shamba pia itakuwa tatizo

Again he knows better na issue sio pesa tu bali anachonunua kama ni fit for purpose
 
Back
Top Bottom