Milioni 200 inatosha nyumba na magari mawili?

Milioni 200 inatosha nyumba na magari mawili?

Naiona hiyo M 200 ikiyeyuka bila jambo la maana..
Je unaacha kazi kwa kustaafu/uzee au unabadili fursa(bado kijana?)
 
Sasa mbona ana uwezo mdogo sana wa kufikiri?
Basi na amuajiri mtu hapo awe anampa ushauri. Kama ana miradi ya zaidi ya mil 500 hivi kweli hajui kuhusu nyumba na magari?
Kwani kipimo cha mtu mwenye akili ni kipi?

Inawezekana aliweza kufanikisha miradi yake kwa kuwauliza watu wengi. Kama amegundua kuwa ni kanuni inayofanua kazi, kwa nini asite kuendelea kuitumia?

Never underestimate the power of ideas! Ukiona mtu anakuuliza ushauri, usifikiri hana mawazo yake binafsi
katika hilo. Anachotafuta ni kuboresha zaidi, au, akiona wazo alilopewa ni bora zaidi, abadilishe kabisa.

Ni mfagizi asiyejua kusoma wala kuandika ndiye aliyetoa wazo la kutengeneza lifti nje ya majengo. Kabla ya hapo, lifti zote zilikuwa kwa ndani.

Maengineer hawakutarajia kuwa mfagizi anaweza kuwa na mawazo bora kuwazidi wasomi.

Ideas ni raw materials!
1. Waulize unaoamini wanajua.
2. Waulize unafikiri hawajui
3. Waulize wasiojua lakini wanaamini kuwa wanajua

4. Ukiyaweka pamoja mawazo kutoka kwao, unaweza ukapata wazo moja bora zaidi kuliko uliyokuwa nayo hapo awali.
 
Ameweza kumiliki pesa km hizo, anashindwa vipi kuzipangia majukumu yake??!!
Wewe unamshauri nini?

Labda nikuambie tu kuwa kuna watu wanamiliki utajiri wa mabilioni ya fedha lakini waoga sana kufanya mambo mapya. Wanazilinda fedha zao kwa umakini mkubwa mno. Ndiyo maana walitaka kufanya jambo wanaomba ushauri kwa watu mbalimbali. Hawataki kukosea, hasa kama hizo fedha alizisotea. Usishangae. Wapo wengi tu!
 
Hajawahi kumiliki nyumba wala gari lake binafsi. Kwa zaidi ya miaka kumi aliyokuwa kwenye ajira alikuwa akiishi na kutumia gari la taasisi.

Sasa anataka kuachana na ajira ili asimamie kwa karibu miradi yake. Ametenga milioni 200 kwa ajili ya nyumba na magari mawili.

Anataka magari mawili kwa sababu miradi yake itamuhitaji kusafri mara kwa mara hivyo anataka gari moja la masafa marefu na gari dogo kwa mizunguko ya mjini.

Ushauri wangu kwake:
1. Atenge milioni tatu kwa ajili ya pango la nyumba kwa miezi sita. Katika kipindi hicho cha miezi sita ahakikishe nyumba yake inakamilika.

Yeye alitaka kuinunua iliyokwishajengwa (kuna inayouzwa milioni tisini) lakini nimemshauri kuwa ya kujenga mwenyewe ni bora zaidi hasa ikizingatiwa kuwa atakapoacha kazi atakuwa na muda mzuri wa kuisimamia kwa karibu.

2(A). Anunue gari dogo (saloon) lisilozidi mililioni thelathini: AUDI, BENZ, BMW, n.k. Akikosa ya bei hiyo show room atafute kwa watu binafsi.

2(B). Anunue gari la masafa marefu lisilozidi milioni sabini. Mashaka yangu ni uwezekano wa kupata gari bora nchini kwa hiyo bajeti, hasa ikizingatiwa kuwa gari lake pendwa la masafa marefu ni LAND CRUISER PICK UP! Lakini sina uhakika kama ataweza kupata "zima" kwa bei hiyo.

Ingelikuwa ni wewe ungemshaurije?
Nyumba ya makazi na una pesa uisimamie mwenyewe, haiwezi kuchukua miezi zote hizo 6 bhana.

Ni miezi mitatu tu inatosha msingi hadi finishing. Miezi 6 ni matumizi mabaya ya rasilimali.

Halafu mtu anaacha kazi, magari mawili ya nini, aanze na moja,la pili ama zaidi ataongeza akishajipata huko mbele ya safari.

Ujue gharama ya matunzo na mafuta ya magari yanahitajika, siyo kuendesha tu, ni gharama.

Nyumba ya kifahari kwa mil. 70 inatosha na mil. 30 kwa gari. Izo zingine asizitapanye, aziwekeze kuendeleza plan B yake.
 
Ameweza kumiliki pesa km hizo, anashindwa vipi kuzipangia majukumu yake??!!
Mfugaji mmoja alikuwa akikaa na zaidi ya milioni mia mbili ndani, siyo benki, ni ndani ya kibanda cha nyasi. Lakini aliposhauriwa kujenga nyumba ya kisasa, haikumchukua muda aliamua kurejea kwenye nyumba yake ya nyasi kwa madai kuwa nyumba ya kisasa ilikuwa ikimsababishia mafua.

Kama huyo angekuomba ushauri, unafikiri ungemjibuje?

Hakuna anayejua kila kitu mkuu. Kwako linaweza likawa jepesi, lakini kwa mwenzio likawa gumu samat.

Kuuliza si mjinga mkuu. Hata kama unaamini unajua, kuna wanaomjua kukizidi japo unaweza ukawa unewazidi pesa.

Kuwa na hela haimaanishi unajua kuliko wengine, na kutokuwa nazo hakumaanishi ni mjinga.

Kila mtu ana kinachoweza kumfaidia mwenzake. Tunategemeana katika mambo mengi!
 
Wewe unamshauri nini?

Labda nikuambie tu kuwa kuna watu wanamiliki utajiri wa mabilioni ya fedha lakini waoga sana kufanya mambo mapya. Wanazilinda fedha zao kwa umakini mkubwa mno. Ndiyo maana walitaka kufanya jambo wanaomba ushauri kwa watu mbalimbali. Hawataki kukosea, hasa kama hizo fedha alizisotea. Usishangae. Wapo wengi tu!
Hizo pesa akiziingiza kwenye mradi au biashara na hana uzoefu lazima akubali hasara.!! Ushauri utapewa ila kuna kitu kinaitwa ”changamoto” hizo hawezi kukwepa. Huko anakoingia unahitajika uvumilivu na kujitoa lasivyo hizo pesa zote anazizika
 
Mkuu, kuna watu ukikutana nao na ukaona maisha wanayoyaishi lakini baadaye ukabahatika kuona akaunti zao hutaamini!

Kuna watu wanaoweza kufanya mambo yao kimya kimya, na siku wakiamua kuyaweka wazi ndiyo wengine hukimbilia kusema ni wezi kumbe walianza kuwekeza kimya kimya miaka mingi.

Sitaki kutoa siri za watu, lakini kuna watu wa aina hiyo.

Milioni mia mbili si tatizo kwa ninayemzungumzia, lakini ukiambiwa ana miradi yenye thamani ya zaidi ya milioni mia tano hutaamini.
Umeulizwa mtu ana 200m inakuwaje anauliza vitu basic kama hivi?
Kana kwamba haitoshi unasema ana miradi ya 500m yaani ndio unazidi kuleta mkanganyiko.
Mtu ana ndoto ya kuwa na kwake lakini ana 200m hajui ajenge nyumba ya aina gani? Ana miradi ya 500m lakini bado hajui kubajeti 200m apate nyumba na gari. Hebu acheni kuchanganya vijana na stori zenu za mamilioni.
 
Aliipataje hiyo 200m, tuqnze hapo kwanza.
Mkuu, mbona unataka kuchimbua hivyo?

Kwa ufupi ni kwamba ana zaidi ya milioni mia mbili. Milioni mia mbili ndizo alizozitenga kwa ajili ya nyumba na gari.

Alizipataje? Kilimo na madini.
1. Nyanda za Juu Kusini ana mashamba ya parachichi na miti ya mbao

2. Kanda ya Ziwa ana miradi ya dhahabu.

Ilikuwa inasimamiwa na aliowaamini, lakini atakapoacha kazi atakuwa huru kuizungukia kwa ukaribu zaidi.

Kwa kipindi chote alipokuwa katika ajira alikuwa akijijenga kiuchumi. Lakini hata sasa, japo ana "hela" lakini anatumia katika hali ya "ubahili" sana. Hataki kukosea.
 
Kweli utumishi ni umasikini yaani 200m hajui afanyeje?
 
Unadhani ni kwanini watu huwa wana ajiri washauri?
Kwenye issues za uwekezaji inaeleweka. Lakini anunue gari gani kwa bei gani, ajenge nyumba ya bei gani...kwa mtu aliyehustle kuitafuta hadi kufika 200m amepitia mengi na ana uelewa wa mengi.
 
Umeulizwa mtu ana 200m inakuwaje anauliza vitu basic kama hivi?
Kana kwamba haitoshi unasema ana miradi ya 500m yaani ndio unazidi kuleta mkanganyiko.
Mtu ana ndoto ya kuwa na kwake lakini ana 200m hajui ajenge nyumba ya aina gani? Ana miradi ya 500m lakini bado hajui kubajeti 200m apate nyumba na gari. Hebu acheni kuchanganya vijana na stori zenu za mamilioni.
Hajawahi kukutana na kesi kama hizo?

Zipo, ila hashirikishwi kila mtu. Mpaka mtu akushirikishe mambo yake ya ndani sana inategemeana na uhusiano wenu.
 
Hajawahi kukutana na kesi kama hizo?

Zipo, ila hashirikishwi kila mtu. Mpaka mtu akushirikishe mambo yake ya ndani sana inategemeana na uhusiano wenu.
Hii ni chai. Huwezi kutafuta hela hadi upate 500m halafu hujui ujenge nyumba ya bei gani na gari ya bei gani latika bajeti yako ya 200m.
 
Hajawahi kukutana na kesi kama hizo?

Zipo, ila hashirikishwi kila mtu. Mpaka mtu akushirikishe mambo yake ya ndani sana inategemeana na uhusiano wenu.
Nashirikishwa kutoa idea ya biashara ipi kwa kiasi hiki inafaa.
 
Hajawahi kumiliki nyumba wala gari lake binafsi. Kwa zaidi ya miaka kumi aliyokuwa kwenye ajira alikuwa akiishi na kutumia gari la taasisi.

Sasa anataka kuachana na ajira ili asimamie kwa karibu miradi yake. Ametenga milioni 200 kwa ajili ya nyumba na magari mawili.
Hiyo "miradi yake" haihitaji boost ya mtaji?
 
Back
Top Bottom