Nyumba ya kifahari kwa mil 70 ni ipi ?
Kwa mtu kama mimi, nikisimamia ujenzi mil. 70 ninajenga nyumba ya kupendeza sana.
Nyumba hiyo itakuwa na master kubwa, sebule kubwa, jiko, vyumba viwili self contained na dinning room.
Nje kutakuwa na car park, bwawa la kuogelea, bwawa la samaki, banda la mlinzi na fance la nguvu.
Hayo yote nitacheza nayo kwa 50m na 20m iliyobaki ntaipiga decoration ya kufa mtu na kubaki na change.
Ujue mkuu, kwenye ujenzi, simamia mwemyewe na manunuzi ya vifaa madukani usitume fundi wala familia, nenda mwenyewe, maana kwenye manunuzi makubwa ya ujenzi kama huo kuna discount kubwa.
Pia waweza kutathimini katika location ulipo, kama bei za mabati, nondo na saruji siyo ghali sana, ukiona inafaa waweza kuorder viwandani ukaokoa gharama.
Sijaculculate kukuwekea mchanganuo kwa sababu ninaongea kwa uzoefu.
Ila ukitaka, haya yote niliyoongea naweza nikakuwekea hesabu zake vile vile.