Milioni 200 inatosha nyumba na magari mawili?

Milioni 200 inatosha nyumba na magari mawili?

Why awekeze hela nyingi hizo kwenye magari (liability) badala ya kuwekeza?!
Kwanini masafa asitumie public transport km ndege nk, hiyo hela aache kwenye mzunguko, bora hata aweke kwenye T bond, izalishe some amount, awe na gari 1 tu!

Nyumba pia inaweza kusubiri, km siyo lazima hiyo hela ya kujenga azalishe mara 2, halafu ndiyo ajenge.
1. Hali yake ya kifedha inamruhusu kufanya hayo bila kuathiri miradi yake. Ni ndoto yake ya miaka mingi kuwa na "kwake".

2. Gari binafsi litampa uhuru wa kusafiri. Huwezi kutegemea usafiri wa uma kwenye shughuli za machimboni.
 
Hivi inawezekana mtu mwenye 200m bank ashindwe kung'amua hizi basics?
No one knows everything! Binafsi, ninapotaka kitu cha gharama, naweza ninaomba ushauri watu kumi lakini najua mwisho wa siku Mimi ndiye nitakayewajibika kufanya maamuzi.

Mara tu nilipohitimu Chuo, nilishawahi kumshauri Mmiliki wa Kampuni jinsi ya kuendesha biashara yake kwa mafanikio makubwa ilhali mimi mwenyewe sikuwa na ajira. Nilikaa naye ofisini kwake nikawa naongea kama mtaalamu fulani hivi na akawa ananisikiliza. Alifurahia ushauri wangu na akanipeleka kupata lunch. Alitaka hata kumfanya Meneja kwenye mradi mpya aliokuwa alitaka kuuanzisha sema tu hakufanikiwa kuufungua.
 
Hapo fanya hivi before hajaacha kazi
1. Anunue either harrier take la nyani/ Mazda CX5 au Subaru forester 25-35Mil
2. Anunue Toyota hilux/ land cruiser Lx/ Ford Ranger au Nissan Nevara 55- 90mil
3. Inayobaki anunue nyumba
 
Kwahio hivyo ni vitendea kazi vyake katika shughuli zake na wala havina majadala kwahio atafute vya bei nafuu na vinavyoweza kuhimili hizo kazi sababu akinunua ambacho kila siku anashinda garage au hawezi kubeba mzigo wa shamba pia itakuwa tatizo

Again he knows better na issue sio pesa tu bali anachonunua kama ni fit for purpose
✅📌🔨
 
No one knows everything! Binafsi, ninapotaka kitu cha gharama, naweza ninaomba ushauri watu kumi lakini najua mwisho wa siku Mimi ndiye nitakayewajibika kufanya maamuzi.

Mara tu nilipohitimu Chuo, nilishawahi kumshauri Mmiliki wa Kampuni jinsi ya kuendesha biashara yake kwa mafanikio makubwa ilhali mimi mwenyewe sikuwa na ajira. Nilikaa naye ofisini kwake nikawa naongea kama mtaalamu fulani hivi na akawa ananisikiliza. Alifurahia ushauri wangu na akanipeleka kupata lunch. Alitaka hata kumfanya Meneja kwenye mradi mpya aliokuwa alitaka kuuanzisha sema tu hakufanikiwa kuufungua.
Sawa mkuu, naelewa.
 
Hizo hela kaokota? Au kashinda bet?
Milioni 200 halafu analeta discussion za kipuuzi. Mleta mada, muulize kwanza, huyo mtu anaijua mil 200 au anaisikia tu?
Mkuu, kuna watu ukikutana nao na ukaona maisha wanayoyaishi lakini baadaye ukabahatika kuona akaunti zao hutaamini!

Kuna watu wanaoweza kufanya mambo yao kimya kimya, na siku wakiamua kuyaweka wazi ndiyo wengine hukimbilia kusema ni wezi kumbe walianza kuwekeza kimya kimya miaka mingi.

Sitaki kutoa siri za watu, lakini kuna watu wa aina hiyo.

Milioni mia mbili si tatizo kwa ninayemzungumzia, lakini ukiambiwa ana miradi yenye thamani ya zaidi ya milioni mia tano hutaamini.
 
Sasa mbona ana uwezo mdogo sana wa kufikiri?
Basi na amuajiri mtu hapo awe anampa ushauri. Kama ana miradi ya zaidi ya mil 500 hivi kweli hajui kuhusu nyumba na magari?
 
Hajawahi kumiliki nyumba wala gari lake binafsi. Kwa zaidi ya miaka kumi aliyokuwa kwenye ajira alikuwa akiishi na kutumia gari la taasisi.

Sasa anataka kuachana na ajira ili asimamie kwa karibu miradi yake. Ametenga milioni 200 kwa ajili ya nyumba na magari mawili.

Anataka magari mawili kwa sababu miradi yake itamuhitaji kusafri mara kwa mara hivyo anataka gari moja la masafa marefu na gari dogo kwa mizunguko ya mjini.

Ushauri wangu kwake:
1. Atenge milioni tatu kwa ajili ya pango la nyumba kwa miezi sita. Katika kipindi hicho cha miezi sita ahakikishe nyumba yake inakamilika.

Yeye alitaka kuinunua iliyokwishajengwa (kuna inayouzwa milioni tisini) lakini nimemshauri kuwa ya kujenga mwenyewe ni bora zaidi hasa ikizingatiwa kuwa atakapoacha kazi atakuwa na muda mzuri wa kuisimamia kwa karibu.

2(A). Anunue gari dogo (saloon) lisilozidi mililioni thelathini: AUDI, BENZ, BMW, n.k. Akikosa ya bei hiyo show room atafute kwa watu binafsi.

2(B). Anunue gari la masafa marefu lisilozidi milioni sabini. Mashaka yangu ni uwezekano wa kupata gari bora nchini kwa hiyo bajeti, hasa ikizingatiwa kuwa gari lake pendwa la masafa marefu ni LAND CRUISER PICK UP! Lakini sina uhakika kama ataweza kupata "zima" kwa bei hiyo.

Ingelikuwa ni wewe ungemshaurije?
Nimeamini somo la FEDHA ni gumu......
HUKO NI KUTUPA PESA.
 
Huo usimamizi wa miradi yake unahitaji kumiliki nyumba na gari mbili? Cha maana yeye asimamie miradi yake na kuwekeza pesa kwenye huo usimamizi wa miradi (sababu kama maswali haya kwake ni magumu kuyajibu huenda huo usimamizi katika miradi yake ukawa mgumu hivyo awaze mara mbili mbili kuacha ajira yake ambayo mpaka sasa ndio imempatia hizo seed money)

He knows best about his case than me and you...
anaomba ushauri mwingine wewe unaleta mambo ambayo hajaomba ushauri
 
Back
Top Bottom