Milioni 200 inatosha nyumba na magari mawili?

Dah hongera sana kwa kujipata. Ktk harakati zako za kilimo na madini ukiamua kupanua biashara mpka maeneo ya Rukwa, Mbeya, Mpanda na Songwe tuwasiliane naweza pata rizki na mimi. Kuhusu ushauri usiwe na haraka. Wako watu wengi humu wenye uzoefu watakushauri then utafata moyo wako.
 
Aisee bila shaka utakuwa ni wewe umepitia njia hii kuficha
Ndugu yangu millioni 200 kama unafikiria kwanza ndio ukajenge halafu unafikiria magari mawili eti moja la masafa marefu hiyo hela ni shillingi mbili.

Mimi nafanya kazi migodini nina uzoefu usipange malengo makubwa sana kwa hela hiyo kama hujaanza kupata uzoefu.
Hiyo hela ingekuwa tamu kama ungekuwa unastaafu au unaacha kazi lakini una mradi ambao unakuingizia kwa siku angalau hata shs laki moja au hata elfu hamsini.

Hapa migodini hiyo ni hela anayopata mtu ambaye hajastaafu maana migodini watu hawastaafu wanachaga wenyewe kwa kuchoka na unakuta mtu kafanya kazi miaka 10 tu cha ajabu baada ya mwaka au miaka miwili unakuta anarudi kuomba kazi tena ile hela imekwisha ukijaribu kufuatilia alikuwa na malengo makubwa kupita kiasi.
Yuko mmoja alijiingiza kwenye mradi wa kununua ngombe awanenepeshe kisha awauze wale ngombe walikufa wote kwa ugonjwa.
Yuko mmoja alipata tenda kupeleka ngombe Mafia bot lilizama na ngombe wote wakafu jamaa sasa ni marehemu.

Yuko mwingine alinunua hice ikagongwa akawa hawezi hata kutengeneza.
Yuko mwingine alijiingiza biashara ya mbao na magogo kumbe hakujua ni nyara za serikali gari lile lilikamatwa jamaa akaliacha polisi fine aliyopigwa ilimpeleka kuzimu pressure.


Ushauri wangu hiyo hela sio nyingi unavyofikiri unless uliashaanza siku nyingi sio ndio unafikiria kujenga sasa hivyi hebu njoo inbox tupeane ushauri na mimi nimepitia hali kama yako
 
Jenga Kwanza nyumbani, hapa kuna Uzi una bei za kujenga gorofa 75m-85m
 
Itakuwa pengine ni yeye au ndiye anayerun project.
 
Hiyo hela kama ana akili ni ndogo ila kama ni mjinga ni nyingi sana kwanza ahakikishe miradi imesimama kweli ila atafute kluger au harrier kwa ajili ya safari zake ujenzi ni kuzika hela aende nao taratibu sana

Mtaji ndo mambo yote mengine yatawezekana tu
 
Mbona umemshauri vibaya sana?kodi miezi sita milioni 3????
 
Mtu mwenye mzunguko wa million 200 hawezi kuwa na akili za kijinga kama hizi.
Mkuu inaonekana una stress sana za maisha aisee... punguza negativity

Kuna kama mara 2 niliwahi kupost, aisee uli comment as if tunahusama nilikugongea demu wako..... nikaona nikupiuzie tu 😂

Mtu akiuliza kitu anaonekana mjinga, asipouliza akaja kuvurunda mtaanza tena kwanini hukutafuta ushauri?

Kuna memba aliuliza anunue gari gani ya kuanzia maisha mliponda utadhani sijui kafanya jambo gani la kijinga
 
Anunue gari moja la masafa lkn atafute nyumba nzuri anunue lkn kujenga ni gharama sana.mm niliishajenga lkn sikuweza madirisha ,marumaru,rangi imenicost almost mil 38 plus
 
Mleta mada ndio muhusika mwenyewe.
 
Kwa ushauri wangu,gari la masafa marefu anunue Kluger,la misele ya mjini anunue Mazda CX 5 la diesel.Zote hazifiki mil70.

Mil100 ajenge hiyo nyumba.

Atabakia na chenchi ya kutosha tu.
 
Kama ndio kwanza anataka kuanza kufanya hizo shughuli zake kwa mara ya kwanza anatakiwa awe makini sana kwasababu 70% ya biashara zinazoanzishwa from the scratch huwa zinakufa baada ya miaka miwili tu kwasababu ya matumizi makubwa kuliko mapato

Inakua ngumu kushauri kwasababu hatujui ni shughuli gani hizo anazotaka kuanza kufanya zikawana na mahitaji haya

Kama anaanzisha shughuli mbili sehemu tofauti ita msumbua sana, aanze na shughuli moja sehemu moja akomae kwanza hadi itakapo simama kisha aanzishe nyingine, kusafiri na gari ni cost kubwa na risk pia kama hujazoe kudrive masafa marefu na inachosha haraka gari

Land cruiser ni gari nzuri sana lakini kwa biashara zetu za tia maji tiamaji linakua na liability kubwa sana ya mafuta na matengenezao
Nadhani Kluger itamfaa kwa shughuli zote, kuanzia masafa hadi misele ya town

Kama ni lazima apate gari ya pili aangalie Probox ni kagari fulani hivi amazing kwa kazi za mjini mjini

Muhimu kabisa asiache kujenga nyumba hata ya M70 ili mambo yakigoma unakua na kwako

Kwa mahesabu yangu hapo ni chini ya M150
 
mh najaribu kuvaa viatu vya muhusika ila kila nikivivaa najiona mjinga mpumbavu na popoma bora nisivivae kabisa...

kama hajui nn afanye hata usimamizi wa miradi yake ataambulia patupu.
 
Asante nimekupata.
 
Kwa mawazo anayoomba huyo mwenye hiyo milioni 200 anaonekana kabisa sio mfanyabiashara na hafai kuwa mfanyabiashara aendelee tu kuajiriwa.
Hakuna mfanyabiashara anayetumia hela kichwakichwa hivyo.
Na kama ni kweli kuna miradi anaifanya akiacha kazi haitachukua mwaka 1 itapukutika.
Kwanza hajui hata gari zinahitaji nini kwenye matunzo,zina gharama kiasi gani kwenye service anakurupuka kununua mbili kwa mpigo.
Kwa mtu mwenye akili ya biashara angefanya hivi.
1.Anajenga apartment ndogo 4 kwenye compound moja kwa gharama ya milioni 100 na kwenye hizo apartment 4 moja anaishi mwenyewe zingine zinaleta pesa.
2.Angenunua gari moja hata ya milioni 20 yenye fuel economy nzuri aitumie kwenye safari zake zote.
3.Milioni 50 anaingiza kwenye miradi yake ya kibiashara ili ikue zaidi.
4.Itabaki milioni 30 hii itakuwa saving ataamua ahiifadhi popote hata kwenye treasury bonds hapo atakuwa yuko salama kwa muda wa miaka mingi ijayo hatokuwa na stress ya aina yoyote hapo ni kuwa bize tu na miradi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…