Milioni 550 Kujenga Shule ya Sekondari Mufindi

Milioni 550 Kujenga Shule ya Sekondari Mufindi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
SEKTA YA ELIMU KATIKA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI

Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara amekagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mufindi iliyopo Kata ya Ikongosi.

Shule ya Sekondari Mufindi ina Madarasa Nane na ofisi Moja kwa kila Madarasa Mawili pamoja na jengo la utawala (Administration Block), Chumba cha Kompyuta (Computer room/ICT), Maktaba, Matundu 20 (Wavulana Matundu 10 na Wasichana Matundu 10) ya Vyoo vya Kisasa na Maabara ya Kisasa ya Kemia, Fizikia na Biolojia.

Mradi wa Shule ya Sekondari Mufindi umetekelezwa kwa Jumla ya Tsh Milioni 550 ikiwa fedha kutoka Serikali Kuu ni Shilingi Milioni 470 na Fedha kutoka Halmashauri (W) Mufindi Shilingi Milioni 80 pamoja na Nguvu za Wananchi (Benki ya Tofali).

Hadi Sasa Shule ya Sekondari Mufindi imefunguliwa na ina jumla ya Wanafunzi 171 (Wavulana na Wasichana) wanaendelea kupata Elimu. Shukrani za dhati kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan; Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe (Mb); Diwani wa Kata ya Ikongosi Mhe. Negro Sanga na Diwani Viti Maalumu Kata ya Ikongosi Mhe. Magreth Kaguo Kwa kuweza kuwajibika vema katika utumishi wenu katika utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.

#Maendeleo ni Mchakato Endelevu, Maendeleo ni Watu.

Imeandikwa na;
Ndugu Rajabu A. Mpinge
Katibu wa Mbunge Jimbo la Mufindi Kaskazini.
Tarehe 29. 05. 2023.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.27.44.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.27.44.jpeg
    45.7 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.27.44(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.27.44(1).jpeg
    102.8 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.29.35.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.29.35.jpeg
    91.7 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.29.34(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-30 at 20.29.34(1).jpeg
    132.5 KB · Views: 7
Back
Top Bottom