Millard Ayo ana tatizo gani na habari za Upinzani?

Diamond akili nyingi za kuzaliwa
 
Simlaumu milard bila shaka anacheza vile NGOMA inadunda, dw, BBC, voa wamegongeka itakuwa Millard? Milard endelea na mambo yako usiandike habari za majirani.. Mara ghafla usije kudaiwa Kodi ya bilioni 2
 
Mwisho wa haya yote ni October ndugu. Wait and see. Watanzania wa sasa sio wa juzi. Wanaona yote na watatoa hukumu yao baada ya uchaguzi.
Unaota mchana ngoja baada ya 28 Oct utazinduka na utakuja na maneno mengine hapa. Time will talk wala sina haja ya kubishana saaana
 
Kijana huyu baada ya kupata mafanikio kupitia sisi vijana, ghafla ameanza kujisahau. Zaidi ya 90% ya followers wake instagram pamoja na subscribers wake ni wafuasi kindakindaki wa CHADEMA na hilo analijua...
Acheni majungu, Millard kufika hapo alipofika ni msingi wa kujituma yeye mwenyewe binafsi. Ninyi CHADEMA mmemsaidia nini? Kum_follow? Sasa acheni ku_follow halafu muone Kama hataendelea kupata followers.

Rais wa awamu ya sita ni JPM, na kazi iliyoanzishwa lazima iendelee hakuna namna.
 
Kijana huyu baada ya kupata mafanikio kupitia sisi vijana, ghafla ameanza kujisahau. Zaidi ya 90% ya followers wake instagram pamoja na subscribers wake ni wafuasi kindakindaki wa CHADEMA na hilo analijua...
Mbona mnampangia cha kufanya? Sasa tofauti yenu na hao mnaowatuhumu kuminya vyombo vya habari ni nini?
Mmeanza kufanya hivyo bila meno, je! Mkipata mkiota meno?
 
Hivi kweli Kabendera kaufyata! Yuko wapi siku hizi?
 
Hivi kweli Kabendera kaufyata! Yuko wapi siku hizi?
Kaufya mkuu.. Unajua hata kifo cha mzee wake kilikuwa chakutatanisha walisema amejitosa majini lakini kipindi hicho alikuwaga na mgogoro na utawala wakasema siyo MTZ
 
Sio kweli, Tanzania Daima, Mawio, Mwana Halisi ziko wapi. Katika utawala wowote wa kiimla vyombo vyote vya habari vinatakiwa kumtukuza Dictator na si vinginevyo. Period.
Sasa wanaoalamika wanataka Millardayo afungiwe ili ale wapi? yeye siyo mwanaharakati ile kazia anifanya apate ugali yani kibiashara zaidi
 
Hivi Chadema miaka yote hiyo mmeshindwa kuanzisha hata YouTube channel? Kweli nyie ni mazuzu namba moja duniani. Huyo Millard Ayo huwa mnamchangia hata senti 1. Msipende mtelemko nyie
 
Sasa watapigaje mpunga wakiondoa mianya ya malipo ya kipigaji?
 
CHADEMA kwa kweli wametuangusha katika hili. Hivi hayo mabilioni ya 2015-2020 yasingetosha kuanzisha TV ama Radio station?
 
kumlaumu millard ni kumuonea tu kijana wa watu vyombo vya kimataifa vyenyewe vimenyooshewa kidole
yeye akizingua wanaweza kumuita mbele ya kamera na kamwili kake kalivyo kadogo watakachapa bakora tu kama adhabu🤣🤣🤣🤣
 

Kumlaumu leo Millard Ayo ni kutaka Kumuonea tu Mkuu na nadhani hujafanya 'Utafiti' wako vizuri na kwa kina kujua tatizo ni nini. Kama kuna Kipindi ambacho Kwanza Waandishi wa Habari na Bloggers wengi 'wanatishwa' ni hiki lakini pia hapo hapo kama kuna Kipindi ambacho Waandishi wa Habari na Bloggers wengi ndiyo wanapiga 'Pesa' kutoka katika Chama chenye 'Financial Muscle' nchini Tanzania ( kinajulikana na wengi ) ni hiki. Ayo asiwaposikiliza au kujipendekeza Kwao lile Gari lake la Kifahari alilonalo Mafuta utamjazia Wewe? Wale Wafanyakazi wake na ile Nyumba aliyoikodisha kama Ofisi Kimara Kodi utamlipia Wewe? Njia ya kwenda Msalani ( Chooni ) Nyumbani Kwake ikiota Nyasi kwa Wanafamilia wake watakuja Kwako Kula? Acheni 'Unafiki' ili Vyombo vya Habari na Wanahabari wengi wawe Imara wanatakiwa wawe na Uwezo wao wa Kipesa lakini pia Sheria 'Kandamizi' zipigiwe Kelele na Haki iwepo. Nchi nyingi za Kiafrika 'Media' zake huwa 'zinatawaliwa' na Serikali zao husika. Afrika bado sana Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…